Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,668
- 40,917
Mchakato wa kuanzishwa somo la historia ya Taifa letu umepingwa sana na wafuasi wa vyama vya upinzani hapa nchini.
Inashangaza kwa Raia kutotaka kujua historia ya Taifa lake.
Jambo la kusikitisha mno katika baadhi ya mijadala hapa jamvini unakutana na comment ya mtu ambaye anasema kwamba hakuwahi kujua kama Singida ipo katikati ya Tanzania na sio Dodoma, lakini mtu huyo huyo haoni umuhimu wa kuwa na somo la historia kuhusiana na Taifa lake.
Ninachokiona hapa ni woga tu usiokuwa na mashiko kwamba labda kwakua serikali iliyopo madarakani ni ya CCM basi itajipendelea na kujipa nafasi kubwa kwenye somo husika na mambo yahusuyo vyama vingine kutohusishwa kabisa.
Jamani tuacheni woga usiokua na msingi, kitachofundishwa ni historia ya Taifa sio maswala ya vyama.
Baada ya kusema hayo naomba Wizara husika iharakishe mchakato huo ili kuwapa fursa wanafunzi kujifunza maswala muhimu ya kitaifa.