Women Lounge: Shogangu kazaa na mdingi, hebu nambieni nimfanyeje huyu?

Acha tu mmama wa watu apate presha.
Sie wanawake wabaya sana.
Yani kama namuona vile mdingi anavyochezea vichuchu na vita.ko vya shoga angu,
akirudi home mkali kama pilipili.
Hahahahahahaha! Tumelaaniwa ati, Zinduna tulipie nauli ya boti mimi na Madame B tuje kumsalimia mzazi.
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahahaha! Tumelaaniwa ati, Zinduna tulipie nauli ya boti mimi na Madame B tuje kumsalimia mzazi.

Tena atulipie FirstClass asijishaue.
Twataka kumuona na kumsalimia baba na 'mama'.
Ila usisahau kubeba na lile Pensi lako na First Aid Kit kbs maana huko ni kurudi aidha Mzima ama Mfu.
sweetlady twen'zetu.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana shosti Zinduna inauma i can imagine. Nahisi unahisi usingekuwa na ushoga na huyo koroboi wala yasingetokea haya. Usijali. Yatakwisha. Yatakwishaje? Mtulie mtumie akili....namuunga mkono Lisa, muendee polepole tena mpelekee mijizawadi shosti (ofkozi cheap cheap things...lol mpkaka ashangae ile like haamini you can buy those cheap things for her while you are her bestito....dhe knows you better) then kusanya picha etc za huyo mtu wa maskati, za wanaume wake wote....the rest endelea wewe. Haribu kwa mizombie yake yote - kama unawajua. baada ya fumanizi/ndio akishalose kila kitu ndo mumuendee na matarumbeta (na kiduku ikibidi) na sare mumkatie...!

Yani i cant imagine alikuwa anafikiria nini kutembea na mshua wakati ni rafiki yako!!!
i mean..........huo ni urafiki kweli?!?!?!?.......kama sio kutengeneza uadui?!?!?

Kwlei kikulacho kinguoni mwako!
 
Last edited by a moderator:
Yani acha shost sweetlady.
Wanawake sisi wabaya sie acha tu.
Ukute hapo huyo baba akiwa nae siri zenu zoote za home anamwagia huyo Shetwani wa kike mchambia wima.
Aliekosa uso akapewa komwe.
Yani mie ningekuwa Zinduna,ningekuwa nishagawana majengo ya Serikali na huyo Kibibi-duka aliekosa bwana akaja zaa na Mshua anaetufanya tusiioteshe majani njia ya chooni.
Alaaa...
Nahs huyo Baba kama sio Bishanga basi ni Baba V au Dark City kama sio Asprin.

Sasa wewe madame unatafuta laana,

Ndiyo inauma ila hata ukikengeuka kiasi gani, huna ruhusa ya kuwatukana wakubwa zako...

Nenda katubu kwanza...kaone na umri wake usiofika 18 kama Lulu...

Pole sana Zinduna...

Nitarudi next time kulisema hili.....
 
Last edited by a moderator:
Sasa wewe madame unatafuta laana,

Ndiyo inauma ila hata ukikengeuka kiasi gani, huna ruhusa ya kuwatukana wakubwa zako...

Nenda katubu kwanza...kaone na umri wake usiofika 18 kama Lulu...

Pole sana Zinduna...

Nitarudi next time kulisema hili.....

Nimerusha jiwe gizani.
Atakaesema yalaa...!!
Jua limempata.
Nawe limekupata.
Utajiju.
Mimi mkubwa na ninaweza kukumilika na usiende kwa bibi wala kwa mjukuu wako Kongosho.
 
Last edited by a moderator:
Nimerusha jiwe gizani.
Atakaesema yalaa...!!
Jua limempata.
Nawe limekupata.
Utajiju.
Mimi mkubwa na ninaweza kukumilika na usiende kwa bibi wala kwa mjukuu wako Kongosho.

Hawa mama wa kujiongeza kwa umri. Madame B, ....Mie nasema hivi,....kwaherini....

Ila hakikisha hammpi mwenzenu Zinduna sumu!

Najua mkishatulia mtatuita tuwape hitimisho au conclusion kabla hamjaharibu....


Kumbuka kuwa moto hauzimwi kwa papara.......!!


I hope you all know what Babu is saying!!


Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Hawa mama wa kujiongeza kwa umri. Madame B, ....Mie nasema hivi,....kwaherini....

Ila hakikisha hammpi mwenzenu Zinduna sumu!

Najua mkishatulia mtatuita tuwape hitimisho au conclusion kabla hamjaharibu....


Kumbuka kuwa moto hauzimwi kwa papara.......!!


I hope you all know what Babu is saying!!


Babu DC!!

Nisalimie,
tumpe sumu kabla ya kibano?
Thubutu.
Haya salamu zao huko Nyumba mpya.
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha haaaaa, kwa usongo sasa na ww kazae na Dingi yakeee, kama dingi yake hajulikani, mshawishi bro wako akazae na mamayake ngoma droooo
.Yalahh msinipige mawe napita tuuu, yalaaa...........................................................! wananiua hukuuuuuuuuuuuu!
Chap.
 
Yani acha shost sweetlady.
Wanawake sisi wabaya sie acha tu.
Ukute hapo huyo baba akiwa nae siri zenu zoote za home anamwagia huyo Shetwani wa kike mchambia wima.
Aliekosa uso akapewa komwe.
Yani mie ningekuwa Zinduna,ningekuwa nishagawana majengo ya Serikali na huyo Kibibi-duka aliekosa bwana akaja zaa na Mshua anaetufanya tusiioteshe majani njia ya chooni.
Alaaa...
Nahs huyo Baba kama sio Bishanga basi ni Baba V au Dark City kama sio Asprin.
Una hamu na mimi? Nakuuliza unan'taka?
 
madingi nao jamani,
kwanini asitafute mwingine huko kitaani,
but, mchukueni mdogo wengu mlee ili bi dada atafute jiko lake.
 
Tena atulipie FirstClass asijishaue.
Twataka kumuona na kumsalimia baba na 'mama'.
Ila usisahau kubeba na lile Pensi lako na First Aid Kit kbs maana huko ni kurudi aidha Mzima ama Mfu.
sweetlady twen'zetu.
sasaukifa utapewa first aid ya namna gani?
 
Kichwa cha habari hapo juu kinahusika sana. Hiki ni kibaraza cha wanawake wenzangu, wanaume haiwahusu kabisa maana hapa tunataka kumsengenya mtu, anayejijua kwamba ana ?€˜K?€™ ndiye ahusike hapa. Mnaweza kushangaa kwa nini nimeweka hapa huu mkasa wakati ni kisa cha kweli, hapa ninataka tumsengenye mtu kisawasawa kwa raha zetu, naogopa nikiweka kule MMU hatutafaidi maana mijanadume itaingilia.

Haya shoga zangu iko hivi wenzangu:

Ninaye shogangu wa wa damudamu, yaani twaambiana siri, hatufichani, yale mambo ya kujirusha na mabwana ndo usisema, lake langu langu lake, nakwambieni twaazimana Madera na twapakana piko, siku zingine aja kulala kwetu na mie nenda lala kwao. Nakwambieni shoga wa ukweli.Kumbe mwenzangu anakula na mdingi mie hata sijui. Sasa siku moja mama katoa wazo eti kaka yetu mkubwa amchumbie shoga maana ana nidhamu na anafaa kuwa mke mwema. Mh, mdingi kusikia hivyo kaja juu, akasema haiwezekani kaka kumwoa shogangu kwa kuwa hana staha, hajatulia na hana malezi ya pande mbili, mama yake keshaolewa na kuachika mara saba na kaishi kama nyumba ndogo miaka saba(Shoga ni zao la nyumba ndogo). Mama akajinyamazia, kumbe mdingi ashaonja na keshanogewa na hapo alikuwa anataka kuchonga mzinga.

Mara namwona shoga kitumbo hicho, namuuliza mwenzangu vipi, nani mhusika? Maana shoga alikuwa anakula na mambwana wawili, akanambia muhusika yuko Maskat na mwakani atafunga ndoa na kuhamia Makati na mumewe.
Mwenzangu mbona huyo bwana hujawahi nitambulisha, maana sie mashoga hatufichani, akanambia walijuana wakati niliposafiri kwenda Tanga,(kuna kipindi nilikwenda Tanga kwa mjomba) na alipata hiyo mimba kwa ule mtindo wa one night stand. Mie mh, nikamuuliza je, jamaa kajua na amekubali, shoga akanambia kakubali na atamuoa. Mie tena, shoga hata picha huna nimjue shemeji, shoga akadai picha hana ila atatumiwa kwenye internet. Basi ndo siku kajiendea huko kwenye internet kajiokotea mipicha ya kijana wa kiarabu handsome boy na kuja kunionyesha, mie acha nimsifu, kumbe shoga ana lake moyoni.

Sasa mwezi wa 11 mwishoni kajifungua, na hivi majuzi mdingi kafunguka kwa mother kuwa amezaa na shogangu na anataka kumuoa mke wa pili. Mama Presha imepanda, nyumbani hapaliki wala hakulaliki.. Mie na dada zangu wawili mbio kwa shoga, kwenda kulianzisha, kufika tukaambiwa eti ana presha na amelala haitakiwi asumbuliwe, tukarudi kutafakari na mama. Lakini mother anadai kwamba dalili alikwishaziona toka mwanzo kuwa mdingi ana kidudu mtu kinamzingua, lakini akapuuza akijua ni hisia potofu tu, kumbe kidudu mtu anamlia mali zake.Huyo mtoto mwenyewe nikimwangalia DNA inahusika sana ,maana kuna dalili zote kwamba mdingi kabambikwa. Kwani shogangu mwenyewe yuko mwingi na mpana kama unga wa ngano.

Hivi hapa nyumbani hali ni tete watoto wote tumemuwekea mdingi mgomo hakuna hata anayeongea naye na sasa tunajipanga mie na dada zangu kwenda kumchamba shoga mpaka atie akili.Mtoto mbaya ka nini yule, yaani binti wa miaka 25, kuzaa na mdingi wa over 50 na kuhatarisha ndoa ya mama yangu iliyodumu kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Basi shoga zangu, hili ndilo nililowaitieni na baada ya kupewa cha Arusha na Karucee na Da King'asti ndio nimeona nifunguke hapa ili mnipe ushauri nimfanyeje huyu shogangu jamani.Karibuni kibarazani: cacico, snowhite, Karucee, Ciello, MwanajamiiOne, Madame B, MadameX, AshaDii, Mamndenyi, Kabakabana, Kipipi, Smile, lara 1, charminglady, sweetlady, FirstLady 1, Angel Msoffe, flora msoffe, Lisa, nivea, farkhina na mashoga zangu wengine wenye mapenzi mema na mie
Du kweli nyie mapashkuna!
Mnalileta pashkuna lililojilegeza nyumbani halafu mnafikiri mzee anameza mate kavu kavu?
Hata mie nala vitu nilivoletewa ati!
 
Back
Top Bottom