Wizi wizi mkubwa wa airtel kwenye moderm zao za promotion.

Muwe makini hao Airtel ndio wanafadhili huu mtandao msiwaseme vibaya!

When are you going to do this? Please do it now and whenever it happens. Do not wait until things worsen even further. I am also a customer at airtel. I have experienced this kind of trouble. When I contacted hao mabwana walishindwa kunijibu. Ni tatizo. Mambo haya ni kama yanavyotokea kwenye madini na mirahaba. Hao wanaoitwa wawekezaji ni tatizo sana nchi hii. Hakuna sheria zinazowabana wanaiba wanavyotaka halafu kesho wanabadilisha jina la kampuni mambo yao yanasonga mbele. Wasitufanyie huku Zenji, hawatavuka hata bahari.
 
Hawa airtell wamekuwa wakitangaza kuwa ukinunua moderm zao za tsh 30000.unapata ofa ya kutumia internet kwa miezi 6 huo niungo mkubwa na utapeli kwa watanzania wameshawaona Watanzania makondoo wanapeleka mambo kiwizi wizi tu ukweli ni kwamba wanakupa kifurushi tu cha 200mb kila mwezi wakati tangazo lao linasema utapata kutumia kwa miezi sita.Hivi wakuu hakuna namna ya kuwachukulia hatua wezi wa namna hii mwenye kujua taratibu au sheria za kibiashara atujuze tuone uwezekano wa kuwatia hatiani wezi hawa nawasilisha wakuu mwenye kutaka kuangalia tangazo lao lilivyo atizame hapo kwenye ubao wa matangazo ndani ya jukwaa hili la JF.

Na inawezekana pia tangazo hilo halikueleweka
 
Hilo ni kosa category ya 'deceptive advertising.'
Kule Marekani wana sheria kali sana kumrudi mtu anafanya deceptive advertising.
Kwa hapa kwetu sidhani kama sheria hiyo ipo. Na hasa makampuni ya simu ndiyo vinara wa deceptive advertising.

Labda tutumie uzi huu kuanzisha msala kufight deceptive advertising.
It's not healthy at all katika biashara!
 
Hawa airtell wamekuwa wakitangaza kuwa ukinunua moderm zao za tsh 30000.unapata ofa ya kutumia internet kwa miezi 6 huo niungo mkubwa na utapeli kwa watanzania wameshawaona Watanzania makondoo wanapeleka mambo kiwizi wizi tu ukweli ni kwamba wanakupa kifurushi tu cha 200mb kila mwezi wakati tangazo lao linasema utapata kutumia kwa miezi sita.Hivi wakuu hakuna namna ya kuwachukulia hatua wezi wa namna hii mwenye kujua taratibu au sheria za kibiashara atujuze tuone uwezekano wa kuwatia hatiani wezi hawa nawasilisha wakuu mwenye kutaka kuangalia tangazo lao lilivyo atizame hapo kwenye ubao wa matangazo ndani ya jukwaa hili la JF.

kwenye sheria ya mikataba kuna vitu viwili ambavyo nara nyingi usipokuwa maikini vinachanganya, kuna 'offer' na 'invitation to treat' sasa kituwanachokifanya airtel ni invitation to treat na sio offer, hivyo sio wezi na kisheria inaruhusiwa. kenye invitation to treat huwezi kum-'sue' muuzaji kwani wewe ndiye uliyealikwa kufanya manunuzi.
 
Nafikiri sasa serikali ione umuhimu wa kuyatazama haya mambo kwa jicho la tatu na sisi hatutakaa kimya kwenye suala hili hata kidogo haya mambo ya wizi wa kijanja kijanja ndio yanayoturudisha nyuma Watanzania tuweni macho kabisa.
 
