Wosia kwa vijana mashuleni na vyuoni na wazazi wanobeba gharama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wosia kwa vijana mashuleni na vyuoni na wazazi wanobeba gharama

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Jatropha, Sep 23, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sehemu ya Tatu ya Kifungu ya cha 11 kinasema kuwa “serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo vya mafunzo”.
  Itakumbukwa kuwa wakati Serikali ya Hayati Mwalimu Nyerere ikitoa huduma za Elimu, Afya, Maji Safi n,k bure kwa wananchi wote bila ya ubaguzi wala matabaka, ilikuwa ikichimba aina moja ya madini tu nayo ni Almasi katika mgodi wa Mwadui.
  Madini mengine kama vile Dhahabu, Tanzanite, Uranium, Gesi n.k yalivihifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo kwa kuwa Mwalimu Nyerere alitambua Serikali zitakazofuata zitakuwa na changamoto ya ongezeko la watu watakaohitaji huduma hizo.
  Wakati Serikali ya Mwalimu Nyerere ikitoa kutoa huduma hizo bure ilikuwa ikipokea kiwango kidogo au kinacholingana kinachopokelewa na Serikali zilizofuata hadi sasa. Lakini Serikali ya Mwalimu ililazimika kugawana rasli mali ilizokuwa nazo na harakati za ukombozi katika nchi za Kusini mwa Afrika na kwingineko kama vile Msumbiji, Angola, Namibia, Zimbabwe na Afrika ya Kusini ambazo kwa hakika Tanzania ilikuwa ikitoa mchango mkubwa sana. Kwa kuwa jukumu hilo limekamilika ni wzi kuwa rasli mali zilizokuwa zikielekezwa huko zilipaswa kutumika kuwaendeleza watanzania na sio wawekezaji kutoka nje

  Kwa kuwa idadi kubwa ya vijana ndio kwanza wanapata umri wa kuanza kupiga kura mwaka 2010, au mapema kidogo. Na Kwa kuwa vijana hawa toka wapate uelewa walikuta Serikali ya Tanzania chini ya CCM ikitekeleza Sera za Uchangiaji huduma za Jamii kama vile Elimu, Afya, Maji Safi., hivyo hawafahamu ama hawajawahi kupata uzoefu wa namna huduma hizi zilivyokuwa zikitolewa bure na Serikali iliyokuwa ikiongozwa na Marehemu Baba wa taifa Mwalimu Nyerere.
  Hivyo ni vyema baadhi yetu tulioshuhudia wananchi wa Tanzania wakipatiwa huduma hizi bure bila ya ubaguzi wa aina yoyote wala matabaka / ama akunufaika; tukawapatia uzoefu huo ili kuwathibitishia vijana kuwa suala hilo limo ndani ya uwezo wa Serikali ya Tanzania endapo umakini na utashi utakuwepo.
  Maelezo ambayo tunatakiwa kushare na vijana hawa ni pamoja na:-

  a) Mazingira ya shule, vyuo yalikuwaje ikilinganishwa na mazingira ya shule za serikali za sasa? Wanafunzi wa shule na vyuo mbali mbali kutokea miaka ya tisini hadi sasa tusaidieni hali ya sasa ilivyokuwa/ikoje.
  b) Wanafynzi walikuwa wakisafiri kwa gharama za nani kutoka majumbani hadi mashuleni, vyuoni na kurejea majumbani wakati wa likizo.
  c) Mazingira ya mabweni, chakula katika hizo shule na vyuo vilikuwaje ikilinganishwa na shule na vyuo vya sasa.? Wanafunzi wa shule na vyuo wa kutokea miaka ya tisini hadi sasa tusaidieni hali ya sasa ilivyokuwa/ikoje.

  KARIBUNI SANA TUWAPATIE VIJANA WETU MWANGA

  JASUSI AMECHANGIA
  Wakati Jaji Mfalila akiwa sekondari mimi nilikuwa middle school. Tulipewa vitabu, peni na waliokaa mabwenini chakula kilikuwa bure. Wakati shule zinafungwa tulipewa warranti za kupanda treni/meli/mabasi kwenda nyumbani vijijini na kurudi. Pale shuleni kwetu waalimu walikuwa na nyumba nzuri, jioni tukienda kwao kusikiliza redio. Kila mwanafunzi alikuwa na dawati lake. Of course chakula cha shule ni cha shule tu. Tulikula dona na maharage, halafu wikendi tunapewa wali na nyama. Shule nyingine nasikia, kama vile Bwiru, walikuwa na chai na mkate saa kumi jioni. Nadhani hilo jibu linakupa picha ya kutosha.
  JASUSI-NAKUSHUKURU SANA UNAWEZA KUTUPATIA MIFANO MIWILI AU MITATU HIVI ILI VIJANA NA WAZAZI WAO WAAMINI KUWA ULIKUWA UKIPATA HUDUMA HIZO BURE.
  KUNA MZEE MMOJA KANIAMBIA KUWA KWAO NI MUSOMA NA SHULE ILIKUWA BUKOBA. WANAFUNZI WOTE WANAOKWENDA BUKOBA WANAPATIWA WARANTI MUSOMA KWA DC, NA KUPOKELEWA KWA DC MWANZA ASUBUHI, WANANULIWA MIKATE NA MAZIWA NA KUPATIWA WARANTI YA MELI KWENDA BUKOBA.
  JIONI WANAFUNZI WOTE WANAOPANDA MELI KUTOKA MIKOA MBALI MBALI WANABEBWA NA MABASI KWENDA BANDARINI KUPANDA MELI- ANASEME ALIKUWA ANAJISIKIA KUWA MTOTO NI MALI YA SERIKALI KWA JINSI WANAFUNZI WALIVYOKUWA WAKIHUDUMIWA NA WAKUU WA WILAYA KILA WANAPOPITA. WEWE JE ILIKUWAJE? CHANGIA
   
 2. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  mzee mmoja aliyesoma chuo kikuu cha dar es salaam miaka ya sabini anasema kuwa mwanachuo wa wakati ukitoka shule za mikoani ndio ulinzia kujifunza ustaarabu hapo mlimani, chakula kilkuwa ni cha kiwango cha mahoteli ya kitalii.
   
Loading...