Wosia wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
:

MKIONEKANA MNAJENGA NCHI NA KUENDELEA WATAJITOKEZA WATAKAOWAPINGA TENA KWA MAKELELE

Sasa katika mambo haya yakujenga nchi, haya ya shabaha, Shabaha kubwa kama hizi za Kuleta haki zakuondoa dhulma, za kuleta haki duniani mnajipa shabaha kubwa kabisa.

Tunataka kujenga nchi ambayo hakuna dhuluma na safari yake ni ngumu sana.

Na mimi nina hakika kila mtakavyozidi kuendelea huko mtaambiwa kwa makelele huyo huyoo huyoo wale wasiotaka mufike huko watafanya hivyo huyo huyoo huyoo.

Na kila mtakavyo kusogea kila nchi itakavyosogea .... inaonekana kweli ina msimamo, ipo katika njia ile ile na inakwenda kelele zitazidi ... huyoo huyoo wamepotea haoo.

Na mimi nasema kama nazisikia hizo kelele sasa hivi. Kama nazisikia zingine hapa hapa Tanzania, zingine zinatoka nje ya Tanzania haoo haoo wamekosea njia hao haoo wachinje.

Sasa Watanzania Mimi sikubali kuwa Jiwe. Sasa kama ukisema ni uoga potelea mbali lakini kuwa jiwe sikubali hata kidogo, sigeuki nyuma maana ama tulikusudia kweli ama tulitania? Ama tulikusudia kweli kujenga nchi ya haki ama tulikuwa tunatania tu?

Sasa kama tulikusudia hatuwezi tukarudi nyuma kwa kelele za wapumbavu na wanyonyaji tutakwenda tu!

Tutapata matatizo, tutapata majizi humu humu, tutapata wanyang'anyi humu humu, tutapata watetezi wa mabepari humu humu, watazidisha kelele lakini tutakwenda wanaotaka kugeuka mawe geukeni.

#NiKusongaMbeleTu
#HapaKaziTu
#WasiotakaWatatukuta
 
"......tunataka raisi anayeuchukia ukabila......", "......mnaulizana makabila, mnataka kutambika...?"
 
Back
Top Bottom