Wizi wa vitu kwenye magari si Mlimani City pekee, hata ukipaki benki wanakomba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi wa vitu kwenye magari si Mlimani City pekee, hata ukipaki benki wanakomba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bassanda, Jul 14, 2010.

 1. Bassanda

  Bassanda Member

  #1
  Jul 14, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Salam zenu wana JF. Kuna taarifa za uhakika kwamba wizi wa vitu kama laptop na "pawa windo" kwenye magari yaliyoegeshwa haufanyiki Mlimani City pekee, bali ni mji mzima wa Dar es Salaam kwa sasa, kuanzia majumbani hadi kwenye mabenki! Siku chache zilizopita kuna mdau alipaki gari yake nje ya Benki ya CRDB Mbezi Beach akaacha laptop akiwa ameifungia ndani ya gari, labda kwa kuamini kwamba pale ni Benki kuna ulinzi wa polisi, na walikuwepo. Cha kushangaza muda mchache wa dakika 20 alizokaa mle ndani ya Benki kutoka akakuta kioo cha gari kimevunjwa na laptop imeambaa na wakora, polisi nao wakiwa nje ya jengo eti huko ndiyo wanakokaa. Eneo jingine hatari ni Chuo Kikuu Mlimani ambao kila leo wanafunzi kwa walimu wanalizwa. Hao vibaka wanatumia magari na kuegesha pembeni ya gari lako kisha wanafanya mavitu yao na kutokomea, ni vibaka middle class hawatembei kwa miguu. Sasa kama wanashirikiana na walinzi au askari kwenye maeneo husika hicho ni kitendawili. Kwa hiyo haijalishi una mpango wa kufanya transaction benki na una sanduku lako ndani ya gari we ingia nalo tu Benki kwani ukiliacha utakuta kioo kimevunjwa na sanduku limeyeyuka. Hiyo ndiyo habari.
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ndo bongoland hiyo! Akili kukichwa.
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,435
  Likes Received: 2,310
  Trophy Points: 280
  Jambo ambalo mimi huwa nalikata kata kata ni kuiita Tz eti bongoland. Hivi watanzania tunatumia ubongo gani? Ningekuwa na furaha zaidi kama tungejiita bongolala.
  Back to issue ya vibaka.... this is just the beginning. Unategemea nini kwa nchi ambayo chama kinachotawala kinapofanya mkutano wake mkuu wa kumteua mgombea wa urais badala ya kujadili mambo ya maana wanaugeuza ukumbi kuwa uwanja wa kucheza madogoli?
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ulinzi wa mali na usalama wa raia ni jukumu kuu la serikali iliyomadarakani. Sasa kama raia wanaibiwa mali zao na pia kuuliwa tumlaumu nani? Serikali ya ccm imeshindwa kuwalinda raia wke na mali zao ndio maana watu kila leo wanaporwa na hata kupoteza maisha a' la professor Mwaikusa aliyeuawa hivi karibuni. Polisi hawalipwi vizuru as such wanajitengenezea utaratibu wao wa kuongeza kipato kwa kufanya uhalifu wakishirikiana na raia ambao pia wamekata tamaa ya maisha kwani hawana ajira!! Huu ujambazi ni salaam wanazopewa wananchi kuwa serikali yenu haifai iondoeni madarakani!
   
Loading...