Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi Wa Parcels: Posta, EMS na Swissport unachefua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Indume Yene, May 17, 2008.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,916
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Shirika la Posta Tanzania pamoja EMS kwa kweli mnachefua kwa jinsi mnavyofanya kazi zenu. Wizi umekubuhu katika mashirika haya. Cha kushangaza Posta pamoja na EMS mmeshindwa kabisa kufanya kazi zenu kwa uaminifu. Hainiingii kichwani mnadirikia hata kuiba Birthday Card. Kama ni suala la usalama, angalieni kilichomo kisha mrudishe na kuhakikisha barua au kadi inafika kwa MLENGWA.

  Hivi karibuni nilimtumia Mzazi wangu documents za kwenda nazo Embassy kwa ajili ya kuchukuwa Viza aweze kupata matibabu zaidi, cha kushanganza Tracking number inaonyesha EMS mmepokea tangu tarehe 21/04/08 na leo is almost a month hizo dox bado hamja-deliver pamoja na kwamba niliweka namba ya simu to call before Delivery.
  That's the same way I've using to send dox and other things kwa kutumia makampuni mengine, sasa inakuwaje nyie mnashindwa kufanya hivyo??

  Ukitumia SLP mkiona barua imenonanona mnafungua kuangalia kama kuna cash, mpate msipate still mnaitupa. Nani katika dunia ya leo atatuma cash kwa P.O. BOX wakati kuna Western Union, Moneygram, PayPal n.k?

  Jaribuni kwenda na wakati, hapa ninakuwa na wasiwasi maana sijui huyo aliyechukuwa hizo dox atatumiaje IDs zangu. Kulikuwa na vitu muhimu ambavyo vinahusu my Privacy like Soc. Sec #, Cert. ya uraia, Driv. Lic, Pay stb na vinginevyo. Mtashindwa kufanya biashara kwa kukosa clients kutokana na njaa. Mzazi wangu anazidi kuumia kwa sababu ya negligency na upuuzi wenu.

  Nendeni na wakati katika biashara na kama hamuwezi basi fungeni hilo/hayo mashirika.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,569
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mbona Unazungumza Na Marehemu? Hili Shirika Kwa Kweli Liko Icu Huna Habari? Limekwisha Kufa Siku Nyingi. Kwanza Siku Hizi Baru Nyingi Zinakuja Kwa Email Nani Anawatumia Tena? Pole Maana Hukujua. Wengi Hatuwatumii Tena. Tunatumia Courriers Wengine!@!
   
 3. P

  PanguPakavu Amy Senior Member

  #3
  May 18, 2008
  Joined: Jul 7, 2007
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  njaa mbaya!!these guys are crooks.its true and very sad.they steal anything without consent.as if they are there to collect customer stuffs.instead of dispatching them.

  they have stolen my parcel before.i no longer use their service.better go with private companies.

  anyway,pole sana ndugu.
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,089
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hii ni aibu tena kubwa sana

  unajua wengi wetu tunapotaka kutuma mizigo nyumbani ikifika kutumia njia ya posta hujiuliza mara mbili mbili.


  na si huko hata bandarini mambo yako hivyo hivyo mtu atafungua basi hata vifulana pia mwaiba ? aah aibu wajameni kama wakuu wa haya mashirika mnapita jaribuni kuwapanga tena hawa watendaji wenu na wanaotia aibu waadhibiwe bila ya kuwatazama usoni
   
 5. m

  mjinga JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 329
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mmh, pole ndugu yangu. mie baada ya kulizwa mda mrefu sasa natumia makampuni binafsi kwa mfano DHL,
   
 6. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,044
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Sikutaka kusema hapo mwanzoni kwa kudhani labda ni mimi pekeyangu tu ndo niliyetiwa mchanga wa macho, kumbe tuko wengi. Nina mizigo yangu miwili huu ni mwezi wa nne sasa haijafika.....hata kama ningetumia jahazi ingekuwa ishafika; Sehemu iliyotokea wamenithibitishia kwa kunionyesha kwenye tarakilishi kuwa mzigo ulishaondoka na uko mikononi mwa Posta, wale waheshimiwa wanasema haujafika...basi ufanyeje tena; ndo mambo ya mitaa ya Gerezani kariakoo zamani 'au sijui bado yapo' unavuliwa viatu, ukipiga kelele, wanakupiga mkwala uondoke...Mmh!
   
 7. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,916
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145

  Nilitumia USPS na huko ilipaswa kuwa delivered by EMS lakini wameiminya utafikiri watafaidi chochote.
   
 8. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,916
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nashukuru kwa kujali.
   
 9. I

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Njaa mzeee!!!!!! kijimshahara kiduchu, basi wakiona tu kijibahasha kimetuna basi kina kazi.
   
 10. M

  Msengi Kiula Member

  #10
  May 18, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 81
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Yaani waibe hata picha ya mtoto mdogo inayokwenda kwa Bibi yake!Jamaa wamekwisha.
   
