World Military Geniuses Of All Time

14. William Wallace
15. Frederick Barbarossa
16. ...
17. MWANAMALUNDI
18. FIELD MARSHAL IDD AMIN DADAA
19. MAJOR GENERAL WALDEN -from Iringa -Tanzania
20. Lt. GENERAL PETER SILAS MAYUNGA From sukuma land in Maswa District
21. MILAMBO
22. ISIKE
23. MKWAWA
 
Maana genius ni nini? Siyo walio wengi walikuwa wahalifu waliochukiwa na wadharauliwa na wengi? Maana walileta kifo na uharibifu tu...

Wengi wao walikuwa wezi wakubwa tu, kama ni Napoleon au Shaka Zulu.
Naweza kuheshimu hao waliotetea nchi yao dhidi ya wengine , naheshimu zaidi hao ambao walizuia vita kwa kuonyesha nguvu na ujanja.
Kidogo nawaheshimu waliofaulu kutawala wanajeshi wao na kuwadhibiti wasipore, wasiibe, wasiwe wabaka, wasichinjechinje tu....

Ila tu wengi wa hao hawakuweza.
 
Orodha yangu binafsi ni hawa jamaa:

1. HANNIBAL BARCA.
- Huyu jamaa alipigana vita kwa zaidi ya miaka 10 kwenye nchi ya wenzake bila kushindwa na bila kupokea majeshi kutoka nchini kwake (Reinforcements) kwa muda mrefu mno. Uwezo wake wa kutumia ulaghai na kustukiza ilimfanya awapige Waroma hadi kuwafanya wakimbilie kwenye kufanya kafara za binadamu. Umahili wake wa kupigana vita nyingi zanye mafanikio kwenye eneo la adui mwenye nguvu kama Roma nadhani hauwezi kulinganishwa na majemedari wengine dunia.

Wanahistoria wanasema hakuna Jemedari wa vita ambaye alikuwa anafahamu matumizi ya Intelijensia ya kiraia na ile ya jeshi kama Hannibal. Maana inasemekana kitendo cha yeye kuweza kulifahamu eneo la adui lilitokana na kuweza kujaza majasusi wengi kweny jeshi la Roma na wengine hadi Roma kwenyewe kwenye vyombo vya kisiasa. Alikuwa pia ni mtaalamu wa propaganda kiasi kwamba aliweza kuwavuruga Waroma na kusababisha wasiliamini jeshi lao.

Baada ya vita ya Ziwa Trasimene, ambapo walikufa wanajeshi zaidi ya 20000 wa Roma ndani ya masaa machache. Hannibal alikata vidole vya wanajeshi wa Roma akatoa pete za watoto wa familia tajiri halafu akazituma nchini kwake Karthago ambapo zilikuwa nyingi na zikamwagwa nje ya mlango wa bunge lao. Hili lilisaidia sana kukuza morali ya wakarthago na kudidimiza morali ya Waroma. Mpaka leo huwa sielewi kabisa ni kwanini Roma walishinda ile vita.....

2. JULIUS CAESAR
- Huyu aliweza kufanya jambo ambalo ni wanajeshi wachache wana uwezo wa kufanya. Mbali na kuwa mwana mkakati mzuri, huyu jamaa alitumia dini, ujasusi na siasa katika kushinda vita zake. Ukianza kufuatilia vita zake alizopigana kule Gaul na Uingereza utatambua haraka sana alikuwa ni mtu mwenye uwezo wa hali ya juu sana. Alikuwa akikamata wanajeshi wa Gaul anaanza kuwahoji mwenyewe kuhusu mbinu zao na mikakati yao: Kuanzia imani zao za kishirikina na tamaduni zao halafu anapata pa kuanzia.

Kitendo cha kumshinda baba mkwe wake Pompey ambaye alikuwa ni mwanajeshi mkongwe aliyeshinda vita nyingi sana na kuheshima Roma kote ni kitu ambacho kinafikirisha. Pompey alikimbia Roma akamwacha Julius Caesar na ushindi lakini alihakikisha kwamba Misri ambayo ndiyo kitovu cha utajiri wa Roma haiwi chini ya Caesar. Lakini Julius Caesar aligeuza meza wakati ambao hakuna aliyetegemea angeshinda.

Akiona anazidiwa kwenye vita alikuwa anatumia diplomasia, dini, rushwa na ulaghai. Kuna sehemu hadi alishawahi kukiri na kumwambia mama yake kwamba nimetumia rushwa sana hadi kufika hichi cheo cha Kuhani Mkuu wa Roma "The Pontifex Maximus". Baada ya kuvuka mpaka wa Rubicon aliamua kutuma ujumbe kwa Pompey kwamba Pompey akijiudhuru na yeye angejiudhuru, lakini Pompey alijua jamaa amemwekea mtego.

