Wizi wa muda wa maongezi, sms na bando za internet unaofanyika pasipo watu kujua

Fursa Pesa

JF-Expert Member
May 30, 2012
4,430
3,250
Kwa niaba ya watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini napenda kuwaomba wamiliki/management ya makampuni ya simu/mawasiliano kuondoa ukomo wa muda katika huduma zao (sms,calls na internet bando).

Kutumia kigezo cha muda ni kuingilia uhuru wa mtumiaji huduma kwa kumlazima atumie kwa muda mliompatia ilihali kifurushi alichonunua amekilipia kodi, lakini pia ni utashi wake kutumia kwa budget aliyoweka.

Huduma za mawasiliano ni sawasawa na huduma nyingine,hivyo malipo yawe kadri unavyotumia.

Tunaiomba TCRA na vyombo vingine vinavyotetea walaji wa huduma za mawasiliano waangalie namna gani watumiaji wa huduma wanafaidika na malipo wanayotoa kwani sio haki kupangiwa muda kutumia muda wa maongezi, jumbe za sauti na vifurushi vya internet.
 
Kuna jamaa alinunua bando 1Gb lakini sm ilikua inasoma h+ yenye mshangao yaan data za internet ila hazifungui akaamua kutupa lain tu
 
Kuna bundle linaitwa"HALICHACHI" mkuu ni vyema ungeunga bundle hilo au uweke vocha pasipo kujiunga nadhani ungetumia mpaka pale vocha yako itakapoisha
 
Back
Top Bottom