Wizi wa zaidi ya mil 100 za Wanafunzi Chuo cha IFM

Rwatami

Member
Sep 26, 2013
6
20
Chuo cha usimamizi wa fedha IFM kilichoko jijini Dar es salaam kimepoteza pesa zaidi- ya shilingi Milioni 100 na kusababisha deni la ml. 83.katika mazingira ya kutatanisha na yaliyoghubikwa na usiri mkubwa. Chanzo chetu cha habari kimebaini kuwa waliohusika katika kufanikisha wizi huo ni pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi IFMSO, watendaji kwenye ofisi ya mshauri wa wanafunzi na viongozi wakubwa wa chuo hicho.

Pesa zilizoibiwa zinatokana na michango ya wanafunzi ambapo kila mwanafunzi humulazimu kuchangia shilingi 10,000 kila mwaka kama ada ya serikali ya wanafunzi. Fedha hizo zililipwa na wanafunzi kwa wakati tofauti kupitia akaunti za chuo zikiambatana na ada ya masomo.

Baadaye fedha hizo za IFMSO za kila mwanafunzi zinaamishiwa kwenye akaunti ya serikali ya wanafunzi (IFMSO account) ili zitumike katika kuendeshea shughuli za serikali ya wanafunzi.

Upotevu wa fedha hizo uligundulika pale viongozi wa serikali ya wanafunzi ya 2013/2014 iliyokuwa ikiongozwa na Bw Hemed Ally walipoanza kudai fedha za wanafunzi zitumike kutekeleza shughuli mbalimbali kama ilivyopangwa, ofisi ya mshauri wa wanafunzi iliwaambia kuwa akaunti ya IFMSO haina pesa na kuwa inadaiwa deni la ml.83 ambazo zinapaswa kulipwa na serikali ya wanafunzi.

Upotevu wa fedha hizo ulilileta mgomo ndani ya viongozi wa serikali ya wanafunzi ambapo viongozi waligoma kufanya kazi baada ya kutolipwa posho zao za miezi minne kwa kigezo kuwa akaunti ya IFMSO haina ela na inadaiwa ml. 83. Baada ya mgomo huo kuwa mkali uliopelekea kugoma kukabidhi madaraka kwa serikali mpya na kutishia kuita vyombo vya habari kuripoti ubadhilifu huo viongozi hao walilipwa posho kutoka kwenye akaunti ya chuo.

Chanzo chetu kimechunguza habari hii kwa undani tangu kuwepo kwa malalamiko ya viongozi wa serikali ya wanafunzi ya mwaka 2013/2014 iliyoongozwa na kugundua kuwa jambo hili lilileta mtafaruku mkubwa ndani ya serikali ya wanafunzi na uongozi wa chuo, kwani kila upande ulikuwa ukikanusha kuwa haujatumia pesa hizi.

Suala la deni hewa ml.83 lihojiwa kwenye kikao cha bodi ya wadhamini wa IFMSO na hawakupata majibu ya kuridhisha kutoka kwa wahusika. Kila mtu alikuwa akishangazwa na upotevu wa fedha hizi na vikao kadhaa vilikaaa kutafuta majibu ya jambo hilo ambayo haikuwa raisi kuyapata. Aidha, katibu mtendaji wa bodi ya wadhamini wa IFMSO alimwandikia barua mkuu wa chuo akiomba bodi kupewa mafaili ya akaunti ya IFMSO ili yapitiwe kubaini tatizo liko wapi, hata hivyo hakutoa taarifa yoyote ya kilichoendelea juu ya pesa hizo za wanafunzi.

Uchunguzi wetu ulibaini kuwa kuna mihamala kadhaa iliyofanyika kwenye akaunti hiyo ya IFMSO kwenda- kwa watu binafsi wakiwemo watumishi wa chuo wakiwemo watendaji ndani ya ofisi ya mshauri wa wanafunzi, viongozi wakuu wa IFMSO na ofisi ya muhasibu. Pia imegundulika kuwa kuna baadhi ya viongozi wa chuo wanahusika kwenye sakata hili ndio maana wamekuwa wakilikumbatia na kutotaka kulifanyia kazi kujua pesa ilienda wapi.

Watu waliobainika kuchukua pesa ni pamoja na Mr Semkiwa, ambaye ni mtumishi, Bw Agustino aliyekuwa Kiongozi serikali ya wanafunzi, Mwalimu Rashidi ambaye ni ofisa mshauri wa wanafunzi, Emmanuel Mushi aliyekuwa mshauri wa wanafunzi, Hemedi Ally ambaye alikuwa rais wa serikali ya wanafunzi na viongozi wakuu wa chuo hicho.

Pesa hizi zimelipwa na wanafunzi maskini ambao wazazi wao wanajinyima na kuuza mali zao ili watoto wao wasome, cha kushangaza baadhi ya watu waliopewa dhamana ya kusimamia maslahi ya wanafunzi hawa wanajineemesha wenyewe huku wanafunzi wakiendelea kuteseka kwa kutokuudumiwa vizuri na serikali ya wanafunzi kwani wakati mwingine mwanafunzi akiumwa hapatiwi msaada wowote na amechanga pesa hiyo.

Upotevu wa fedha kama hizi za wanafunzi uliwahi kutokea nchini Malaysia katika chuo cha Wawasani (WOU) na kusababisha mgomo mkubwa kwa wanafunzi waliokuwa wakichanga pesa hizo. Ni wakati wa mamlaka zinazohusika na IFM sasa kuchukua hatua stahiki kwani suala hili si la kufumbia macho na watu ambao ni wasomi maprofesa wakaendelea kujineemesha huku watoto wa maskini wanaotaka kusoma kufikia hapo wanaibiwa.-
 
Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,636
2,000
Huwa mna mkutano wa kusomewa Mapato na matumizi?

Huwa mna mkutano wa kupitisha pesa za matumizi?

Ni nani Mwenye jukumu la kusimamia Fedha za wanafunzi?

Ni nani anatoa ruhusa za fedha kutoka?

Ni nani amethibitisha kuna upotevu wa pesa hizo?

Kafungueni case!
 
Jungumawe

JF-Expert Member
May 2, 2009
249
195
Huwa mna mkutano wa kusomewa Mapato na matumizi?

Huwa mna mkutano wa kupitisha pesa za matumizi?

Ni nani Mwenye jukumu la kusimamia Fedha za wanafunzi?

Ni nani anatoa ruhusa za fedha kutoka?

Ni nani amethibitisha kuna upotevu wa pesa hizo?

Kafungueni case!
Mmmmmh sasa inakuwaje chuo cha usimamizi wa fedha au chuo cha ubadhirifu wa fedha sielewi wanafundisha nini hapa
 
bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,040
2,000
Ni kawaida hela kupigwa ukiwa Rais wa wanafunzi chuoni ukashindwa kununua ata baloon ujue wewe ni mtakatifu. UKAWA MBELE DAIMA.
 
Gsana

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
4,399
1,500
Ni kawaida hela kipigwa na mara nyingi uongozid WA ifmso uwekwa na viongozi wa chuo ili kuzibabua kirahisi, ni kama 2008 au 2009 wakati wa rais mdoe aliyenunua AC/kiyoyozi kwa mil10 kila a.c ....yani matumizi
yale yalikuwa vichekesho!! Na baada ya kuleta auditors hakuna kilichowezekana na akina mdoe wakadunda mtaani, iyo ndio IFM bhana"!!
 
MO11

JF-Expert Member
Mar 23, 2014
17,450
2,000
Huwa mna mkutano wa kusomewa Mapato na matumizi?

Huwa mna mkutano waw kupitisha pesa za matumizi?

Ni nani Mwenye jukumu la kusimamia Fedha za wanafunzi?

Ni nani anatoa ruhusa za fedha kutoka?

Ni nani amethibitisha kuna upotevu wa pesa hizo?

Kafungueni case!
huyu ndio Ruttashobolwa yule mwengine anayetetea ccm ni fake.
 
Last edited by a moderator:

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,159
2,000
We unafikiri zile mbwembwe za kukodi magari ya kifahari, printing t-shirts, vipeperushi e.t.c hela itarudi vipi?
 
kunguni wa ulaya

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
4,048
2,000
Hao jamaniwamezoea.hapo IFMSO hawajaanza leo. Kwa ninaowajua mimi Ysuf Mdoe na Benard Lupungu waliiba mamilioni hivyohivyo. Mdoe hadi alienda Bagamoyo inavyosemekana kwa mganga ili kuyafifilisha hayo mambo yasifike mbali
 
JICHO TAI

JF-Expert Member
May 27, 2013
1,110
1,500
wewe Rwatami ukiambiwa utoe ushaidi utautoa? do you know exactly how IFMSO account operates? do you know the history of the account? maana wewe umeongelea 2013/2014 vipi miaka ya nyuma? unajuaje kama account au chama chenu kina madeni? don't jump on issues! najua ninachokisema.
 
uvungu

JF-Expert Member
Nov 30, 2014
384
250
Daaah inauma sana nikiwa mmoja kati ya wahitimu wa chuo kile mi toka nimeanza kusoma had nimemaliza cjawah ona tunakaa kikao kupitisha matumizi sir I kubwa wanayo ifmso
 
Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
7,593
2,000
Chuo cha usimamizi wa fedha IFM kilichoko jijini Dar es salaam kimepoteza pesa zaidi- ya shilingi Milioni 100 na kusababisha deni la ml. 83.katika mazingira ya kutatanisha na yaliyoghubikwa na usiri mkubwa. Chanzo chetu cha habari kimebaini kuwa waliohusika katika kufanikisha wizi huo ni pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi IFMSO, watendaji kwenye ofisi ya mshauri wa wanafunzi na viongozi wakubwa wa chuo hicho.

Pesa zilizoibiwa zinatokana na michango ya wanafunzi ambapo kila mwanafunzi humulazimu kuchangia shilingi 10,000 kila mwaka kama ada ya serikali ya wanafunzi. Fedha hizo zililipwa na wanafunzi kwa wakati tofauti kupitia akaunti za chuo zikiambatana na ada ya masomo.

Baadaye fedha hizo za IFMSO za kila mwanafunzi zinaamishiwa kwenye akaunti ya serikali ya wanafunzi (IFMSO account) ili zitumike katika kuendeshea shughuli za serikali ya wanafunzi.

Upotevu wa fedha hizo uligundulika pale viongozi wa serikali ya wanafunzi ya 2013/2014 iliyokuwa ikiongozwa na Bw Hemed Ally walipoanza kudai fedha za wanafunzi zitumike kutekeleza shughuli mbalimbali kama ilivyopangwa, ofisi ya mshauri wa wanafunzi iliwaambia kuwa akaunti ya IFMSO haina pesa na kuwa inadaiwa deni la ml.83 ambazo zinapaswa kulipwa na serikali ya wanafunzi.

Upotevu wa fedha hizo ulilileta mgomo ndani ya viongozi wa serikali ya wanafunzi ambapo viongozi waligoma kufanya kazi baada ya kutolipwa posho zao za miezi minne kwa kigezo kuwa akaunti ya IFMSO haina ela na inadaiwa ml. 83. Baada ya mgomo huo kuwa mkali uliopelekea kugoma kukabidhi madaraka kwa serikali mpya na kutishia kuita vyombo vya habari kuripoti ubadhilifu huo viongozi hao walilipwa posho kutoka kwenye akaunti ya chuo.

Chanzo chetu kimechunguza habari hii kwa undani tangu kuwepo kwa malalamiko ya viongozi wa serikali ya wanafunzi ya mwaka 2013/2014 iliyoongozwa na kugundua kuwa jambo hili lilileta mtafaruku mkubwa ndani ya serikali ya wanafunzi na uongozi wa chuo, kwani kila upande ulikuwa ukikanusha kuwa haujatumia pesa hizi.

Suala la deni hewa ml.83 lihojiwa kwenye kikao cha bodi ya wadhamini wa IFMSO na hawakupata majibu ya kuridhisha kutoka kwa wahusika. Kila mtu alikuwa akishangazwa na upotevu wa fedha hizi na vikao kadhaa vilikaaa kutafuta majibu ya jambo hilo ambayo haikuwa raisi kuyapata. Aidha, katibu mtendaji wa bodi ya wadhamini wa IFMSO alimwandikia barua mkuu wa chuo akiomba bodi kupewa mafaili ya akaunti ya IFMSO ili yapitiwe kubaini tatizo liko wapi, hata hivyo hakutoa taarifa yoyote ya kilichoendelea juu ya pesa hizo za wanafunzi.

Uchunguzi wetu ulibaini kuwa kuna mihamala kadhaa iliyofanyika kwenye akaunti hiyo ya IFMSO kwenda- kwa watu binafsi wakiwemo watumishi wa chuo wakiwemo watendaji ndani ya ofisi ya mshauri wa wanafunzi, viongozi wakuu wa IFMSO na ofisi ya muhasibu. Pia imegundulika kuwa kuna baadhi ya viongozi wa chuo wanahusika kwenye sakata hili ndio maana wamekuwa wakilikumbatia na kutotaka kulifanyia kazi kujua pesa ilienda wapi.

Watu waliobainika kuchukua pesa ni pamoja na Mr Semkiwa, ambaye ni mtumishi, Bw Agustino aliyekuwa Kiongozi serikali ya wanafunzi, Mwalimu Rashidi ambaye ni ofisa mshauri wa wanafunzi, Emmanuel Mushi aliyekuwa mshauri wa wanafunzi, Hemedi Ally ambaye alikuwa rais wa serikali ya wanafunzi na viongozi wakuu wa chuo hicho.

Pesa hizi zimelipwa na wanafunzi maskini ambao wazazi wao wanajinyima na kuuza mali zao ili watoto wao wasome, cha kushangaza baadhi ya watu waliopewa dhamana ya kusimamia maslahi ya wanafunzi hawa wanajineemesha wenyewe huku wanafunzi wakiendelea kuteseka kwa kutokuudumiwa vizuri na serikali ya wanafunzi kwani wakati mwingine mwanafunzi akiumwa hapatiwi msaada wowote na amechanga pesa hiyo.

Upotevu wa fedha kama hizi za wanafunzi uliwahi kutokea nchini Malaysia katika chuo cha Wawasani (WOU) na kusababisha mgomo mkubwa kwa wanafunzi waliokuwa wakichanga pesa hizo. Ni wakati wa mamlaka zinazohusika na IFM sasa kuchukua hatua stahiki kwani suala hili si la kufumbia macho na watu ambao ni wasomi maprofesa wakaendelea kujineemesha huku watoto wa maskini wanaotaka kusoma kufikia hapo wanaibiwa.-
Source plz!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom