Wolper anyang’anywa gari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wolper anyang’anywa gari

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Chenge, Jun 20, 2012.

 1. Chenge

  Chenge JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 1,077
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  [​IMG]Mwigizaji ‘five star’ kutoka tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, amenyang’anywa ‘mkoko’ (gari) wa kifahari aliokuwa akitanua nao katika mitaa ya mbalimbali ya jiji la Bongo.


  Habari zenye ukweli 100% ambazo blog hi imezinyaka zinasomeka kuwa Wolper anayejulikana kama Amber Rose wa Bongo amenyang’anywa mkoko huo aina ya BMW X6 wenye thamani ya ‘ngawira’ za kibongo ML 170, sambamba na kupigwa ‘stop’ kukaribiana na mshefa aliyekuwa amemnunulia ndinga hiyo.


  Kwa mujibu wa chanzo chetu, hatua ya mshefa huyo kuamua kuchukua ndinga yake ni baada ya kugundua kuwa Wolper anatoka kimapenzi na ‘sharobaro’ mmoja anayemiliki duka maarufu la viwalo pande za Kinondoni.


  Aidha chanzo hicho, kimeieleza blog hii kuwa hivi sasa mwanadada huyo ameamua kutembelea ndinga aina ya Noah aliyokuwa anaitumia hapo awali sambamba na kutoka kwa kuvizia kukwepa watu wake wa karibu washitukie mchongo.

  Katika kuhakikisha kuwa ukweli unajulikana blog hii iliamua kumsaka na baada ya kupatikana Wolper aligeuka mbongo na kudai kuwa hakuna jambo kama hilo isipokuwa kilichotokea ni kuwa gari limepata matatizo na ameamua kulipeleka ‘garage’.  Alipotakiwa kueleza kuwa imekuwaje gari mpya kama ile aipeleke garage tene kwa siku tatu Wolper alisme hivi:


  “Bwana eeh wee jua liko ‘garage’ hayo maswali mengine mimi sitaki kuayasikia na kama una taka ugomvi endelea kuniuliza” alisema na kuondoka haraka eneo alilokuwa amekaa
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  pole yake
   
 3. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Wasanii wa kibongo wana kazi sana.Alikuwa anamuhadaa nani sasa!!!! Ona sasa ameumbuka
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Hii siyo Habari mpya hapa JF.
   
 5. T

  TUMY JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  so what?
   
 6. andate

  andate JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 2,655
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Huyo mshefa nae ni mwehu tu. alidhani anaweza kufuga kunguru?
   
 7. stineriga

  stineriga JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 2,033
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  pole yake, fujo zile $10K anazikumbuka ,
   
Loading...