Woga Wa Yanga Na Simba Ni Moja Ya Sababu Za Udhaifu Wa Taifa Stars

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Si mara Ya kwanza kusikia Simba na Yanga zikijitoa kwenye michuano mikubwa hasa Ya hapa East Africa,wote wamekua mara nyingi wakitoa sababu ambazo hazina mashiko, lakini inafikia mtu unajiuliza ni lini wachezaji wetu hawa ambao wengi wao ni wachezaji wanaoaminiwa na taifa,Ni lini watajenga moyo wa upambanaji? Kwanini wanaogopa sana mipambano Ya kimataifa? Ni lini watajijengea ujasiri? (Fighting Spirit)
T. P. Mazembe ni klabu kubwa Sana ukilinganisha na Yanga na Simba mbona wao hawana dharau na woga huu na wamekubali kuja shiriki Kagame Cup hivi Wao Simba na Yanga ni Nani?
Timu hizi mbili zinajenga na ni kiini cha Udhaifu mkubwa wa maendeleo Ya soka nchini
Kesho jumapili Everton inacheza na Kariobang Sharks pale Nairobi Kenya isingekua Udhaifu wa hawa ndg zetu tungeshuhudia mtanange huu hapa nyumbani pengine! na huu ni mwaka wa pili mfululizo timu za kenya zina fanikiwa kucheza na everton
Na ndio Kisa tulifungwa na harambee stars sikushangaa ni kutokana na madhaifu haya! Na ndiyo kisa hatutaweza pia kuwashinda Drc wenzetu wanaona mbali si klabu hizi zinazoona kuanzia Jangwani na mwisho mtaa wa msimbazi kariakoo!
Serikali zifuteni klabu hizi ni mzigo tu tokea miaka ya 1930's hata viwanja hazina!
 
Kwamba kwa thread kama hii mpaka sasa akuna member ata moja aliyechangia? Au wote wameenda chato? Come on njoo mtwambie kwann tunaogopa kwenda kagame challange wakati ili ndio dirisha la maandalizi kwa msimu ujao?
 
Katibu wa cecafa anadharau sana
Wambadilishe. Maana huwa anajibu ujinga sana utazani kuwa yeye ndo anasajili au kulipa mshahara.
 
Yawezekana ana mapungufu yake lakini simba na yanga zinatuangusha... Huyo katibu amezidharau timu hiz mbili tu?
 
Mkuu Ibanezafrica,
Ni kweli maana hizo timu kongwe za Tanzania kama hata wangepeleka vikosi vyao vya pili pia ingewapatia uzoefu wachezaji ambao hawako Taifa Stars lakini wanasota benchi ktk timu zao.

Maana yake timu kongwe wangepata kikosi 'kipana' zaidi ukichanganya na wale first eleven ambao pia wanachezea timu ya Taifa ktk mashindano ngazi ya vilabu na national team ktk mashindano ya kimataifa.
 
Wanadhani aliyeanzisha hii thread ni Musonye!
Kwamba kwa thread kama hii mpaka sasa akuna member ata moja aliyechangia? Au wote wameenda chato? Come on njoo mtwambie kwann tunaogopa kwenda kagame challange wakati ili ndio dirisha la maandalizi kwa msimu ujao?
 
Japo ni shabiki wa mnyama, lakini nilishasema ili soka la TZ likuwe hatuna budi kuhakikisha hizi yeam mbili zina kufa au zina baki huko daraja la nne na ndondo, matatizo matupu kuanzia kwa hao wanaojiita wadhamini hewa na walioshikiria hati, hawana maono wala mwelekeo wa timu kesho, wanacho zani team inashinda via karumanzira na si mipango thibiti.
 
simba na yanga zina athari kubwa sana kwenye maendeleo ya soka la Tanzania.
Wakati mwingine mi nadhani haya ni magenge ya siasa zaidi kuliko vilabu vya mpira.
Kweli kabisa nashangaa mazembe inafadhiliwa sijui kumilikiwa na Katumbi lakini inafanya vizuri Simba na Yanga wafadhili wakijitokeza figisu kibao kama wasenge ivi

'Na hii tabia imeenea kila sekta '
 
Si mara Ya kwanza kusikia Simba na Yanga zikijitoa kwenye michuano mikubwa hasa Ya hapa East Africa,wote wamekua mara nyingi wakitoa sababu ambazo hazina mashiko, lakini inafikia mtu unajiuliza ni lini wachezaji wetu hawa ambao wengi wao ni wachezaji wanaoaminiwa na taifa,Ni lini watajenga moyo wa upambanaji? Kwanini wanaogopa sana mipambano Ya kimataifa? Ni lini watajijengea ujasiri? (Fighting Spirit)
T. P. Mazembe ni klabu kubwa Sana ukilinganisha na Yanga na Simba mbona wao hawana dharau na woga huu na wamekubali kuja shiriki Kagame Cup hivi Wao Simba na Yanga ni Nani?
Timu hizi mbili zinajenga na ni kiini cha Udhaifu mkubwa wa maendeleo Ya soka nchini
Kesho jumapili Everton inacheza na Kariobang Sharks pale Nairobi Kenya isingekua Udhaifu wa hawa ndg zetu tungeshuhudia mtanange huu hapa nyumbani pengine! na huu ni mwaka wa pili mfululizo timu za kenya zina fanikiwa kucheza na everton
Na ndio Kisa tulifungwa na harambee stars sikushangaa ni kutokana na madhaifu haya! Na ndiyo kisa hatutaweza pia kuwashinda Drc wenzetu wanaona mbali si klabu hizi zinazoona kuanzia Jangwani na mwisho mtaa wa msimbazi kariakoo!
Serikali zifuteni klabu hizi ni mzigo tu tokea miaka ya 1930's hata viwanja hazina!
Kama ulikuwa akilini mwangu,timu 4 za tz zinawakilisha nchi mashindano ya caf,zote makocha kutoka kwa majirani,mpaka wasaidizi wao,alafu et tufanye vizuri,maweee
 
Simba, Yanga na ccm hivi vitatu ni chanzo cha hasara ya taifa, hasara michezoni na hasara kwa maendeleo ya uchumi wa taifa
 
Ungeenza na wale wapuuzi wanaopanga ratiba hata haieleweki,wanaunga unga tu,Kagame cup nikama bonanza tu halina faida yoyote kwa timu za east Africa, timing yake mbovu,mfano Afcon inaendelea na mashindano yanaanza nani atakuwa busy na kagame???

Kabla ya kuleta Uzi ungempigia msonyi na genge lake waache upuuzi kwanza na wafanye mambo kwa weledi na si kijinga jinga hivi
 
Kwa hiyo simba na yanga wamefanya jambo la maana kujitoa?
 
Ungeenza na wale wapuuzi wanaopanga ratiba hata haieleweki,wanaunga unga tu,Kagame cup nikama bonanza tu halina faida yoyote kwa timu za east Africa, timing yake mbovu,mfano Afcon inaendelea na mashindano yanaanza nani atakuwa busy na kagame???

Kabla ya kuleta Uzi ungempigia msonyi na genge lake waache upuuzi kwanza na wafanye mambo kwa weledi na si kijinga jinga hivi
Na vipi ushiriki wao mashindano ya sportipesa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom