Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Kati ya mambo yanayoweza kumdumaza binadamu kwenye medani ya kujiendeleza na nchi kukua ni woga. Woga umewafanya watanzania kuwa watumwa kwenye nchi yao kwa kutawala mioyo na fikra za wananchi walio wengi kwa kiwango cha kutisha.
Hali ya woga imetanda kama wingu machoni mwetu kiasi cha kutoweza kuona na kuwa na mkakati wowote wa kujinasuru na jinamizi la ujinga na umasikini. Woga unatufanya tusiwe na ubavu wa kupambana na uovu miongoni mwetu kwa kujificha nyuma ya pazia hewa tunayoibatiza bila aibu kuwa ni amani na utulivu.
Woga umetulemaza kiakili kiasi cha kutoweza kufikiria njia mbadala ya kuondokana na serikali za kiimla na kibabe. Woga unalitafuna taifa na kuna hatari kuwa hali ikiendelea hivyo Taifa litaangamia. Kwa nini natamka mambo mazito kama haya na huo woga ni upi ?
Woga uliowafanya watanzania zaidi ya asilimia 80% wapige kura kukataa vyama vingi kwa kuogopa vurugu na vita na mpaka sasa kuna wanaoamini hivyo. Huu ni woga unaoletwa na ujinga.
Woga unaowafanya wananchi kuwa na imani na Rais aliyechaguliwa kwa idadi ya wapiga kura karibu 80% kusita kuchukua hatua madhubuti kupambana na uovu. Woga huu ni utii uliokubuhu (sycophancy).
Woga unaomfanya mbunge ashindwe kutetea maslahi ya wananchi waliomchagua awawakilishe kwa kuogopa kukaripiwa na chama chake cha siasa. Woga huu ni unafiki na ulafi.
Woga unaowafanya wananchi kwa wingi wao wakaridhika na tamko la serikali hadharani kuwa inawaogopa wenye pesa kwa kuwa wana nguvu ya kuiyumbisha nchi . Woga huu nauita uzembe.
Woga unaowafanya wananchi wasione umuhimu wa Raisi kuwajibika anapovurunda mambo ati hii kwa siasa ya bongo haiwezekani. Raisi ni binadamu tu wa kawaida na lazima awajibishwe akikoroga. Woga huu ni ukondoo.
Woga unaomfanya mwananchi aogope kuwalaumu na kuona mapungufu ya walio madarakani lakini yuko tayari kuwanyoshea kidole wapinzani wanaojaribu kutetea maslahi yake. Woga huu ni ukwepaji wa uwajibikaji.
Wananchi kuwapokea mafisadi wanaojiuzulu kwa vifijo na nderemo kunaelezea woga kwa wenye vijisenti. Huu woga hata hivyo unajificha ndani ya ukabila na hata hili hatuna ujasiri wa kuukemea.
Woga unaoifanya serikali kuchukua hatua za zimamoto kwa mambo yanayohitaji maamuzi makini ili kuwafurahisha wahisani. Bila shaka huu ni zaidi ya utumwa - ni usanii.
Woga wa kutoifikiria Tanzania bila CCM au kuisubiri imeguka ndio ati upinzani wa kweli upatikane. Huu ni uelemavu wa kiakili.
Je tufanye nini:
Huu si muda tena wa kukubali kuendelea kupumbazwa, kuzugwa na kudanganywa. Hata paka huweza kukimbizwa lakini akafikia mahali hana usalama tena na njia pekee ni kumparua mtu. Hivyo huu si muda tena wa kuendelea kulipalilia hili shamba la woga na kuliacha linastawi.
Hapana, serikali hii ya kisanii lazima iachie madaraka na isiachiwe nafasi hata ya kupumua kama haitafanya hivyo. Huu si wakati wa kupeana hongera bali kuongeza jitihada za kumtoa nyoka pangoni. Kilichoziba njia yetu kuelekea maendeleo ya kweli ni woga wetu tu ambao unatufanya kuwa wanyonge.
Tusichoweza kukifanya tusikiruhusu kuwa kisiki na kuzuia tunachoweza kukifanya kwa kuwa uwezo tunao, nia tunayo na sasa hivi kuliko wakati wowote mwingine sababu tosha kabisa tunayo.