 11. I

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Msengi Kiula,

  Njaa kitu kibaya sana, waisrael siku zile njaa ilipowagwata walilalama, wakalia, hata kutaka kumtukana mola, sasa iweje hawa wa posta mshahara unalipwa 80,000? toa basi nauli hapo, vipi kuhusu chakula , watoto hawajaugua!!!! real it is very bad but alitle wage it can create some problem,kwa mantiki hiyo shirika liboreshe vipato vya wafanyakazi.
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,983
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  hahaha ukata mkuu unajua tena kule hakuna dili za kifisadi kwa wafanyazi wa chini wanafaidi wajuu tu mamanager kwa hiyo wadogo inawalazimu waponee humo humo kwenye vibarua si unajua mshahara wenyewe kima cha mbuzi huu.
   
 13. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu wao anachota zake mapema nao wameamua kujichotea kila wanapopata mwanya.
  Ila kwa kweli watu wa EMS kila kitu kizuri kitoke Ulaya? Hata uaminifu utoke Ulaya. Bora muache kazi kuliko kuwaibia wateja wenu unaiba dox ambazo ni muhimu kwa mhusika, mlaaniwe kabisa.
   
 14. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2008
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 490
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mhh pole mwenzangu wewe. Mi nafikiri huenda nilibahatisha. Nilituma mizigo yangu minne @10 kgs nikiwa Sweden. Niliituma wiki moja kabla sijaondoka huko.Baada ya kufika dar, ndani ya wiki moja nikawa nimeitwa Posta kuchukua mizigo yangu.Nikiwa na hofu kama hiyo ya kuibiwa, niliikagua hapohapo kabla sijaondoka na yote ilikuwa salama. Huenda nilibahatisha au labda wesha anza jipanga uzuri kuzuia wizi kama huo, au labda vijibahasha vya 1-2kg ndio vinavyoshughulikiwa na hivyo vifisadi vidogovidogo. Mungu wasamehe maana hawajui walitendalo.
   
 15. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,479
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  USPS halafu delivery by EMS, inakuwaje hapo?
  Nani mwenye experience ya delivery and reliability ya UPS, DHL, FedEx...?
   
 16. T

  Thuraya Member

  #16
  Aug 22, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  EMS ni marehemu.Nilituma barua kwenda Bodi ya mikopo elimu ya juu.It took 3 weeks!
   
 17. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Sio EMS peke yake wakuu. Kuna watu wengine wapo pale uwanja wa ndege wanaitwa Swissport. Hawa jamaa ndio hupokea mizigo inayoingia kupitia ndege hapa nchini. Basi kuna kamchezo kanachochezeka hapo kuweni makini.

  Hawa jamaa huwa wanaangalia packaging ya mzigo. Kama umetuma package ambayo inaonekana kama ni simu uwezekano mkubwa ni kwamba utaambulia hewa. Wafanyakazi wa pale swissport huficha vi-parcel vidogo vidogo.

  Hapa jirani yangu alituma Blackberry totak US kupitia FedEx kuja huku bongo. Packaging yake ilikua inaonekana kama simu... maana ilikua inaonyesha kuwa ndani kuna kutu kigogo.. basi kwa njaa zetu wabongo simu ikaenda kusiko julikana.

  Kuna utata, watu wa swissport wanadai mzigo utakua ulibaki kwenye ndege, lakini FedEx wenyewe wanadai ulishatumwa.. so ni kuzungushana sasa.

  Kuna jamaa huwa wanaagiza vitu toka Japan kama Camera n.k, ikabidi niende nimuulize inakuaje mambo kama haya ya wizi. Then akanidokeza huo mchezo. Akasema wao huwa wana pack mizigo yao kwenye box kubwa, hata kama ni kitu kidogo sababu anafaham washkaji wa pale swissport ni wezi sana wa vitu vidogo vidogo, hasa hasa simu.

  Haya ndio mambo yetu tanzania. Mimi nilikua niagize camera toka nje, nikasita. Next time hata mimi nikiagiza kitu, hata kama ni simu I hope ntamuomba sender atumie box la TV... lol!
   
 18. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,033
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 133
  Tabia ya staff wa EMS na POSTA ni ya kishirikina, hata wanavyoonekana wako ki-sangoma sangoma tu, afadhali ya POSTAL BANK wanaonekana ni binadamu.
   
 19. The Spit

  The Spit JF-Expert Member

  #19
  Aug 22, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 374
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Nilitumiwa Crdb Visa CARD Kwa EMS toka bongo,mpaka leo sijaiona.
  Hata Tracking # waliyonipa haina record yoyote katika system zao,
  It's very sad....it's criminals we are dealing with here!
   
 20. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,479
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Yaani hata ukitumia FedEx bado hakuna uhakika kwamba mzigo utafika salama? This is terrible. Itabidi nisubiri mzigo uletwe na mtu atakayesafiri kuja bongo.

  Ikiwa kuna mizigo inaibwa na hakuna anayewajibishwa, je, makusanyo ya kodi yanafuatiliwa kweli? Aibu!
   
Loading...