Work smarter not harder

Nxt Millionaire

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
406
89
Are you working harder or smarter?
Katika Ulimwengu wa kipato na kujitafutia riziki watu wote tumegawanyika katika makundi makuu manne, Waajiriwa au Waliojiajiri, Wamiliki wa Biashara na Wawekezaji, makundi hayo pia yamegawanyika katika pande kuu mbili, Kushoto na Kulia.

Upande wa kushoto kuna makundi ya Waajiriwa na Waliojiajiri, upande wa kulia ni Wamiliki wa biashara na Wawekezaji, mgawanyiko huu unatokana na wapi chanzo kikuu cha mtu mapato yake kinakopakina.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, wasomi na wataalamu wa uchumi duniani, upande wa kushoto (Waajiriwa na waliojiajiri) ndio wenye watu wengi zaidi duniani asilimiam 95%, ndio wenye kipato kidogo zaidi, unalipa kodi nyingi zaidi, ulio masikini, wasio na uhuru na muda, kipato ama kukaa na familia zao, huku asilimia mkubwa wakiwafanyia kazi walio upande wa kulia na kumiliki asilimia 20 ya utajiri wa dunia.

Lakini upande wa Kulia, Wamiliki wa mifumo ya Biashara na Wawekezaji, ndio upande wenye watu wachache zaidi duniani asilimia 5% tu huku wakimiliki asilimia 80% ya utajiri woote wa dunia, huu ndio upande ambao kipato chao hakitegemei ufanyaji kazi wao moja kwa moja, wanalipa kodi chache, wana uhuru wa kipato, muda na pia kwenda popote watakapo na kufanya kazi na watu wawatakao.

Upande huu wa kulia unamiliki mifumo ya biashara na pia unatumia pesa kuingiza pesa kwa walio katika kundi la wawekezaji, hawa hawaitaji kuamka kila siku asubui kwenda kutafuta riziki, mifumo waliotengeneza uwawezesha kuwa na uhakika wa kipato hata kama yuko mbugani au ng’ambo na familia wakitalii kwa muda wowote ule.


 
Hiyo ni cash flow quandrant, learn how to move from left side to right need moyo wa mamba! Courageous heart, risks are many!, but still people move slowly from being employee to self employed. Yaan we acha kaka, namkumbuka Rober Kiyosaki katika haya madude. Very impressing! 90pecent Ya wote wanaopata A darasani wako hapo kwenye left side tena ni employees.
 
Hiyo ni cash flow quadrant, learn how to move from left side to right need moyo wa mamba! Courageous heart, risks are many!, but still people move slowly from being employee to self employed. Yaan we acha kaka, namkumbuka brain Rober Kiyosaki katika haya madude. Very impressing! 90pecent Ya wote wanaopata A darasani wako hapo kwenye left side tena ni employees.
 
Hiyo ni cash flow quadrant, learn how to move from left side to right need moyo wa mamba! Courageous heart, risks are many!, but still people move slowly from being employee to self employed. Yaan we acha kaka, namkumbuka brain Rober Kiyosaki katika haya madude. Very impressing! 90pecent Ya wote wanaopata A darasani wako hapo kwenye left side tena ni employees.

Yaah, umenena mkuu, inahitaji juhdi za ziada, but with time it pays, je mwanamichezo mwenye ndoto za kuwa super star wa ulimwengu anafanyaje? wanasema Winners never quits, if you have your Definite Chief Aim in life and apply the Self Confidence formula properly coupled with ACTION you will eventually move from left side to the Light side.
Remember "PRACTICES MAKES PERFECT"
 
Back
Top Bottom