Women Lounge: Shogangu kazaa na mdingi, hebu nambieni nimfanyeje huyu?


Zinduna

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Messages
2,381
Points
1,500
Zinduna

Zinduna

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2011
2,381 1,500
Kichwa cha habari hapo juu kinahusika sana. Hiki ni kibaraza cha wanawake wenzangu, wanaume haiwahusu kabisa maana hapa tunataka kumsengenya mtu, anayejijua kwamba ana ‘K’ ndiye ahusike hapa. Mnaweza kushangaa kwa nini nimeweka hapa huu mkasa wakati ni kisa cha kweli, hapa ninataka tumsengenye mtu kisawasawa kwa raha zetu, naogopa nikiweka kule MMU hatutafaidi maana mijanadume itaingilia.

Haya shoga zangu iko hivi wenzangu:

Ninaye shogangu wa wa damudamu, yaani twaambiana siri, hatufichani, yale mambo ya kujirusha na mabwana ndo usisema, lake langu langu lake, nakwambieni twaazimana Madera na twapakana piko, siku zingine aja kulala kwetu na mie nenda lala kwao. Nakwambieni shoga wa ukweli.Kumbe mwenzangu anakula na mdingi mie hata sijui. Sasa siku moja mama katoa wazo eti kaka yetu mkubwa amchumbie shoga maana ana nidhamu na anafaa kuwa mke mwema. Mh, mdingi kusikia hivyo kaja juu, akasema haiwezekani kaka kumwoa shogangu kwa kuwa hana staha, hajatulia na hana malezi ya pande mbili, mama yake keshaolewa na kuachika mara saba na kaishi kama nyumba ndogo miaka saba(Shoga ni zao la nyumba ndogo). Mama akajinyamazia, kumbe mdingi ashaonja na keshanogewa na hapo alikuwa anataka kuchonga mzinga.

Mara namwona shoga kitumbo hicho, namuuliza mwenzangu vipi, nani mhusika? Maana shoga alikuwa anakula na mambwana wawili, akanambia muhusika yuko Maskat na mwakani atafunga ndoa na kuhamia Makati na mumewe.
Mwenzangu mbona huyo bwana hujawahi nitambulisha, maana sie mashoga hatufichani, akanambia walijuana wakati niliposafiri kwenda Tanga,(kuna kipindi nilikwenda Tanga kwa mjomba) na alipata hiyo mimba kwa ule mtindo wa one night stand. Mie mh, nikamuuliza je, jamaa kajua na amekubali, shoga akanambia kakubali na atamuoa. Mie tena, shoga hata picha huna nimjue shemeji, shoga akadai picha hana ila atatumiwa kwenye internet. Basi ndo siku kajiendea huko kwenye internet kajiokotea mipicha ya kijana wa kiarabu handsome boy na kuja kunionyesha, mie acha nimsifu, kumbe shoga ana lake moyoni.

Sasa mwezi wa 11 mwishoni kajifungua, na hivi majuzi mdingi kafunguka kwa mother kuwa amezaa na shogangu na anataka kumuoa mke wa pili. Mama Presha imepanda, nyumbani hapaliki wala hakulaliki.. Mie na dada zangu wawili mbio kwa shoga, kwenda kulianzisha, kufika tukaambiwa eti ana presha na amelala haitakiwi asumbuliwe, tukarudi kutafakari na mama. Lakini mother anadai kwamba dalili alikwishaziona toka mwanzo kuwa mdingi ana kidudu mtu kinamzingua, lakini akapuuza akijua ni hisia potofu tu, kumbe kidudu mtu anamlia mali zake.Huyo mtoto mwenyewe nikimwangalia DNA inahusika sana ,maana kuna dalili zote kwamba mdingi kabambikwa. Kwani shogangu mwenyewe yuko mwingi na mpana kama unga wa ngano.

