ShockStopper
Senior Member
- Apr 10, 2009
- 124
- 56
Kuna habari ya kushtua nimeipata karibuni.
Inadaiwa kwamba vijana wa kitengo cha IT kinachosimamia Tigopesa wamekuwa wakiwaibia wateja wanaotumia huduma hiyo kwa kupunguza salio kidogo kidogo toka akaunti za wateja wasioweza kustukia huo mchezo mchafu.
Katika tukio moja, inadaiwa mzee mmoja aligundua hela kiasi cha sh 30,000/= haionekani kwenye account, na baada ya kazi ngumu sana ya kufuatilia, inadaiwa kijana mmoja wa kitengo hicho alikiri kwamba alijikuta hana hela ya kutumia weekend ndipo akaamua kuchota salio la mzee huyo.
Habari zaidi zinadai kuwa ma boss wa kampuni hiyo hawazingatii kigezo cha UAMINIFU katika kutoa ajira, kitu ambacho muhimu sana kwa taasisi za fedha.
Kibaya zaidi, inadaiwa kuwa mteja anapotoa malalamiko ma boss hawachukui hatua za kutosha zaidi za kumwambia 'kachukue RB'.\
Binafsi, mimi ni mtuamiaji mkubwa wa huduma hii na baada kupata taarifa hizi nilikimbilia haraka ku check statement. Lakini niligundua kuwa hiyo taarifa yao fupi ina entries chache mno na haijulikani mteja anawezaje kupata statement kamili ya kipindi anachotaka.
Natoa wito wana JF tulifanyie kazi hili ili kama kuna ukweli tujue hatua za kuchukua. Na iwapo hakuna ukweli, mamlaka zinazohusika zitutoe hofu.