Woga mkubwa wa Wabunge ni uchaguzi huru

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Wabunge wengi wanajifanya wanapenda mipango ya mpendwa wetu Magufuli lakini kelele zote za kusema Mama afanye ya Magufuli ni woga wa uchaguzi huru. Kama wabunge wanafanya kazi ya wananchi na wamechaguliwa kihalali uoga wa nini?

Tuwape siri tu mipango yenu sio mipango ya Mungu na kama wewe umepata kinyemela Mungu atatafuta njia za kurekebisha ili haki ipatikane.

Mama anapenda haki na sio muda ataweka viongozi kwenye tume ya uchaguzi ambao wana nia ya kupeleka nchi mbele na sio kutumia pesa kunyanyasa wananchi. Mama katokea Zanzibar ambao kule kuna ushindani ukiacha huu uchaguzi haramu wa mwaka jana. Sio kitu cha ajabu kule Zanzibar kufanya kazi pamoja kwasababu wanajua fika jinsi gani uhasama unaweza kuzuia maendeleo.

Hivyo ndugu zangu tuwapuuzie hawa wabunge ambao hawana nia na nchi. Badala ya kujali nchi wanajali matumbo mpaka leo hawana lipya. Hii ni awamu ya sita na Mama atanyoosha nchi kwasababu ana akili, anajua kujieleza, anaelewa mifumo ya serikali na matatizo ya Watanzania. Lakini Mama vilevile anajua cha kufanya ni nini. Kaimu wake Mpango anajua miradi yote ya Tanzania.

Tusubiri Tanzania iende mbele zaidi. Kuna watu wanapenda ugomvi kila siku watapata shida maana mama hana drama hizo.
 
Ukitaka kujua kwanini MUNGU ni fundi ni jinsi wabunge wanavyoparuana. Hizi drama ni mtaji na ushahidi Mkubwa ifikapo 2025 kwasabb wengi wao watakuwa hawana walilofanya zaidi ya kutetea chama Tu.

Wabunge wengi hivisasa wapo Kwenye makundi ya kimaslahi badala ya wananchi wao.
 
Hizi drama za kugombana wao Kwa wao ni mtaji Mkubwa Sana Kwa wapinzani kwasabb mpaka kutoka 2025 wabunge wengi watakuwa Kwenye makundi ya kimaslahi badala ya wananchi wao...hawa wajinga wameshagawanyika tayar bado kuzikwa
 
Dawa yao ni kuvunja BUNGE tuone wangapi wataludi ,ijulikane wanaccm angalau wenye mvuto wa kupanda jukwaani na kuleta ushindani wengi NDO waliachwa majimboni KWA malengo ya mwendazake, hasa lile la atake asitake lazima kuongezea mda, na mwaka huu usingeisha wangeongezea mda ,Sasa dawa ni kuvunja bunge
 
Usijindanganye kila aliye msaliti JPM Hawezi kurudi bunge. Sisi wananchi kila msaliti tunamjua
 
Hizi drama za kugombana wao Kwa wao ni mtaji Mkubwa Sana Kwa wapinzani kwasabb mpaka kutoka 2025 wabunge wengi watakuwa Kwenye makundi ya kimaslahi badala ya wananchi wao. Hawa wajinga wameshagawanyika tayar bado kuzikwa
Wapinzani wako wapi wa kutumia fursa ya mgawanyiko. Wao kila siku kuwaza kumkosoa marehemu hata kama hayupo.
 
Wapi amemtenganishwa na CCM? Mama ndio kajitenga na udhalimu wa yule ibilisi, hapa watu wanatoa mrejesho tu.
Tatizo upumbavu ndio unaowasumbua miaka yote, huyo unayemuita Ibilisi sasa hivi mwanzo mwa utawala wake mlimsifia sana hapa ila akaanza kubadilika kidogo kidogo sasa naona upumbavu hamjaacha mnarudia tena yaleyale kwa huyu Mama hata miezi sita hana hapo madarakani. Najua tu mlivyo wapumbavu najua tu lazima mtakuja tu kumtukana Mama wa watu maana ndio mpo hivyo miaka yote maana mnajulikana kwa upumbavu wenu.

Mimi nasisitiza tu kuwa huyo Mama ni Ccm.
 
Tafuta popote nilipowahi kumsifia ibilisi, sio akiwa rais hata alipokuwa waziri tu. Huyu mimi sijaanza kumsifu hadi zifike siku 100, ila kwasasa ni kwamba kaamua kujitenga na tabia za dhalimu.
 
Wabunge wengi wanajifanya wanapenda mipango ya mpendwa wetu Magufuli lakini kelele zote za kusema Mama afanye ya Magufuli ni woga wa uchaguzi huru. Kama wabunge wanafanya kazi ya wananchi na wamechaguliwa kihalali uoga wa nini?

Tuwape siri tu mipango yenu sio mipango ya Mungu na kama wewe umepata kinyemela Mungu atatafuta njia za kurekebisha ili haki ipatikane.

Mama anapenda haki na sio muda ataweka viongozi kwenye tume ya uchaguzi ambao wana nia ya kupeleka nchi mbele na sio kutumia pesa kunyanyasa wananchi. Mama katokea Zanzibar ambao kule kuna ushindani ukiacha huu uchaguzi haramu wa mwaka jana. Sio kitu cha ajabu kule Zanzibar kufanya kazi pamoja kwasababu wanajua fika jinsi gani uhasama unaweza kuzuia maendeleo.

Hivyo ndugu zangu tuwapuuzie hawa wabunge ambao hawana nia na nchi. Badala ya kujali nchi wanajali matumbo mpaka leo hawana lipya. Hii ni awamu ya sita na Mama atanyoosha nchi kwasababu ana akili, anajua kujieleza, anaelewa mifumo ya serikali na matatizo ya Watanzania. Lakini Mama vilevile anajua cha kufanya ni nini. Kaimu wake Mpango anajua miradi yote ya Tanzania.

Tusubiri Tanzania iende mbele zaidi. Kuna watu wanapenda ugomvi kila siku watapata shida maana mama hana drama hizo.
Umepiga penyewe kabisa maana karibu nusu ya wabunge Wa ccm hawakuchaguliwa kihalali
 
Back
Top Bottom