World Bank to officially declare Tanzania a Middle Income Country (MIC) on July 01, 2020

Cicero

JF-Expert Member
Jan 20, 2016
2,915
2,000
The World Bank is to officially declare Tanzania a middle income country as of 1st July 2020. Jumuiya ya Afrika Mashariki sasa inakuwa na mataifa mawili kwenye kundi la MICs.

Swali: Itakuwaje kuhusu East African Community - European Union Economic Partnership Agreement? Maana Tanzania iligoma ikiamini kwamba italindwa na ile special arrangement kwa nchi maskini. Yetu macho!
Hongereni watanzania!

1593495793335.png
 

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
2,882
2,000
Hakuna kitu hicho. Unawajua GAVI na Global Fund? Nchi za uchumi wa kati km Botswana hazipati msaada wa GAVI Alliance na Global Fund. Lakini huwa hawakati mara moja. Wanakuachisha taratibu kama mama anamwachisha mtoto kunyonya.
Kenya ni middle income mkuu ila still wanapewa misaada sana! Pengine kuliko sisi.
 

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
13,506
2,000
Wana jf

Hiki ndio kishindo kikuu cha awamu ya tano kufika uchumi wa kati (middle income country ) M.I.C .

Ambapo benki ya dunia itaitangaza Tanzania kuwa inchi ya uchumi wa kati kwa kufikia GDI per capital ya U.S. $1026-12476

So kuanzia siku hiyo ule msemo wa sisi sio maskini wa rais magufuli utakuwa bayana


USSR View attachment 1489538

Mkuu haya mambo hayataki haraka wala papara,yafaa ujitulize halafu utafakari kwa kina.

Kenya ina uchumi mkubwa kuliko Tanzania lakini mpaka kesho uchumi wake Kwa mujibu wa takwimu za WB wapo katika kundi la lower middle income.

South Africa Higher middle income sasa sijui Sisi tumo kundi gani !.
 

mculture3

Senior Member
Feb 24, 2017
118
250
Wana jf

Hiki ndio kishindo kikuu cha awamu ya tano kufika uchumi wa kati (middle income country ) M.I.C .

Ambapo benki ya dunia itaitangaza Tanzania kuwa inchi ya uchumi wa kati kwa kufikia GDI per capital ya U.S. $1026-12476

So kuanzia siku hiyo ule msemo wa sisi sio maskini wa rais magufuli utakuwa bayana


USSR View attachment 1489538
Source ni kama hili jambo lilitokea Kitambo huko, back in 2018
IMG-20200626-WA0069.jpeg
IMG-20200626-WA0070.jpeg
 

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
4,714
2,000
Ukubwa unakuja na changamoto, hii mambo ya kuitwa Lower middle Income bado ni matusi ingawa ni hatua nzuri. Vipi kuhusu Ghana mbona siioni hapa.
 

Cicero

JF-Expert Member
Jan 20, 2016
2,915
2,000
East African Community - European Union Economic Partnership Agreement. Inahusu nini?
Ni mkataba flani ivi ulikuwa unabuniwa kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya. Ungelazimisha pande zote mbili kufungua masoko yao na kuruhusu bidhaa kuingizwa kutoka upande wa pili bila kodi/tozo. Kati ya watu waliokuwa mstari wa mbele kupinga ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu mzee mkapa. Alisema kuruhusu bidhaa kutoka Ulaya kuingia Tanzania bila kodi kutaua viwanda vya Tanzania.

Salama ya Tanzania ni kwamba ilikuwa nchi maskini (Low Income Country), kwa hiyo ingeruhusiwa kuingiza bidhaa zake Ulaya ata kama ingegoma kusaini mkataba. Kenya ni nchi ya kipato cha kati na wao ndo wangeumia zaidi. Swali langu limekuja baada ya Tanzania kutaka kupandishwa daraja na kuwa nchi ya kipato cha kati, je bado tutaendelea kugoma kusaini?

SOMA ZAIDI: Trade impasse as EU seeks deal with entire EAC bloc
 

Cicero

JF-Expert Member
Jan 20, 2016
2,915
2,000
Ukubwa unakuja na changamoto,hii mambo ya kuitwa Lower middle Income bado ni matusi ingawa ni hatua nzuri.Vipi kuhusu Ghana mbona siioni hapa
Hiyo ni list ya nchi zilizobadilishwa status zao tu. Nadhani Ghana ilikuwa ni middle income toka mda ndio maana haipo hapo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom