Worldwide: Unafikiri ni nadharia zipi ama vitu vipi tulilaghaiwa..?

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,175
56,767
Sio katika misingi yote dunia imekuwa ikiongozwa katika usahihi!,zipo taarifa ambazo zimekuwa zikileta utata na imekuwa hivyo kwa makusudi ya watu fulanifulani.

Zipo nadharia, taarifa na imani katika misingi yote ambayo kwako inawezakuwa ni taarifa aidha unamashakanayo ama unahakika kabisa ulipigwa/tulipigwa na kitu kizito kisogoni!.
Inawezakuwa siasa,imani,maswala ya uchumi n.k

Binafsi nafikiri vipo vitu binadamu tumehadaiwa na kundi la watu fulani na bado vyengine vinafanya kazi!,vitu hivi vimeegama katika makundi Kama ifuatavyo.

Siasa.
Kwa mtu aliekuwa kufikra anaelewa dhahiri hii nyenzo ina nguvu kiasi gani.. nikianzia hapahapa nyumbani back in days 2015,katika harakati za uchaguzi baada ya mbilinge mbilinge za huku na kule na kukatana majina katika chama cha ccm.
Moja ya mtu aliekuwa akitazamiwa kwa kina kuwa angepewa nafasi ya kugombea lakini mambo hayakwenda sawia!,hivyo alijikuta akikosa nafasi hiyo na kuamia chama pinzani!. Kuhamia haikunipa tabu isipokuwa ktk chama hicho miaka ya nyuma walimpinga bwana huyu ya kuwa ni fisadi lakini mara hii walimkubali na kumpa nafasi nyeti ya kugombea urais!.
Yakawa ya kuwa na baada ya muda mhusika alirudi alipokuwa huku akitoa kauli "narudi nyumbani"..😃
Hili tukio lilifanya nianze kuangalia siasa kama michezo michezo ya kilaghai sana na tunaochezewa michezo hii ni sisi wananchi!.

Chaguzi za marekani.
Hili taifa ni kubwa katika nyanja za kiuchumi,kiuongozi na kijeshi pia. Ni moja kati ya taifa linalohubiri demokrasia,ndio wamejidadavua katika nyanja hii lakini pia sidhani Kama huwa rais wao wanamteua kidemokrasia!.
Vyama vyao viwili vikubwa ndio vimekuwa vikitoa marais,sikatai lakini kwa jinsi mchezo ulivyo naona kama hili ni jambo la kuchoresha tu kwa watu ili ionekane vile inavyotakiwa kuonekana!. Nachoamini lipo kundi lililojichimbia vilivyo ambalo ndio husimamia dira ya taifa na nani awe au asiwe kiongozi wa taifa hili adhimu!.. baadae ndipo wanapelekewa watu wamchague yupi ila kati ya hao wote wameshachaguliwa na wakupita anafahamika na atapita kwa vyovyote tu!..😅
Nafikiri hili hufanyika kwaajili ya ulinzi madhubuti wa taifa hili.

Kifo cha Osama.
Wapo wanaoamini kuwa Osama bado hajafa na ni mshirika wa marekani!,ya kuwa hivi sasa anakula maisha baada ya kumaliza ujira wake!. Kwangu napata ugumu wa kukubaliana na hili zaidi nikiangalia bwana huyu alivyoifanya marekani katika siku ile ya sep 11..!

Kumruhusu huyu mshikaji kuwa mshirika wa marekani hakunipi mantiki kwani ni sawa na kumpa mamlaka mtoto achezee hata kiini cha jicho lako huku akiwa ameshika wembe!..
Twafahamu pentagon ni jengo linalotumika Kama kitovu cha shughuli za kijeshi kwa marekani,Sasa mbali na majengo mengine aliyopiga ikiwamo na ubalozi wa marekani hapa nchini.. bwana huyu alipiga pia jengo hili la pentagon!.
Hata Kama ni mshirika ndo akushike hivi sharubu..?😂
Hii si hatari ya nchi kabisa!.
Naamini kwa marekani mtu huyu waliemtafuta kwa udi na uvumba na hatimae kumpata walimfyekelea mbali!.

Japo tukio hili sifagilii ila naamini walimlaza pale walipohitaji na kwa vurugu za yule jamaa Kama angekuwepo angekuwa amesharudi na kutoa dozi kwa mtesi wake!.


