Nxt Millionaire
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 406
- 89
Are you working harder or smarter?
Katika Ulimwengu wa kipato na kujitafutia riziki watu wote tumegawanyika katika makundi makuu manne, Waajiriwa au Waliojiajiri, Wamiliki wa Biashara na Wawekezaji, makundi hayo pia yamegawanyika katika pande kuu mbili, Kushoto na Kulia.
Katika Ulimwengu wa kipato na kujitafutia riziki watu wote tumegawanyika katika makundi makuu manne, Waajiriwa au Waliojiajiri, Wamiliki wa Biashara na Wawekezaji, makundi hayo pia yamegawanyika katika pande kuu mbili, Kushoto na Kulia.
Upande wa kushoto kuna makundi ya Waajiriwa na Waliojiajiri, upande wa kulia ni Wamiliki wa biashara na Wawekezaji, mgawanyiko huu unatokana na wapi chanzo kikuu cha mtu mapato yake kinakopakina.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, wasomi na wataalamu wa uchumi duniani, upande wa kushoto (Waajiriwa na waliojiajiri) ndio wenye watu wengi zaidi duniani asilimiam 95%, ndio wenye kipato kidogo zaidi, unalipa kodi nyingi zaidi, ulio masikini, wasio na uhuru na muda, kipato ama kukaa na familia zao, huku asilimia mkubwa wakiwafanyia kazi walio upande wa kulia na kumiliki asilimia 20 ya utajiri wa dunia.
Lakini upande wa Kulia, Wamiliki wa mifumo ya Biashara na Wawekezaji, ndio upande wenye watu wachache zaidi duniani asilimia 5% tu huku wakimiliki asilimia 80% ya utajiri woote wa dunia, huu ndio upande ambao kipato chao hakitegemei ufanyaji kazi wao moja kwa moja, wanalipa kodi chache, wana uhuru wa kipato, muda na pia kwenda popote watakapo na kufanya kazi na watu wawatakao.
Upande huu wa kulia unamiliki mifumo ya biashara na pia unatumia pesa kuingiza pesa kwa walio katika kundi la wawekezaji, hawa hawaitaji kuamka kila siku asubui kwenda kutafuta riziki, mifumo waliotengeneza uwawezesha kuwa na uhakika wa kipato hata kama yuko mbugani au ngambo na familia wakitalii kwa muda wowote ule.