Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 528
Michuano ya AFCON 2010 inayoendelea kule Angola imeanza kuwa na msisimko mkubwa hasa baada ya michezo ya pili kuanza. Macho ya Wa-Afrika wengi inaziangalia timu za Ivory Coast, Ghana, Nigeria, Algeria, na Afrika Kusini (Bafanabafana) ambayo haimo kweny fainali hizi na hivyo kutukosesha washabiki wa soka kupima uwezo wao na nafasi yao kwenye kombe la Dunia 2010.
Tujadili timu za kwetu Afrika ambazo zinaweza kufanya maajabu kwenye Kombe la Dunia la FIFA 2010. Maoni yangu ni kuwa Ghana na Ivory Coast ndizo timu za Afrika ambazo nategemea zitafanya vizuri kwenye Kombe la Dunia 2010. Hata hivyo pamoja na kufungwa leo na Ivory Coast kwa mabao mengi, binafsi nimeridhishwa sana na uwezo wa Black Star na kwa kweli naiweka kwenye nafasi ya kufika mbali kulinganisha na timu nyingine za Afrika. Nimezipanga timu za Afrika kwa ubora na uwezo wa kufika mbali kwenye FIFA World Cup 2010 kule Bondeni kwa Madiba kama ifuatavyo:-
1. Ghana (Black Star); timu yenye uchu wa kufika mbali ambayo imesheheni wachezaji wakongwe na vijana ambao wanacheza kwa uzalendo wa hali ya juu kulinganisha na Wawakilishi wengineo wa Afrika.
2. Ivory Coast (The Elephant); timu nyingine ambayo wakiamua kwa dhati kucheza na kuweka u-super star wao pembeni basi watatuwakilisha vema.
3. Nigeria (Super Eagles); timu yenye wachezaji wenye viwango vya hali ya juu duniani lakini wenye nyodo na wasio na uzalendo kwa Taifa lao na Afrika. Hawa wakiweka kando ubishoo na kuamua kupiga soka basi ndiyo watabeba matumaini yetu Waafrika kuliko timu nyingine yoyote.
4. Afrika Kusini (Bafana bafana); hawa kweny michyuano ya FIFA Confederation Cup walikuwa na timu changa ambayo inaweza kufanya maajabu kwenye Kombe la Dunia kuliko Algeria.
5. Algeria (Desert Warriors?); hawa jamaa nimeshindwa kuwaelewa kabisa na siwategemei sana, afadhali Misri wangepenya badala yao matumaini yangu yangekuwa makubwa lakini kwa jinsi wanavyocheza kwenye AFCON 2010 naona kama vile hamna kitu.