STRUGGLE MAN
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 8,638
- 16,566
Benki ya Dunia: Ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupungua sana
Benki ya Dunia imekadiria kuwa kutokana na mlipuko wa COVID-19, ukuaji wa uchumi wa Tanzania mwaka huu utapungua sana na kufikia asilimia 2.5 kutoka asilimia 6.9 kama ilivyokadiriwa na serikali mwaka 2019.
Benki ya Dunia imesema uchumi wa Tanzania utaathiriwa na janga la COVID-19 na msukosuko wa uchumi wa dunia.
Ripoti hiyo iliyotolewa na Benki ya Dunia imesema kuwa serikali ya Tanzania imechukua hatua, na inatarajiwa kuendelea kuchukua hatua za ziada za kiafya na kiuchumi, ili kupunguza athari hasi.
Lakini ripoti hiyo, ambayo ni ya 14 ya Benki ya Dunia kuhusu uchumi wa Tanzania, pia imeonya kuwa, kama hatua za ziada zitacheleweshwa au hazitafanya kazi, na kama mazingira ya nje hayataboreka mwaka huu, ukuaji wa uchumi wa Tanzania huenda utapungua zaidi.
Tathmini ya ripoti hiyo ya Benki ya Dunia inaonyesha kuwa janga la COVID-19 limevuruga maisha ya wananchi wa kawaida ambapo imetabiriwa kuwa Watazania nusu milioni wataingia katika kundi la watu wanaoishi chini ya mstari wa umasikini. Watakaoathirika zaidi ni watoto wanaoishi mijini ambao wamejiajiri na wenye biashara ndogo ndogo.
Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app