World Bank Report: Transforming Agriculture | Realizing the Potential of Agriculture for Inclusive Growth and Poverty Reduction

Benki ya Dunia inazindua sasisho la 13 la Uchumi wa Tanzania lenye jina la 'Mabadiliko katika Kilimo: Kutambua Uwezo wa Kilimo kwa Ukuaji wa Pamoja na Kupunguza Umasikini,' linalotoa udharura katika kuunga mkono sera za umma na kusaidia Umati wa Watu katika uwekezaji wa sekta binafsi na kuchukua fursa ya mabadiliko ya sekta ya Kilimo yanayoendele

Hafla hiyo inaendeshwa na Bi. Bella Bird, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia ya Benki ya Dunia kwa Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe, na kusimamiwa na Mhe. Japhet Hasunga, Waziri wa Kilimo



****

The World Bank launch the 13th Tanzania Economic Update titled, Transforming Agriculture: Realizing the Potential of Agriculture for Inclusive Growth and Poverty Reduction,’ which makes the case for urgent supportive public policies and spending to help crowd in private sector investment and take advantage of the sector’s transformation which is currently underway.

The event will be hosted by Ms Bella Bird, World Bank Country Director for Tanzania, Malawi, Zambia and Zimbabwe, and will be graced by Hon. Japhet Hasunga, Minister of Agriculture.
The Agriculture sector provides livelihoods directly to around 55 percent of the population (and three quarters of the poor) and indirectly to a further 15 percent within related value chain functions such as traders, transporters and processors.

The Tanzanian government recognizes the centrality of Agriculture to realizing its objectives of socioeconomic development, which are well-articulated in the Second Agriculture Sector Development Program (ASDP II).


Ni jambo jema kwa wananchi wa kawaiada,
 
Bila serikali imara tumeona jinsi sekta binafsi ilivyopewa nafasi lakini kwa asilimia kubwa sana walikeza kwa maslahi yao binafsi huku nchi na wananchi wa hali ya chini wakiendelea kubaki kama wateja na watazamaji tuu na kuwa maskini wa kutupwa. Mifano michache inaonyesha uwekezaji haukua kwa maslahi ya nchi sababu uliambatana na hujuma zilizopelekea baadhi ya sekta muhimu kuzorota na unasababisha wananchi wa kawaida kukosa kilicho bora kama kwenye Sekta ya mawasliano, Sekta ya elimu, Sekta ya afya, Taasisi za fedha, Kilimo n.k.

Sekta binafsi inaweza kuwekeza katika uchumi wetu na imekua ikifanya hivyo kwa miaka mingi sasa ila tatizo kubwa lilikuja kwenye
1.Vipaumbele vya wawekezaji vs nchi - tumeona viwanda vyetu vilivyonunuliwa na kufa kabisa
2.Uimamizi kwa upande wa serikali haswa watendaji wakuu
 
Hapa ndipo serikali ya awamu ya tano imefeli kabisa maana haina sera ya kilimo. Awamu ya Tano wameamua kutelekeza kilimo kinachojumuisha wanyonge wengi.

Kwa miaka minne imekazania ma flyover, ndege, mradi wa SGR (reli mpya) ambao hata miaka 15 utakuwa haujaisha kwa kufuatana na ujenzi wake unavyoenda n.k

Kilimo kufuatana na barabara zilizojengwa hadi awamu ya Kikwete na awamu hii ingekarabati reli zote za mkoloni na ya TAZARA tu kisha fedha 'zetu za ndani' zinazojenga SGR RELI, ununuzi wa ndege kwa cash zingeelekezwa ktk sekta ya kilimo yaani kuboresha kilimo kiwe cha kisasa na kuwekeza ktk masoko na viwanda vya kusindika mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi nchi hii ya Tanzania ingekuwa kiuchumi na kuwa donor country.

Sasa wananchi awamu hii kilimo, ufugaji na uvuvi watu wanaambiwa wafanye kazi wakati wapo na juhudi wanJibidisha (resilient ) bila kukata tamaa serikali imewapuuza kwa kutowekeza sera madhubuti ktk kilimo.
Hiyo akili mkuu pale Lumumba unafikri inaweza kutoka kwenye kichwa cha nani? Kifupi ccm hakunaga akili!
 
Bahati mbaya kilimo sio priority kwa serikali ya awamu ya 5. Miaka hii minne kilimo kimezidi kua na hali mbaya sana kwa tz
 
WAZIRI MBARAWA: ''TUSIPOPANGA VIZURI KTK KILA SEKTA, KUTATOKEA MACHAFUKO KAMA NCHINYINGINE'

Prof. Makame Mbarawa - Miradi mingi iliyoanzishwa itakuwa magofu

Tunajenga na kuzindua miradi mingi bila kuwa na mipango madhubuti hivyo miradi hii itageuka magofu 'white elephant'. Ametolea mfano awamu hii hakuna mpango wa kutunza vyanzo vya maji kwa ajili ya kuhakikisha miradi mingi ya WASA water supply nchi nzima DAWASA n.k haina mipango ya kulinda vyanzo vya maji iwe mito n.k



Source: millard ayo
 
Kenya ni nchi ya kibepari na walianza kilimo biashara muda mrefu uliopita , wakati sisi tulipitia kwenye mashamba yakijiji na changamoto zake za uongozi na kukosa motisha, na ukiongezea Bei kuwa controlled na serikali, lakini mabadiliko mbali mbali yameleta tija ktk uzalishaji , ingawa kuna madhara ya uvivu yalio letwa na mambo ya mashamba ya ujamaa, na rushwa kwa jumla, ambayo iliwavutia nguvu kazi wengi kuona kuwa hiyo ndio njia safi ya kuleta maendeleo ktk ngazi mbali mbali, hivyo mabadiliko ya sasa haya wezi kubadilisha hulka za watu wengi/wahusika wengi ndani ya masaa 24
Hapana.
Sikubaliani na mawazo yako, na wala hayaendani na aliyoandika mkuu 'FUSO' na nilivyochangia kwa hoja yake ya kuhudumiwa wakulima.
Wewe umetoka huko kabisa na kuingiza hoja tofauti, ambayo pia huijui. Ningekuwa na muda wa kutosha ningekufundisha juu ya hilo.
Kenya licha ya kuwepo na mashamba makubwa ya michai, mahindi na mengineyo, lakini bado wakulima wadogo wadogo nao bado wapo, na ndio wengi zaidi. Hawa wanapata huduma kutoka kwa wataalam wa kilimo, sio kama hapa kwetu.

Wewe unadhani maziwa mengi yanayozalishwa Kenya na kuuzwa Brookeside, yote yanazalishwa na wafugaji wakubwa?
Una mawazo potofu juu ya 'ujamaa', in fact unaonyesha huelewi lolote.
 
WAZIRI MBARAWA: ''TUSIPOPANGA VIZURI KTK KILA SEKTA, KUTATOKEA MACHAFUKO KAMA NCHINYINGINE'

Prof. Makame Mbarawa - Miradi mingi iliyoanzishwa itakuwa magofu

Tunajenga na kuzindua miradi mingi bila kuwa na mipango madhubuti hivyo miradi hii itageuka magofu 'white elephant'. Ametolea mfano awamu hii hakuna mpango wa kutunza vyanzo vya maji kwa ajili ya kuhakikisha miradi mingi ya WASA water supply nchi nzima DAWASA n.k haina mipango ya kulinda vyanzo vya maji iwe mito n.k



Source: millard ayo

It is about time they start talking; or else, it will be too late!
 






Azam marine, Fastjet n.k watu binafsi wana uwezo hata kuwekeza ktk reli lakini mnadanganywa na awamu ya tano.hukuru

Pia makampuni kama MOTL na Bahkresa Group wanaweza kuchangia rolling stock yaani kununua mabehewa kwa ajili ya usafirishaji mizigo reli ya mkoloni huku kampuni hizo ikilipa tozo kutumia miundo mbinu ya reli ya mkoloni iliyokarabatiwa.

Hii ni kuipunguzia mzigo serikali kununua mabehewa hata vichwa. Serikali kazi yake itakuwa kutunza reli ya mkoloni iliyokarabatiwa kwa gharama nafuu kuliko ujenzi wa SGR reli mpya.

Nchi nyingi dunia zinaendesha sekta ya reli kwa mtindo wa makampuni kushirikiana na serikali.
a
Hapana.
Sikubaliani na mawazo yako, na wala hayaendani na aliyoandika mkuu 'FUSO' na nilivyochangia kwa hoja yake ya kuhudumiwa wakulima.
Wewe umetoka huko kabisa na kuingiza hoja tofauti, ambayo pia huijui. Ningekuwa na muda wa kutosha ningekufundisha juu ya hilo.
Kenya licha ya kuwepo na mashamba makubwa ya michai, mahindi na mengineyo, lakini bado wakulima wadogo wadogo nao bado wapo, na ndio wengi zaidi. Hawa wanapata huduma kutoka kwa wataalam wa kilimo, sio kama hapa kwetu.

Wewe unadhani maziwa mengi yanayozalishwa Kenya na kuuzwa Brookeside, yote yanazalishwa na wafugaji wakubwa?
Una mawazo potofu juu ya 'ujamaa', in fact unaonyesha huelewi lolote.
Ukizungumzia uzalishaji wa Maziwa kwa Tz unatakiwa kujua kwanza historia yetu, baada ya hapo ndio kuja kwa zero grazing na half ilivyo sasa hivi ktk mambo ya zero grazing kwa maeneo ya mjini na changamoto za kupata malisho city by laws.
Lingine ni hili last milk processors kwa mfano Dar??
 
mkuu august, unanionyesha hayo ili iweje. Mbona unataka kuhamisha tuliyokuwa tunajadili na kuyapeleka kwingine?
'FUSO" alizungumzia jinsi asivyopata msaada wowote kutoka kwa wataalamu wa kilimo katika juhudi zake za kilimo.
Wewe unaingiza maswala ya mifumo ya 'ubepari na ujamaa', ambayo hayakuwa mambo yaliyokuwa yakijadiliwa.

Sasa ukitaka kuyajadili hayo, nipo tayari kukukabiri pia. Inaonekana bado umeswekwa kwenye nadharia za mifumo hiyo yote miwili ambayo imekwishaonekana yote inalenga sehemu moja, baada ya waChina kutoa jawabu juu ya mfumo wao.
Wewe bado umeganda tu kule kule kwenye vita baridi?
 
It is about time they start talking; or else, it will be too late!

4 Dec 2019
KITWANGA - "NAMUHESHIMU MAGUFULI, ILA TUTAANDAMANA, ASITULETEE ASKARI"

Mbunge wa Jimbo la Misungwi huko kanda ya Ziwa nchini Tanzania, Mh. Charles Kitwanga ameeleza kuwa kama ahadi za kukamilisha miradi ya maji haitekelezwi hadi Mei mwakani atahamasisha wakazi wa jimbo hilo kuandamana na kufunga mitambo inayotoa maji ziwa Victori kupeleka Shinyanga na Tabora.....

Source: Global TV online
 
1575524812077.png

RIPOTI ya Benki ya Dunia kuhusu Maendeleo ya Kilimo Tanzania, imebainisha kuwa sekta ya kilimo nchini imeanza kuwa na mabadiliko chanya. Imesema mabadiliko hayo yakitumiwa vyema, yataleta fursa zaidi katika kuongeza ajira, kuondoa umasikini na kuongeza uzalishaji.

Aidha, ripoti hiyo iliyofanyiwa utafiti kwa muda wa miaka miwili, pia imeendelea kuitaja Tanzania kuwa ni nchi namba moja kati ya nchi za Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unakua kwa kasi.

Taarifa fupi kuhusu ripoti hiyo iliwasilishwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe, Bella Bird.

Bird alisema pamoja na mabadiliko hayo, iko haja kwa serikali kuchukua hatua za kuboresha sera na mazingira ya uwekezaji katika sekta hiyo ya kilimo.

Alisema ripoti hiyo imeonesha kuwa kutokana na jitihada mbalimbali, zinazofanywa na serikali katika kukuza sekta ya kilimo, mabadiliko chanya yameanza kuonekana, ikiwemo kuwepo kwa ongezeko la wakulima wa kati, huku wakulima wadogo wanaolima kwa ajili ya chakula tu wakipungua.

“Ripoti inaonesha wakulima wa kati wameongezeka na kufikia 368,000 katika kipindi cha mwaka 2018 hadi mwaka 2014 na hivyo kuingiza takribani dola za Marekani milioni 225 hadi 300,” alisema Bird.

Alitaja maeneo ambayo yameanza kuwa na mabadiliko chanya kuwa ni ongezeko la uzalishaji, ongezeko la ardhi ya kilimo, masoko, huduma za kijamii kama vile barabara na huduma za fedha kwa wakulima na ajira za kilimo.

“Hali ya sasa ya kilimo inatoa fursa kubwa ya kuhamasisha uwekezaji wa kibinafsi na wageni na hivyo kuongeza kipato kwa watu masikini,” alisema Bird.

Alisema kwa takwimu za mwaka 2006 hadi 2016, kilimo kinachangia takribani asilimia 3.5 katika Pato la Taifa huku kukiwa na ongezeko la mchango wake kwenye pato hilo kwa asilimia sita kila mwaka.

Hivyo, ni muhimu kwa serikali kuhakikisha sekta hiyo, inatumika vyema kupunguza umaskini. Alieleza kuwa kiuchumi, Tanzania inafanya vizuri, kwani inaongoza kwa nchi za Jangwa la Sahara kwa uchumi wake kukua kwa kasi, huku mfumuko wa bei ukizidi kushuka.

Alitaja maeneo yanayochangia ukuaji wa kasi wa uchumi wa Tanzania kuwa ni sekta ya ujenzi na madini, huku sekta za kilimo na huduma zikielekea kushuka.

Alisema sekta ya nishati, nayo ilipanda kwa asilimia 15, huku akielezea sekta ya ujenzi kuwa ilipanda kutokana na uwekezaji mkubwa wa sekta binafsi na sekta ya uzalishaji iliongezeka kwa asilimia tano.

Kwa upande wake, Meneja wa Kilimo na Chakula kutoka Benki ya Dunia, Holger Kray alisema kwa hali ilivyo ya kilimo Tanzania, endapo kutakuwa na uwekezaji wa kutosha kwa sekta hiyo kwa angalau hata asilimia moja, takribani ajira 220,000 zinaweza kutengenezwa kwa mwaka.

Alishauri uwekezaji zaidi katika sekta ya kilimo, uhusishe sekta binafsi, kwani huko ndiko kutakuwa na mageuzi makubwa ya kilimo. Alieleza kuwa tayari kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ya serikali, uwekezaji binafsi kwenye kilimo unatarajia kuchangia kwenye eneo hilo kiasi cha dola za Marekani bilioni 20, kati ya dola za Marekani bilioni 45, zinazohitajika kwa ajili ya programu hiyo.

Mchumi Mwandamizi Kilimo katika Benki ya Dunia, Emma Modemba alisema ripoti hiyo, imependekeza kuwa ili kuleta mabadiliko chanya zaidi ya kilimo, serikali haina budi kuhakikisha inaboresha mazingira ya biashara.

Aidha, alisema ripoti hiyo imeshauri serikali kutenga fedha zaidi katika eneo hilo la kilimo, kwa kuwa huko ndiko kwenye ajira na kunakomgusa zaidi mtu masikini. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, bajeti ya kilimo imekuwa ikiongezeka kila mwaka, ambapo kuanzia mwaka 2017 hadi 2019 imeongezeka kwa asilimia tatu.

Chanzo: Habari Leo
 
Hizi ni juhudi za kilimo kwanza za Jaakaya Kikwete sasa nchi imeingizwa kwenye ndege kwanza.
Hii awamu itaingia kwenye vitabu vya historia kwa kulitia taifa hasara.
 
mkuu august, unanionyesha hayo ili iweje. Mbona unataka kuhamisha tuliyokuwa tunajadili na kuyapeleka kwingine?
'FUSO" alizungumzia jinsi asivyopata msaada wowote kutoka kwa wataalamu wa kilimo katika juhudi zake za kilimo.
Wewe unaingiza maswala ya mifumo ya 'ubepari na ujamaa', ambayo hayakuwa mambo yaliyokuwa yakijadiliwa.

Sasa ukitaka kuyajadili hayo, nipo tayari kukukabiri pia. Inaonekana bado umeswekwa kwenye nadharia za mifumo hiyo yote miwili ambayo imekwishaonekana yote inalenga sehemu moja, baada ya waChina kutoa jawabu juu ya mfumo wao.
Wewe bado umeganda tu kule kule kwenye vita baridi?
Mimi sipo kwenye vita baridi especially ktk biashara au shughuli zetu za kiuchumi iwe kilimo au biashara na viwanda
Mfano issue ya mkulima au mfugaji wa ngombe wa maziwa, kwanza dam hatuna kiwanda cha maziwa fresh zaidi ya maziwa ya unga ambayo yanawekwa kwenye packet kama maziwa ya maji, cha pili wenye viwanda wanaweza kuwa na mifugo yao na ku complement kutoka kwa wazalishaji wengine na kutoa bidhaa zingine kama samli, jibini n.k.
Na kuhusiana na maafisa ugani, ikumbukwe kwanza wanaweza kuwa wachache, lakini hizi ni biashara binafsi ya mtu si ya serekali, hivyo ili upate huduma yao lazima umlipe, ili aje sehemu yako aone changamoto zako au unataka serikali ikulipie??
Kwenye hilo hilo la ufagaji wa ngombe wa maziwa kuna suala la malisho, je wakati wa masika unahifadhi malisho ya kutumia wakati wa kiangazi ili ku hakikisha uzalishaji unaendelea vizuri, lingine wengi wa wazalishaji ni retired people na umri umekwenda hivyo kushindwa kutekeleza majukumu mengine kama kutafuta malisho ya kutosha hivyo wanabakisha mifugo kama hobby na sio shughuli ya kiuchumi, sasa sijui na hapo serikali iingilie
 
Hizi ni juhudi za kilimo kwanza za Jaakaya Kikwete sasa nchi imeingizwa kwenye ndege kwanza.
Hii awamu itaingia kwenye vitabu vya historia kwa kulitia taifa hasara.
Punguzeni chuki za kitoto....
mna mazivu nyie.....
ina maana mpaka leo hujui viwanda na kilimo ni vitu vinavyokwenda sambamba!!?
 
Back
Top Bottom