Hivi hapa nyumbani hali ni tete watoto wote tumemuwekea mdingi mgomo hakuna hata anayeongea naye na sasa tunajipanga mie na dada zangu kwenda kumchamba shoga mpaka atie akili.Mtoto mbaya ka nini yule, yaani binti wa miaka 25, kuzaa na mdingi wa over 50 na kuhatarisha ndoa ya mama yangu iliyodumu kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Basi shoga zangu, hili ndilo nililowaitieni na baada ya kupewa cha Arusha na Karucee na Da King'asti ndio nimeona nifunguke hapa ili mnipe ushauri nimfanyeje huyu shogangu jamani.Karibuni kibarazani: cacico, snowhite, Karucee, Ciello, MwanajamiiOne, Madame B, MadameX, AshaDii, Mamndenyi, Kabakabana, Kipipi, Smile, lara 1, charminglady, sweetlady, FirstLady 1, Angel Msoffe, flora msoffe, Lisa, nivea, farkhina na mashoga zangu wengine wenye mapenzi mema na mie
 
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Messages
7,464
Points
1,250
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined May 21, 2012
7,464 1,250
lol ya kweli yamewafika lol nafsi yangu mie lol kweli kikulacho kii nguoni mwako aisee ,mwambie mama ajikalie pembeni ngoma ndio ishapasuka tena akae aicheki dogodogo akiicheza ,kwa sasa,mwacheni mama asife presha bure na uyo paka pori mpeni mama moy ajitenge kabisa na huyo bwana huyo mballi na chumba amwachie la sivyo kama huyo dogodogo ndio mwingi ukimwi uko hapo mlangoni bado kuingia tu nakuambia Zinduna hakiamungu ndio sababu sitakagi shoga mie kabisaa wala sitaki wafike kwangu wataniibia mume wangu mie bora aibiwee mballi nisipopajua hapo karibu bora nimfuate lulu huko segerea khaa
 
Last edited by a moderator:
figganigga

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Messages
16,406
Points
2,000
figganigga

figganigga

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2010
16,406 2,000
mke wa baba yako ndo mama yako so kuwa makini kabla haijala kwako. samahani lakini nimecomment bila kusoma stipulate za post. mia
 
Zinduna

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Messages
2,381
Points
1,500
Zinduna

Zinduna

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2011
2,381 1,500
lol ya kweli yamewafika lol nafsi yangu mie lol kweli kikulacho kii nguoni mwako aisee ,mwambie mama ajikalie pembeni ngoma ndio ishapasuka tena akae aicheki dogodogo akiicheza ,kwa sasa,mwacheni mama asife presha bure na uyo paka pori mpeni mama moy ajitenge kabisa na huyo bwana huyo mballi na chumba amwachie la sivyo kama huyo dogodogo ndio mwingi ukimwi uko hapo mlangoni bado kuingia tu nakuambia Zinduna hakiamungu ndio sababu sitakagi shoga mie kabisaa wala sitaki wafike kwangu wataniibia mume wangu mie bora aibiwee mballi nisipopajua hapo karibu bora nimfuate lulu huko segerea khaa
nivea, hapa tuna mkakati wa kumfanyia mie na dada zangu, atuulie mama yetu kwa kisa gani khaaaaa!
 
Last edited by a moderator:
babalao 2

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
4,698
Points
2,000
babalao 2

babalao 2

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2012
4,698 2,000
Hapo kazi mnayo ila huyo n mama hakuna ubishi. Huo ni ushauri na hauna jinsia ila wachangiaji ndyo tuna ke na me
 
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
31,004
Points
2,000
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2011
31,004 2,000
anzisheni timbwili mpaka shoga ahame mji....

Then lianzisheni home au mnamwogopa mdingi? Mnamwanzishia timbwili na kuhakikisha hatoi mguu kwenda popote


sijui ninunue hiyo kesi....
 
Zinduna

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Messages
2,381
Points
1,500
Zinduna

Zinduna

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2011
2,381 1,500
kumfanyizia nani ?baba yenu? Au huyo shost? Baba rahisi tu mbona tafuteni mtu amwagie UPUPUUUU
Tunapanga kumfanyia shogangu na hata mtoto tunataka apimwe DNA lakini mdingi kasema eti kitand hakizai kharamu, balaa gani hili yarabi ala mina
 
Zinduna

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Messages
2,381
Points
1,500
Zinduna

Zinduna

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2011
2,381 1,500
anzisheni timbwili mpaka shoga ahame mji....

Then lianzisheni home au mnamwogopa mdingi? Mnamwanzishia timbwili na kuhakikisha hatoi mguu kwenda popote


sijui ninunue hiyo kesi....
Mdingi katutishia kutuachia laana eti sie wanae hatuna mamlaka ya kumpangia wakni dini inamruhusu,
Mie sina neno na dini lakini kwa shogangu! Hivi naanzaje kumwita mama huyu kidudu mtu?
 

Forum statistics

Threads 1,285,190
Members 494,498
Posts 30,853,217
Top