3. SUN-TZU
- Huyu ufahamu wake kuhusu vita umeiachia dunia urithi mkubwa mno na unaelezea kwamba alikuwa ni mtu wa aina gani. Mbinu zake za kivita zilitumika sana na wanajeshi wakubwa nchini Uchina kama Cao-Cao ambaye alikielezea vizuri (Made a Commentary) kile kitabu cha Art of War katika lugha rahisi inayoeleweka. Sun-Tzu namfananisha sana na Carl Von Clausewitz ambaye aliandika kuhusu mbinu za kivita ambazo zilitumiwa sana na majeshi ya Ulaya.

4. NAPOLEON BONAPARTE (The Corsican Devil)
- Huyu aliiga mkakati wa Hannibal wa kuvuka milima ya Alps ili kuwatandika adui zake kwa kuwastukiza. Napoleon amepigana vita nje ya Ufaransa kwenye maeneo ambayo ni hatari kama Misri ambako ni jangwa, na kuna watu hatari kama Mamluki ambao kwenye The Battle of Pyramids alifanya kitu cha ajabu na kuwatandika mno. Hawa Mamluki ikumbukwe ndiyo waliowatandika Mongols kwenye vita vya Ain Jalut (The Battle of Ain Jalut). Kwenye The Battle of Waterloo mwaka 1815 alichangiwa na mataifa sita makubwa yenye wanajeshi wengi lakini aliwasumbua sana. Halafu vita vilivyokuwa vikali Napoleon alinukuliwa akisema maneno haya huku akifurahi "Hii vita ya leo ni nzuri sana"

5. RUSTAHAN SUREN (Surena)
- Huyu alikuwa ni moja kati ya wanajeshi wa Uajemi aliyedhihirishia dunia kwamba Roma ya Kale ilikuwa inapigika kama mataifa mengine. Crassus alipeleka majeshi mengi kule Uajemi ili aweze kupata ushindi kama wenzake Pompey na Caesar. Haya majeshi aliyoyapeleka kule yalikuwa yana vikosi vya Praetorian Guard ambao walikuwa wana uwezo mkubwa sana wa kupambana. Lakini sasa bahati mbaya sana jeshi la Roma halikufanya utafiti wa kutosha juu ya adui wao kama ambavyo adui wao alifanya utafiti juu ya Roma.

Surena alipogundua kwamba jeshi la Roma lina nguvu sana alikuja na mbinu ya kutumia mishale tu. Jeshi la Roma lilivyofika lilijikuta limezungukwa ndani ya miduara mitatu ya adui. Mduara wa kwanza ulikuwa umejaa wapiga mishale (Archers), mduara wa pili umejaa wapiga mishale ambao wanapokea endapo ule mstari wa kwanza umechoka na mduara wa tatu ulikuwa ni wa wanajeshi wanaoleta mishale kwa ajili ya haya maduara mawili.

Roma waliweka ukuta wa ulinzi lakini Waajemi wakawa wananyesha mvua ya mishale ambayo ilifika muda ukuta wa ulinzi ukaharibika na wakaanza kufa wanajeshi wengi wa Roma. Walipigwa sana Waroma na Surena aliwazunguka pande zote ili washindwe kukimbia. Alipigana vita na adui mkubwa sana bila kutumia nguvu nyingi bali akili.

Cc: zitto junior , Chige , Wick hebu piteni huku...
 
Safi
 
Erwin Rommel

huyu Wamarekani wanamjua, hali kadhalika Waingereza wanamjua

Huyu bwana Akiwa na Silaha duni za kiitaliano katika vita kuu ya pili ya dunia alikuwa anawaburuza Kundi la wamarekani,Waingereza,Wafaransa kwamuda mrefu na akiwa anatumia silaha duni na zana chache

Shujaa Erwin Rommel hata waliowachukia Wajerumani licha ya kuwa Rommel ni mjerumani ila walimpenda Rommel
 
Narudia: ujisomee kabla ya kuandika! Rommel aliongoza kikosi cha Wajerumani dhidi ya Waingereza pekee pale Afrika Kusini - Lybia 1941-Mei 1943. Hajapigana na Wafaransa (walioshindwa tayari 1940 kabla ya wakati alihusika Lybia) . Alifaulu kwa muda didi ya Waingereza (Waingereza, Wahindi, Waafrika Kusini) kabla ya kushindwa pale El Alamein.
Wamarekani hawakufika bado Afrika, aliwakuta 1943 mwishoni tu, wiki chache kabla ya kuondoka Lybia na kurudi Ulaya. Katika vita ya 1944 baada ya uvamizi wa Ufaransa na Allied Forces hakushinda Marekani, kinyume chake.
Pale Lybia alikuwa na faru za Kijerumani, akiwa mkuu wa vikosi vya Italia pia.
 
Yomi Netanyau

Dreyfuss

Paul kagame,

Mansa kan kan Musa.

Ganga zumba

Jakaya Mrisho kikwete, M23 abolished, Seychelles coup attempt

King Makama Malumbo -Mugango/ Bwai people

Mkama commander in chief Manyonyi -Kerewe/ Mwibara People.

Mohamed farah ahdeed-Somalia.

Milambo Tabora
 
Umewahi kumsikia General "Khalid bin Walid" wewe?
Mgoogle huyo mtu, Mtume Muhammad alimuita "The Sword of GOD“ hajawahi kushindwa vita huyo, na Empires mbil kubwa za Wakati wake Byzantine na Persia zilianguka huku yeye akiwa ni Commander wa majeshi yaliyoziangusha!
 
Narudia: ujisomee kabla ya kuandika! Rommel aliongoza kikosi cha Wajerumani dhidi ya Waingereza pekee pale Afrika Kusini - Lybia 1941-Mei 1943. Hajapigana na Wafaransa (walioshindwa tayari 1940 kabla ya wakati alihusika Lybia) . Alifaulu kwa muda didi ya Waingereza (Waingereza, Wahindi, Waafrika Kusini) kabla ya kushindwa pale El Alamein.
Wamarekani hawakufika bado Afrika, aliwakuta 1943 mwishoni tu, wiki chache kabla ya kuondoka Lybia na kurudi Ulaya. Katika vita ya 1944 baada ya uvamizi wa Ufaransa na Allied Forces hakushinda Marekani, kinyume chake.
Pale Lybia alikuwa na faru za Kijerumani, akiwa mkuu wa vikosi vya Italia pia.

Unasema Ufaransa hakuwa........

Ufaransa walipewa zone occupation kule Ujerumani vita inaisha na walishiriki kuivamia Ujerumani mwishoni mwishoni mwa vita

Rommel alipewa command ya ile vita Afrika ya kaskazini ingawa operation ilikuwa ni ya Muitaliano huju mjerumani akiwa kaenda kusaidia tu na ndio maana Zana zilitumika za Muitaliano

Zana za muitaliano zilikuwa zana duni kabisa katika vita ya pili ya dunia: mfano mizinga ya muitaliano baadhi yake ilikuwa inadondosha mabomu ambayo hayalipuki
 
Ushauri ni daima kujisomea kabla ya kuandika! Ufaransa ulishindwa mwaka 1940. Nusu ya kaskazini pamoja na Paris ilitawaliwa moja kwa moja na jeshi la Kijerumani, nusu ya ksini iliendelea chini ya serikali ya jenerali Petain aliyewahi kutia sahihi mkataba ya kusalimisha amri, lakini kwa kufuata maagizo wa Wajerumani (kama kutesa Wayahudi). Pale Uingereza wanajeshi (hasa wanamaji na wanaanga) na wanasiasa Wafaransa waliowahi kukimbia waliunda serikali ya "France Libre" (Ufaransa huru) chini ya jenerali De Gaulle. Makoloni ya Ufaransa katika Afrika yaliamua kufuata amri za jenerali De Gaulle, zile za Vietnam ziliendelea upande wa Petain. Katika Afrika ya Kaskazini makoloni yaligawiwa. De Gaulle alikaribisha Wafaransa wote waliokaa nje ya Ufaransa-Ulaya kujiunga na jeshi lake la "France Libre".

Wamarekani walipovamia Afrika Kaskazini mwisho wa 1942, Wafaransa wengi waliwahi kuwa chini ya Petain walihamia upande wao na upande wa De Gaulle. Hivyo vikosi kadhaa vya jeshi la France Libre vilipigana 1943 pia na Wajerumani na Waitalia pale Tunis.
Wakati Waingereza na Wamarekani walivamia Italia 1943, jeshi la France Libre walikuwa tayari na askari lakhi 1 hivi; zaidi ya nusu askari Waafrika na Wamoroko, wengine Wafaransa waliowahi kuishi nje ya Ufaransa 1940 au walioweza kukimbia.

Hadi Uvamizi wa Normandi 1944 jeshi la France Lbre iliongezeka zaidi, na kadri Wajerumani (mwanzoni chini ya amri ya Rommel aliyekuwa mkuu wa jeshi la kijerumani Ufaransa baada ya kukimbia kutoka Afrika) walivyorudishwa nyuma, Wafaransa wengi walijitolea kuingia katika jeshi la France Libre. Majeshi ya Ushirikiano yalipokaribia Paris, De Gaulle alihakikisha ni vikosi vya kifaransa vilivyoingia kwanza mjini.
Hivyo katika mapatano kuhusu ugawaji wa Ujerumani baada ya vita, pia Ufaransa ilipata kanda la utawala wa kijeshi katika Ujerumani maghrib-kusini, pamoja na kanda mojawapo katika Berlin.
 
Back
Top Bottom