Wolper, Ford, Lulu watarajia makubwa Cosota, Basata kuungana

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878
wolper+pic.jpg

Elizabet Michael (Lulu) akiwa kulia

Dar es Salaam. Wacheza filamu, Jackline Wolper, Elizabet Michael (Lulu) na Shamsa Ford wamesema mpango wa kuunganisha vyombo vya kusimamia sanaa nchini vya Cosota, Basata na Bodi ya Filamu vitachangia kurudisha tasnia hiyo kwenye kiwango bora.

Wasanii hao ni miongoni mwa waliojitokeza kwenye mkutano wa Waziri wa habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na mwenzake wa Viwanda na biashara, Innocent Bashungwa.

Mkutano huo wenye ajenda mbili ikiwamo ya kuona ni namna gani Taasisi hizo tatu zinavyoweza kufanya kazi kwa pamoja sanjari na wasanii kupata gawio (mrabaa) kutokana na kazi yao.

Wakizungumza katika mkutano huo wasanii hao walisema jambo hilo walitamani lifanyike muda mrefu na limekuja wakati muafaka.

"Tukiwa kitu kimoja hata sheria kali zitapunguzwa, lakini pia umoja ni nguvu, hatuwezi kusimamisha Tasnia kama hatuna umoja," alisema Wolper.

Alisema kitendo cha kuwa na matabaka wakati wote wanafanya kazi ya sanaa kinapunguza msisimko hivyo wakiwa kitu kimoja sanaa itapiga hatua.

Chanzo: Mwananchi
 
kwenye huo mkutano hawakuwepo wakina tin white na ringo,maana hao ndo wanaotoa filamu kila kukicha,hao wakina lulu wanaigizia wapi?
 
Back
Top Bottom