Woga wa vyama vya Upinzani kuhusiana na Somo la Historia Ya Tanzania unatokana na nini?

Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,033
2,000
Mchakato wa kuanzishwa somo la historia ya Taifa letu umepingwa sana na wafuasi wa vyama vya upinzani hapa nchini.

Inashangaza kwa Raia kutotaka kujua historia ya Taifa lake.

Jambo la kusikitisha mno katika baadhi ya mijadala hapa jamvini unakutana na comment ya mtu ambaye anasema kwamba hakuwahi kujua kama Singida ipo katikati ya Tanzania na sio Dodoma, lakini mtu huyo huyo haoni umuhimu wa kuwa na somo la historia kuhusiana na Taifa lake.

Ninachokiona hapa ni woga tu usiokuwa na mashiko kwamba labda kwakua serikali iliyopo madarakani ni ya CCM basi itajipendelea na kujipa nafasi kubwa kwenye somo husika na mambo yahusuyo vyama vingine kutohusishwa kabisa.

Jamani tuacheni woga usiokua na msingi, kitachofundishwa ni historia ya Taifa sio maswala ya vyama.

Baada ya kusema hayo naomba Wizara husika iharakishe mchakato huo ili kuwapa fursa wanafunzi kujifunza maswala muhimu ya kitaifa.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
16,784
2,000
Kwani history inayosomwa sasa hivi ni tofauti na hiyo wanayotaka kuanzisha

Haya matapu tapu wanalishwa tu watoto wa masikini huko shule za vidumu na fagio.

Huwezi kuchezea elimu huko FEZA
 
Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,033
2,000
Singida kuwa katikati ya nchi ni Jiografia na si Historia. Elimu yako ina walakini, kuwa msomaji. Usianzishe mada, ficha ujinga wako
Angalia tu isijekua umenizidi huo ujinga,

Swala la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kwakua ni katikati ya Nchi na wakati sio hilo ni la kijiografia au??

Watu wengine bwana sijui kwanini huwa mnapenda sana kujiabisha.
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
28,658
2,000
Nje ya Mada,kwanini kila kitu kuilaumu Chadema
Chadema inasema wekeni tume huru ya uchaguzi ndio tujue.
 
Bepari2020

Senior Member
Nov 7, 2020
108
250
"History is written by victors"

Je itafundishwa historia ya kweli au propaganda? Historia ya kweli inaonyesha mazuri na mabaya lakini ni vigumu sana kwa serikali kukiri makosa iliyofanya. Kwa mfano historia ikionyesha mazuri aliyofanya Nyerere na bila kuyaonyesha mabaya aliyofanya, hiyo ni propaganda.
 
Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,033
2,000
"History is written by victors"

Je itafundishwa historia ya kweli au propaganda? Historia ya kweli inaonyesha mazuri na mabaya lakini ni vigumu sana kwa serikali kukiri makosa iliyofanya. Kwa mfano historia ikionyesha mazuri aliyofanya Nyerere na bila kuyaonyesha mabaya aliyofanya, hiyo ni propaganda.
Huo ndio wasiwasi wa vyama ambavyo havina dola,

Hawatakuwa sehemu ya somo,

Sidhani kama kitachozungumzwa na historia ya vyama,

Lakini unaitofautishaje CCM na historia ya nchi hii ??

Asilimia kubwa ya viongozi wa Kitaifa ambao wameplay role kubwa katika historia ya Taifa letu wanatokana na hicho chama. Itakua vigumu sana kutowahusisha.
 
Ukana Shilungo

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
2,827
2,000
Mchakato wa kuanzishwa somo la historia ya Taifa letu umepingwa sana na wafuasi wa vyama vya upinzani hapa nchini.

Inashangaza kwa Raia kutotaka kujua historia ya Taifa lake.

Jambo la kusikitisha mno katika baadhi ya mijadala hapa jamvini unakutana na comment ya mtu ambaye anasema kwamba hakuwahi kujua kama Singida ipo katikati ya Tanzania na sio Dodoma, lakini mtu huyo huyo haoni umuhimu wa kuwa na somo la historia kuhusiana na Taifa lake.

Ninachokiona hapa ni woga tu usiokuwa na mashiko kwamba labda kwakua serikali iliyopo madarakani ni ya CCM basi itajipendelea na kujipa nafasi kubwa kwenye somo husika na mambo yahusuyo vyama vingine kutohusishwa kabisa.

Jamani tuacheni woga usiokua na msingi, kitachofundishwa ni historia ya Taifa sio maswala ya vyama.

Baada ya kusema hayo naomba Wizara husika iharakishe mchakato huo ili kuwapa fursa wanafunzi kujifunza maswala muhimu ya kitaifa.
UPUUZI ULOANDIKA NA KUPOST UMETOKANA NA JINI???🤣🤣🤣🤣😁😁😁😃😃😃
 
Mayova

Senior Member
May 10, 2018
105
225
Badala ya kuisisitiza serikali iweke mikakati mizuri walimu wa masomo ya sayansi waongezwe wanafunzi wasome masomo ya sayanzi kama physics, chemistry, biology &maths wewe unataka serikali iongeze mzigo usio kua na maana kwa wanafunzi . Its non sense
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom