Wizi waibuka Bandari Dar- Magari yachomolewa vifaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi waibuka Bandari Dar- Magari yachomolewa vifaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Apr 25, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  HALI si shwari ndani ya Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kuibuka tena kwa wizi wa kutisha wa vifaa mbalimbali katika magari yanayotoka nje ya nchi. Habari za ndani kutoka Bandarini zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa takribani mwezi mmoja sasa, magari yote yanayotoka nje ya nchi yanakuwa hayana ripoti ya ukaguzi (VIR) inayoonesha vifaa vyote vilivyomo katika magari hayo, jambo ambalo limesababisha kuibuka tena kwa wizi.

  Taarifa hizo zimeeleza kuwa wateja wa magari hayo wanapofika katika Bandari za Nchi Kavu (ICD) kwa ajili ya kuchukua magari yao hukuta yameibwa vifaa mbalimbali na kwamba wakitoa malalamiko yao huelezwa kuwa hakuna ushahidi kwa kuwa magari hayo hayakuwa na VIR. Zinaeleza kuwa wizi huo uligundulika baada ya meli mbili za magari kuwasili katika bandari hiyo hivi karibuni kasha magari hayo kushushwa na kupelekwa katika ICD zilizopo maeneo ya Kamata na Chang’ombe jijini humo. “Asilimia kubwa ya magari yaliyokwenda kuchukuliwa na wateja katika bandari hizo kavu yalikutwa hayana vifaa mbalimbali kama redio, betri, vioo vya pembeni na vifaa vingine,” zilieleza taarifa hizo kutoka kwa chanzo chetu cha habari bandarini hapo.

  Chanzo hicho kilifafanua kwamba wateja baada ya kubaini hali hiyo waliwasilisha malalamiko yao kwa uongozi wa Bandari hizo za nchi kavu na kujibiwa kuwa magari hayo yalipelekwa eneo hilo yakiwa hayana VIR. “Magari yanafika nchini yakiwa na vifaa vyote, tatizo lipo Bandarini na tunadhani wanaofanya wizi huo ni madereva wanaoendesha magari hayo kutoka Bandarini mpaka katika ICD,” kilieleza chanzo chetu. “Uongozi wa ICD umeliweka wazi suala hilo na kuwataka wateja kuandika barua juu ya wizi huo kisha wao wathibitishe na baada ya hapo wazipeleke barua hizo kwa uongozi wa bandari ya Dar es Salaam ili wateja waliobiwa vifaa katika magari yao waweze kusaidiwa,” zilieleza taarifa kutoka kwa chanzo hicho.

  Habari zaidi zilieleza kuwa Bandari ndio wanaopaswa kulaumiwa kwa kuruhusu magari hayo kuingia nchini bila kuwa na VIR. Akizungumzia suala hilo, Meneja wa Bandari hiyo, Cassian Ngamilo alisema kuwa atatoa ufafanuzi wa kina kuhusu jambo hilo Ijumaa wiki hii. “Sipo Dar es Salaam kwa sasa, ila awali tulikuwa tumepanga kufanya mkutano na waandishi wa habari ili tutoe ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayoihusu Bandari maana kuna taarifa zinatolewa ambazo zinawachanganya watu,” alisema Ngamilo.

  Hata hivyo, Ngamilo ambaye wakati anazungumza na Mwananchi alikuwa Tanga alisema kuwa wateja wa magari hayo wanatakiwa kutoa taarifa za wizi huo kwa uongozi wa bandari na sio kulalamika pembeni kwani hakuwezi kuwasaidia.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wiki moja na nusu nilipotoa gari yangu bandarini nilikuta wiper ya nyuma imenyofolewa na head rest za viti vya kati vimechomolewa, hiyo ndiyo bandari ya Darisalama.
   
 3. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwani hamjui jina la bandari yetu inaitwaje "BANDARI SI-SALAMA" hii ndio bongo nizaidi ya ujuavyo....
   
 4. f

  fardia Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sioni sababu ya kuwa na bandari za nchi kavu zinazomilikiwa na watu binafsi. Hivi kweli serikali imeshindwa kutafuta endeo la kutunza hayo magari?
   
 5. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  huo wizi haujaibuka, sema unaendelea maana ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo pale bandarini
   
 6. Jayfour

  Jayfour Senior Member

  #6
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tanzania kila mtu mwizi, na hasa baada ya kukata tamaa ya maisha yasiyokuwa na matumaini.
   
 7. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,840
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Who cares My friend? Hii Nchi Mwizi Anaitwa Mjanja!! Au ndio ajira 1,000,000? Basically Kuudhibiti huu wizi ni very simple ila Hakuna mwenye Nia ya dhati!! Nia ni Just Kuajiri Reputable security company kutake care na Ulinzi wa mali za Wateja wetu!! Wazambia, Wamalawi, Wakongo, Waburundi etc!! Pia Mali zetu wenyewe!!
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Niliamua tu kuondoka na gari maana kuanza kufuatili kungenighalimu muda wangu zaidi.

  Nakubaliana nawe, kwa nini wasitenge eneo ambalo ni sehemu ya bandari chini ya usimamizi wao wenyewe na hivyo kurahisisha inapotokea dosari, lakini hii ya watu binafsi kuwa inaleta mgongano inapotokea wizi kama huu.

  Hali kadhalika inaongeza gharama, maana ukiagiza gari nje, licha ya gharama za ushuru wa forodha, kuna ushuru wa bandari na tena unaongezwa kwa kiwango hicho hicho ushuru wa bandari kavu kwa huyo mtu binafsi. Hii ni kuongeza gharama ambazo ni mzigo kwa wanunuzi wa magari. Sasa dhana ya maisha bora kwa kila mtanzania imekaaje?
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Vifaa mbalimbali vya magari huibwa na madreva watoapo magari toka kwenye meli wawapo njiani kuyapeleka lot za chang'ombe na sehemu nyingine jina limenitoka. Kwa nini magari hayo yanapoingia hapo hawayakagui kama ni salama tangu yatoke bandarini? Na kama wizi umetokea pale lot gari linapotoka wenye lot wanatakiwa kulipia gharama za wili uliotokea kwenye lot yao. Kumbuka magari haya hulilipiwa bina ya usafirishaji toka yanakonunuliwa.
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Kabisa haujawai isha wizi bandarini
   
 11. nxon

  nxon JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,149
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  hii ni laana kila mtanzania ni mwizi
   
 12. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii VIR (Vehicle Inspection Report) Inaandikwa pale gari ikitoka melini na Chief officer au Captain wa meli huisaini kukubali ya kuwa hilo gari hivyo vitu vilivyoandikwa vipo au vimemiss.

  Mteja wakati wa kuchukua gari lake kabla ya kuanza kuitupia lawama mamlaka ya bandari, inampasa kwanza kuangalia VIR kama wakati gari linashuka walirekodi kama redio, au power window n.k je vilikuwepo wakati wa upakuzi kutoka melini au la! VIR ndio itakupa majibu.
  Kama havikuandikwa wakati gari linashuka, maana yake vimekwapuliwa huko huko melini. naomba udeal na transport wako.
  Na kama VIR inaonyesha gari imeshuka na vifaa vyote wakati wa kulichukua gari lako unaona kuna vitu hamna basi wewe lia na Bandari.

  Kabla gari haijafika hapa nchini kuna Bandari kadha wa kadha meli inapita, sasa basi mfano imepita Cape town, au Mombasa kabla ya kuja huku nchini, na wakati wa upakuzi wakakwapua kule wakati wakitoa magari ya kwao na wale ma Crew wa meli hawakuwa makini....! huwezi jua

  Ection zinachukuliwa sana tu na Usiwe mnyonge fuatilia haki yako ukweli utajulikana tu, na hatua zinachukuliwa juu ya wote wanaosababishia Bandari kila siku inatupiwa lawama

   
 13. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Tafadhali ndugu hata kama uzao wenu wote ni wezi lakini usiseme ''kila mtu''. Mtu kama mimi nafanya kazi, naamini katika kazi na sitaki kabisa kusikia habari za wizi.
   
 14. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #14
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu! ni hatua gani ambazo zimechukuliwa? unaweza kututajia?.........kwa sababu watu bado wanalizwa!
   
 15. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #15
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hawa jamaa wanakatisha tamaa sana bora upitishie gari mombasa au horohoro Tanga
   
 16. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hilo la wizi katika bandari ya Salama hata sio mgeni.
  Na wakubwa wanajua fika lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.
   
 17. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,814
  Likes Received: 20,786
  Trophy Points: 280
  Ur right mkuu,watu wanalaumu TPA tu wakati mwingine vifaa vinaibiwa bandari za nje ambako m?li inaanza kushusha magari hasa bandari za west africa ni wezi mara mia ya wabongo!wanaiba hadi milango achilia mbali power windows
   
 18. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Duh! Bora nifate gari south kwa mzee madiba nipige gia mpaka tunduma to dar city kwanza hata gharama nafkir ni ndogo kuriko kuibiwa viungo vya gari langu. Harafu mnasema wanaiba watu wa west afrika mbona magari kutoka japan pale capetown ayanyofolewi viungo au ayabebwi na meli hizi zinazobeba magari yetu huu ni mchanganyiko wa maisha bora na zile kasi mpya
   
 19. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Mbona wamezoea kuiba?Yaani hawa jamaa wanachomoa kila kinachowezekana!!Muda ukiruhusu,wanabadilisha Rim na matairi!!!
  Ila,kama maboss wao wanaiba mchana kweupe,wao wafanyeje?Tuanze kuwawajibisha wa ngazi za juu kwanza!!!
   
 20. F

  Fofader JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Zile CCTV tulizoambiwa zimewekwa zimeshakufa?
   
Loading...