We kiazi kweli kuna kitu wanaita terms&conditions apply(vigezo na masharti kuzingatiwa) hicho ndo kinga yao so kawadanganye viazi wenzio huko mashambani na si hapa !!!Mi nimehamia zantel unlimited downloads kwa 5000/= kwa wiki hapa nakaribia kumaliza muvi ya nne comptr sijaizima wiki ya pili sasa ni full kudownload!!:flypig:

nyie wote wale wale, nnji hii haina ISP wa hakika, mkongo wala mnini hakuna
 
We kiazi kweli kuna kitu wanaita terms&conditions apply(vigezo na masharti kuzingatiwa) hicho ndo kinga yao so kawadanganye viazi wenzio huko mashambani na si hapa !!!Mi nimehamia zantel unlimited downloads kwa 5000/= kwa wiki hapa nakaribia kumaliza muvi ya nne comptr sijaizima wiki ya pili sasa ni full kudownload!!:flypig:
Mkuu naona shule ya nguvu imekupitia kwa mbali.
Haya mambo waachie wanoyajua, mimi nilikua natoa hint tu.

Kwa vile umjionyesha wai kuwa ni mbumbumbu wa maswala ya "Law of Contract", basi kaa kimyA kama mtu anayenyolewa ufaidike na elimu ya bure ikusaidie wewe na nduguzo miaka mingi baadaye.

Airtel wametoa OFFER, na wewe ukiikubali offer hiyo kwa kuchukua hatua ya kununua hiyo bidhaa basi mnakuwa na CONTRACT na Airtel.
Sasa ukiwa mbumbumbu wa sheria utakubali Terms and Conditions kama utazipitia KABLA ya kununua, ukazikataa na bado ukauziwa huduma hiyo, Airtel watakuwa in breach of contract , kwani kwa kununua bila kukubaliana na terms zao, na wao wakakubali,bado contract inakuwa na nguvu.

At any rate watchout for the"terms and Conditions" clauses. Zinaweza kuwa unfair au ku exclude biashara yenyewe.
Kwa mfano ukiuziwa hiyo service halafu hizo terms zika sema hiyo service utaipata bada ya miezi miwili,na ni baada ya kununua.
That will bean unfair clause. Au baada ya kununua hupati kabisa sevice kwa muda wote, na Terms zikasema pesa yako hutarudishiwa, thats an exclusion clause.

Clauses hizo unaweza zipeleka mahakamani na waweza ukashinda kama hazikukutende haki.

Hili ni somo pana sana, sina uhakika hata hivyo kama utaelewa logic na kimombo chake, ndio maana kuna watu kama wewe wa shule za kata, na sisi Learned Brothers.
Botilo, umeelewa?
 
dah!hata mie kidogo niingie mkenge kununua hiyo moderm,nikawa nimechukua TTCL ukweli iko poa sana.poleni kwa wale mliyo ibiwa.
 
Wanaposema "masharti na vigezo kuzingatiwa" ndio hivyo, ingawa ww kama mteja hawakuelezi kwa undani. Hiyo 3.75G ni mazingaombwe tu, nadhani ni vice verse
 
Jaribu kununua hata kile kifurushi cha 2,500 400mb wanachosema kinadumu kwa mwezi, ni uongo, mi haijawahi kudumu hata wiki, just kusoma email na kujibu na hapo no download, hawa jamaa sio wakweli
Naomba nikufahamishe kitu ndugu yangu, wanapokuambia kifurushi cha mwezi maana yake ni kwamba "expire date" yake ni baada ya siku 30. Kwa hivyo kama matumizi yako siyo makubwa unaweza kukitumia ndani ya muda huo, na kama ni makubwa unaweza kukimaliza hata ndani ya dakika 10.
 
Hilo swala hata mimi nimeliona nafikiria kesho kwenda kwenye tume ya mawasiliano kupata ufafanuzi.

Mimi nilisikia hilo tangazo nunua moderm kwa 30,000 upate miezi sita bure, nikanunua nilipoulizia kuhusu hiyo offer ya miezi sita inakuaje? Akaniambia inabidi kwanza uweke 6000 baada ya hapo akaniambia kila mwezi nitakapokuwa naweka 6000 nitakuwa napewa 200mb kila mwenzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom