WM Majaliwa, maliza yote ya Faru John ili mengine yafanyike

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,068
2,000
Nianze kwa kukupongeza kwa namna unavyolishughulikia suala la Faru John. Tangu mwanzo wa sakata hili, Waziri Mkuu Majaliwa umekuwa ukionesha umakini, werevu na uthabiti wa kulifuatilia na kulimaliza suala la Faru John.

Nakujua. Najua uwezo wako mkubwa wa kiuongozi unaofanana na wa Rais Magufuli. Ndiyo maana mnaendana. Najua wajua mambo mengi kuhusu Faru John. Najua kuwa una kila taarifa nzuri, kali, za kutosha na kutisha kumhusu Faru John.

Tusaidie watanzania kufunga ukurasa huu wa Faru John. Anika mambo yote ya Faru John kadiri uyajuavyo. Wakuwajibika wawajibike; wasiohusika wasalimike. Kuna mambo mengi ya kufanya kama nchi. Faru John asitukwamishe muda wote huo kufanya mambo mengine.

Waumbue na uwatumbue tubadili mada!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,776
2,000
Maghembe yupo kwenye hali mbaya sana, awamu iliyopita aliitwa waziri mzigo awamu hii sijui ataitwa jangili
 

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,946
2,000
Ningeshukuru sana kama ungemshauri aache kwanza hiyo issue ya mnyama ashugulikie masuala ya binadamu ambao wameuwawa na kutupwa Ruvu na kutoonekana kwa Ben S8.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom