Wizi wa wanyama kutumia ndege ya kijeshi: Hili ni suala la Rais kutueleza kilichojiri

Jambo moja linaloniudhi kila siku ni jinsi watanzania tunavyochukuliwa kuwa malofa na mataifa mengine. Habari iliyopo katika magazeti ya Guardian Ltd ni kwamba Qatar walitumia ndege ya kijeshi kuiba wanyama toka Tanzania, ndege iliyotua pale KIA na kuondoka majira ya alfajiri na mapema na wanyama 116.

Hili si jambo ndogo. Ni uhaini wa hali ya juu kwamba ndege ya jeshi la nchi nyingine inaweza kuingia kinyemela nchini na kuondoka. Nani katika jeshi alitoa kibali cha ndege hiyo si tu kuingia anga la Tanzania bali hata kutua, kwa mamlaka ya nani? Ina maana ndege kubwa ya jeshi jingine inaweza kutua nchini bila JK, raisi wa nchi kuwa na taarifa? Na kama raisi alijua aliambiwa inakuja kufanya nini? Na huko Qatar, nani aliruhusu hiyo ndege ya jeshi kuja Tanzania kuchukua wanyama? Nani katika jeshi au serikali za Tanzania na Qatar walijua? Au labda Maige amesema kweli kwamba katolewa kafara?

Inakuwaje nchi inaruhusu hali ambayo inaweza hata kuingiza askari mamluki (mercanaries) kwa kutumia ndege kubwa ya kijeshi na wala lolote lisifanyike? Viongozi wanatenda kulingana na kiapo cha ofisi walic


View attachment 56608
Ndege ya kijeshi ya Qatar iliyotumika kuiba wanyama Tanzania pale KIA

Source: IPP Media

Tanzania tunawasomi waliobobea kwenye tasnia ya habari. Hawa waandishi ya kiuchunguzi wako wapi????????
Taifa lina mambo mengi yanayoitaji uchunguzi wa kina AU wao wamebobea kwenye nyanja ya taarifa za udaku?
 
Mbona nilishawahi sikia kuwa huko Arusha kunamahali wameuziwa waarabu kipindi cha mwinyi na ni milki Yao wanaruhusiwa kuingiza ndege na kuondoka bila kuuluzwa? Kama hii ilitokea KIA je kwenye Kiwanja Chao wameondoka wangapi? Tunahitaji majibu kutoka kwa Raised! Huu ni uchezeaji wa mipaka yetu!
 
Nashawishika kuamini rais aliwatoa hao wanyama kama zawadi kwa waarabu, haingii akili dege la kijeshi la taifa jingine litue lipakie wanyama na jamaa wawe wanalichekea chekea hivi hivi.
 
Kiongozi,hili suala lisiwaumize kichwa sana nchi hii ishauzwa. Hii issue ilisukwa na wakubwa wote wanahusika including viongozi wa vyama vya upinzani wanajua na walihusika kwa asilimia zote. Hivi hamuoni kwamba pamoja na ufukunyuaji maovu wote unaofanywa na chadema hawajawahi kulivalia njuga hili swala? The deal was in the making way back in 2009 Dr.Slaa akiwa bado mbunge tena machachari kabisa wa kupinga ufisadi na ubadhilifu. Msiumize vichwa bana tujadili mambo mengine. Wote Slaa,Mbowe,Zitto wanajua na waliupokea mgao wao vizuri sana. Asante.

BACARD usiambukize wengine kilevi chako tafadhali. Naamini wote tunaumizwa na mambo yayoendelea katika nchi hii. lakini isiwe sababu ya kutaka kuwachafua watu wengine ambao hawahusiki.

Dr. slaa, Mbowe na Zitto walikuwepo bungeni ila ukumbuke hawako kwenye system ya serikali. hivyo hawawezi kukurupuka kama hawajapata taarifa na kuzifanyia kazi na kujiridhisha kuwa zina ukweli. ukumbuke kuwa pamoja na kuwa viongozi wa kitaifa lakini hawana upenyo wa kujua kila kinachoendelea ndani ya serikali kwa kile kinachoitwa "siri za serikali". kwa kuwa wao wanafanya kazi nje ya mfumo wa serikali.

Ila tu pale wanapopata taarifa ndipo wanapoweza kuzifanyia kazi na kuanza kufuatilia, wakipata uhakika ndipo wanaweza kulisema hadharani.

Kwa hiyo kutolisemea haina maana kuwa wanahusika na wamepata mgao. inawezekana hawajapata taarifa au wamepata wakashindwa kupata uthibitisho wa kutosha kwao kulisema.

Hata wewe mwenyewe hukulileta hapa JF tulijadili ina maana nawewe ulipata mgao??
 
Bacardi naona kwenye hili unaweza ukatupa ukweli coz inaonekana unalijua vizuri, tuambie ilikuwakuwaje na Dr. Slaa na wenzake wakapokea mgao naomba utufungue zaidi. Lkn usije ukawa unaenda kuwauliza kina ritz, panadol, tume ya k. . . na wenzake kwa sababu kwenye hoja hii ya ukweli wanakaa kimya kidogo lkn lazima wamuulize Nape kwanza wasije wakaharibu
 
Tukihoji hili kwa upande wa jeshi, Pinda atasema maswala haya yanayohusu utendaji wa jeshi ni siri hivyo basi tukae kimya lishuhulikiwe kwa umakini na siri kubwa, ila kiukweli hakuna SIRI YA JESHI zaidi ya "when to attck"( Mda wa kuanza kumshambulia adui ndo siri pekee jeshini).

Tafathali tusikubali kuzibwa mdomo kwa kisingizio cha SIRI ZA JA JESHI.

Juzi katika habari nimeona wajanja flani(nimewakubali kiaina) wamekamatwa na maboga ya sumu walitumia kutegea tembo mbugani,Sasa hebu imagine kifungo watakachofungwa while hawa ndio wanaopaswa kupata gawio kubwa la keki ya taifa.

Naamini pesa zinazopatikana kupitia mbuga zetu zingetumika kihalali kumnufaisha mtanzania kwa nia ya kumkwamua kwenye umaskini basi hawa majangili wasingefanya huu ujangili,.

Aliyekamatwa na maboga ya sumu na aliyesafirisha wanyama hai tena kwa ndege ya jeshi ni nani kati yao anapaswa kuburuzwa mahakamani nakuhukumiwa kifungu kirefu???

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
siamani kama ni kweli waandishi wa habari za uchunguzi na wapinzani wameshindwa kupata data juu ya hili swala.!
 
Waziri Mh Kagasheki kakiri utajiri wa raslimali za asili Tanzania ni mwingi sana. Lakini naona tatizo ni waliopewa dhamana ya kuzisimamia. Uchoyo na uroho wao, Hakika udhibiti ni dhaifu, ni kama mafisi wanaogombea nyama. Total reform/overhaul in the WL sector is necesary, there is total lack of transparency, accountability and responsibility. Shame on you people for your greedy!
 
naam na MPAMBANAJI STAN KATABALO alilipa gharama ya habari zake za kiuchunguzi kwa zawadi isiyo na akiba yaani alikufa kifo usichoweza kukiita cha asili.Tena ukienda eneo hilo eti simu yako inakukaribisha ...karibu UAE yaani Falme za Kiarabu......ukishangaa ya Serikali ya CCM utayaona ya Firauni!
 
Back
Top Bottom