ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,699
- 9,455
hii ni kwa wanawake na wadada wa jf
nina jambo nataka kuwashirikisha hasa wanawake wa jf kama watapenda kuwa tayari katika kujisajiri katika group la women issues basi wasisite kujitokeza na kujisajiri
nimpenda kuwashirikisha mambo kadhaa ya kufanya kama wanawake kabla hatujamaliza mwaka huu,
kwani wanawake ndo msingi na nguzo ya familia na vilevile wanawake tunaweza tukipewa naafasi katika ngazi mbalimbali.
issue ya 1. Kuanzisha kitu au biashara kuwa wajasiliamali wa jf
ambayo tutaweza kutuinua na kutufanya tusiwe tegemezi kwa wanaume kuwa na mapendekezo au mchango wa maoni , ushauri, ni kitu gani tuanzishe ili tuwe. Kwa hiyo mwanamke wa jf changamkia tenda hii toa maoni , ushauri wako
issue 2: Kuwa na chombo cha wanawake wa jf
ambacho kitatetea maslahi ya wanawake hususani katika ukandamizaji juu ya mfumo dume uliopo na kuwainua wanawake ambao hawajiwezi km vile; walemavu, wenye matatizo ya uzazi, magonjwa ya kufisha na wanawake walioko vijijiini n.k, kuwatembelea na kujua matatizo yao na kuweza kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine.
isuue 3: Utamaduni na desturi za mwanamke wa kitanzania ziweje
hii itahusika na maadili ya mwanamke wa kitanzania aweje na mambo mengine ya kitamaduni
mavazi, maisha kwa ujumla
issue 4: Mambo ya burudani
yaani tuwe na studio yetu wenyewe ambayo tutaimiliki na tuwe na na vitu ambavyo tutafanya vya burudani ili kutunisha mfuko wetu wa women issue.
issue 5: Mambo ya kitabibu na kisaikolojia zaidi,
tuwe na watu waliosomea mambo ya cancelling, ushauri na mambo ya kitabibu tuwapo katika
vikao vyetu ama makongamano yetu ambayo tutawaita wataalamu na kutufundisha zaidi
maisha ya uzzazi wa mpango na mambo ya ndoa na maisha kwa ujumla.
issue 6: Tuwe na mambo ya ujasiliamali
mwanamke ni nguzo ya familia hivyo hana budi kuwa mchapakazi ili kuinua uchumi wa familia
yake.
kama kuna mambo mengine ambayo sijayaoroddhesha hapa basi wewe mwanamke wa jf naomba ushirikiano wako na mchango wako wa ushauri namna gani tufanye ili tuweze kuwa kitu kimoja ndani ya jf hii na ili tuweze kutambuana na kuinuana kama wanawake wa jf, ili ni jambo jema tena la busara kuwa pamoja kwa umoja na kufanya jambo au kitu kwa pamoja ni jukwaa la wanawake wa jf. Basi usisite kutwanga hapa mtazamo wako tufanye nini ili tuinuane wanawake wa jf.
Sikakatai ushauri, maoni, mapendekezo, au jambo lolote liwe jema au baya we twanga tu tutasaidiana na kama mnataka lilni tuanzishe kitu hiki basi msisite kusema hapa.
Natumia tuko pamoja
slogan: 'tutajenga women issue kwa umoja na upendo'