Uchumi.
Hapa tunakutana na ma master wengine ambao wanajua kuchezesha shekeli vizuri mpaka unaingia mkenge nakuwa chini yao!.

Kwenye hili nitaligusia zaidi bara letu haswa linavyohadaika na mikopo toka nchi zilizoendelea!.. sisemi kuwa mikopo ni mibaya hapana isipokuwa ipo mikopo ambayo ukiingia kuchomoka lazima uliwe hili nafikiri hata mifano tunayo Kuna nchi huko imeachia kiwanja chake cha ndege kiwe controlled na nchi fulanifulani kisa mikopo..!

Forex.. kwenye swala la uchumi hii ndio biashara yenye mzunguko zaidi,sipingi kuwa ni real lakini nje na kwamba utaifanya biashara hii kwa signals fulanifulani pia ujue kucheza na walioshikilia biashara hii!.. ipo michezo inaweza kuchezeshwa makusudi ama mtu mkubwa ama nchi wanaweza fanya jambo fulani ili kufanya soko pia licharuke..😃

Michezo kwenye biashara hufanyika hata kwenye hizi biashara physical.. kwa hapa kwetu wakati ule sukari iliposimama mpaka kufikia 5000 hadi 6000 tzs,kwa baadhi ya maeneo naamini hapa kuna jambo lilifanyika makusudi kwa wafanyabiashara wenyewe ili kufanya walichokitaka..! Wenyewe tunasema mambo ya kimchongo..😂

Back in days kuna tukio lilishasimuliwa humu na moja wa nguli wa uandishi,ambapo kichwa kimoja kiliamua kiichezee nchi hadi kuleta kanyabazonngo isiyokifani!.
Link... Nguvu ya Biashara ya Forex, Ujasusi na yaliyo nyuma ya pazia

Katika swala la uchumi kuna wafanyabiashara wakubwa ambao hawataki biashara zao zife,hivyo katika namna yoyote hawapendi kuona kitu pinzani kikija na kuua biashara yao mfano moja ya nguli wa maswala ya umeme Nikola tesla,aligundua njia ya kuweza kusambaza umeme pasipo kutumia nyaya!.. lakini ni mfanyabiashara gani wa nyaya angekubali hili lije tu!.

Hata alipogundua umeme wa maji alipingwa vikali japo wazo hili lilipita na mpaka leo watu wanafaidika na wazo lake!. Inasemekana makabrasha mengi ya huyu mwamba baada ya kifo chake ambacho nacho kilikuwa tata!, makabrasha yake mengi yalidhibitiwa na wale vipepeo weusi wa USA!.

Inaendelea...
 
Kila mtu kujiona anaangalia juu wakati kuna wengine upande wa pili wa dunia huko kwa chini. Maelezo yake pale mpaka utulie kweli kweli
 
Yote uliyoandika hapa ni debunked conspiracy theories tupu.
 
Kuambiwa Mungu alimtoa mwanaye wa pekee atufie Msalabani ili tusamehewe dhambi zetu wakati mtenda dhambi mwenyewe Shetani yupo ahhhh nachoka kabisa

Kuambiwa katika Biblia kuwa Mungu alimuumba Shetani halafu akaja kumuasi na tunaambiwa yeye aijua kesho yetu tangu tupo kwenye viuno vya baba zetu mimi nimegoma kusadiki. Ina maana hakujua kuwa shetani angekuja kumuasi!?

Kuambiwa kuwa Mungu aliziumba Mbingu na Dunia kwa siku sita tena kwa kutamka ili hali sasa hivi huku kwetu ni asubuhi, kwingine ni usiku ama kwingine ni mchana, hapana kwakweli.

Kwenye kitabu cha Ayubu yule mtu wa Usi, kinasema Mungu alimuuliza Shetani atokako ajamjibu ametoka kuhangaika huko Duniani na akamuuliza kama amemuona mtumishi wake Ayubu aliyemkamilifu. Kumbe Mungu na Shetani ni washkaji huwa wanapiga stori!?


Mjukuu wangu, nachoka kabisaa niko Hoves(in her voice)
 
Dini Dini Dini!kuna sehemu tunaumizwa Sana!!nadhara ya MUNGU na utendaji KAZI na utoaji fedha kama sadaka!!!Moja ya jambo limeumiza wengi Sana AISEH!!!
 
Back
Top Bottom