Wizi wa vifaa vya magari University of Dar es Salaam-Mlimani campus | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi wa vifaa vya magari University of Dar es Salaam-Mlimani campus

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by everybody, Mar 28, 2012.

 1. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu nimeona nilete hii taarifa kwanza kupata maoni ya nini kifanyike na pia kuwapa tahadhari wale wanaopaki UDSM -Mlimani campus.
  Kumezuka uwizi wa kutisha wa vifaa vya magari kwa wale wanaotumia parking za UDSM. Kwa kweli hali ni ya kutisha kwani ndani ya siku moja unaweza kwenda kituo cha polisi mlimani ukakutana na watu zaidi ya watano wanaripoti kuibiwa vifaa vya magari. Ninachojiuliza ni kwamba hili linawezekanaje wakati mageti yote ya chuo yana ulinzi na huwaga wanasimamisha magari ya kuyakagua.
  Hii inamaanisha kwamba ukaguzi haufanyiki inavyotakiwa, vinginevyo hao askari wa magetini wangekua wanakama hivyo vifaa vinavyoibiwa. Mara nyingi sana nimekua nikiingia na kutoka University of Dar es Salaam bila kuambiwa nifungue boot ya gari na mara nyingine get linakua wazi watu tunapita tu bila kusimamishwa kwa ukaguzi. Kuna weakness hapa na uongozi wa chuo inabidi waingilie kati. Vinginevyo tunaweza kusema kwamba hawa askari getini wanashirikiana na hao wezi.
  Inabidi kutambua kwamba njia za UDSM Mlimani campus siku hizi zinatumika kama short-cut kwa wale wanaoishi Kimara, Mbezi ya shamba na kwingineko ili kufika mjini mapema na kuepuka foleni ya Ubungo. Sasa lazima kufahamu kua katika msafara wa mamba, kenge nao wamo. Hivyo UDSM sasa iamke na kusisitiza uimarishaji wa ulinzi kwenye mageti. Ni bora watu kuchelewesha wakiwa wanakaguliwa kulikowa kuishi bila amani ndani ya campus. Siku hizi ukipaki gari inabidi kila baada ya dakika mbili ukachungulie. Tutaishije hivi. Hii inakera.
  Tuibiwa Sinza, Manzese na Kariakoo ambako hakuna mageti na bado tuibiwe ndani ya campus ya Mlimani ambako kuna mageti na walinzi. Inakera na hapa ipo namna.

  Nawapa tahadhari wale wanaotumia parking za Mlimani campus kua makini. Hali sio salama tena.
   
 2. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 997
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 60
  Mimi nadhani kila sehemu kwa Dar sio salama kwa kupaki gari hovyo bila ulinzi binafsi kama alarm n.k
   
 3. c

  collezione JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mkuu polisi wenyewe siku hizi ni majambazi. Viongozi wetu wenyewe wanalea majambazi. So usitegemee wizi au uhalifu kupungua Tanzania.

  Hukusikia malima anasema "silaha zake ni mtaji mkubwa"

  Haha, Dunia yako ndo chagua lako. Na CCM ndo serikali yakooo...
   
 4. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,609
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Mkuu..
   
 5. c

  collezione JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mimi nimekaa India, Malaysia, Singapore, China,... Unaweza ukawa sokoni na bahati mbaya umesahau milango ya gari lako.. Nenda urudi, Hakuna mtu anayegusa..

  Tanzania hata kama umepaki pembeni ya ikulu, ukirudi vitasa vya gari hakuna ..

  Na ukienda polisi. Wanakuomba hela wakurudishie vitu vyako..haha
  Hii ndo tanzania.
   
 6. P

  Peter Nyanje Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama wale askari wanaokaa kwenye mageti wanaweza kusaidia maana kuna njia nyingi za miguu kutoka katika eneo hilo. lakini pia anayeiba si lazima atoke navyo wakati huohuo, vinaweza kwua nivahifadhiwa hapahapa Mlimani na kuuzwa baadaye sana
   
 7. c

  collezione JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ndo hivyo kaka, Tanzania inabidi tuishi kama digidigi.... Ukigeuka nyuma tu, watu wameshakuibia...Hahaha
   
 8. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  USDM iko ndani ya Tz na inaelekea Tanzania sasa tumealibikiwa! Mungu tu ndiye atatunusuru maana hizi tabia zingine za udokozi zinafanyika kwa watu ambao wapo on the lowest class of humanity, mtu asiyeona tabu kukuua ili achukue viatu ulivyovaa tu
   
 9. m

  mgebuka Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka pole sana,nahis watakua wamekuibia leo leo hapo udsm,kuna vifaa vya kichina(alarm system),unafunga.Katika keyholder yako unakua unaweza kuona milango yote mitano au mitatu ya gari yako,ukiguswa/kufunguliwa hata mmoja unapata alarm pale kwenye key holder wakat gar iko parking.
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Parking iliyo salama ni ile ya CoET na Admin lkn nyingine chaka!
   
 11. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,111
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Na airport term 2 na 1 veeeeeeeeeeerrrrrrrrriiiiii veeeeriiiiiiiiiiiii safe
  loh
   
 12. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,111
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Wanawaibia nyie mangwini wanawaona mazuzu wajaribu kule chini waone
  thosedays sio akiiba tukihisi mtu ni mwizi kichapo chake anamkumbuka marehemu hawara yake
  watawachezea kweli huko juu lakini sio coet...
   
 13. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,170
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  nikipaki gari dar airport na nikiwa arusha town........Kifaa kitafanya kazi? Ni swali tu
   
 14. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Kama mawaziri makatibu,wakurugenzi,wabunge,mameneja na mkuu wao wezi.
  Unategemea nini?
  Kila mtu anakula kufuatana na urefu wa kamba yake.
   
 15. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2017
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 4,585
  Likes Received: 2,691
  Trophy Points: 280
  Hali imebana wakuu, serikali itafute mbadala ya vijana wasio na kazi, kuwakamua kodi kila kukicha ndo madhara yake haya
   
Loading...