Wizi wa mizigo uliokithiri Dar airport, Viongozi wa Swissport wanastahili kulaumiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi wa mizigo uliokithiri Dar airport, Viongozi wa Swissport wanastahili kulaumiwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ujengelele, Dec 28, 2009.

 1. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umekua ukisikia mara kwa mara vituko vya uwanja wa ndege wa JKN kuanzia kuibiwa , kusachiwa kwa baadhi ya abiria , kulaghaiwa na aina nyingine nyiingi sana za uharamu ndani ya uwanja huo kutokana na ukuaji wa tekinologia hata hawa wezi na matepeli nao wanapandisha viwango hata aina nyingine za uharamia wao .

  Kwanza ni kwenye sehemu za kupitisha mizigo inayotoka na kuingia nchini sehemu hiyo imejaa watu mbalimbali wanaohusika na usalama wa uwanja na watu wanaotumia uwanja ule watu hawa kushirikiana na maduka ndani ya uwanja huo ya kuuza vitu ambao ni wadau wakubwa wa wizi unaoendelea ndani ya uwanja .

  Kama umewahi kuibiwa kitu kama laptop hatua ya kwanza ni kutoa taarifa hapo uwanjani mara nyingi watasema vitu vyako vimeibiwa Nairobi au Kilimanjaro na Ethiopia ukweli ni kwamba vitu hivyo huibiwa na watu wa (majina kapuni kwa sababu maalum za maadili), sehemu za kwanza kuuzwa au kuhifadhiwa ni Duka namba nanihii ambao kuna Huduma za Internet. Duka hilo hujaa mali zilizoibwa ndani kwa kujidai Used Vimetoka Ulaya na Bara Asia .

  Duka hilo hilo kama una haraka na kupanda ndege watakuuzia hata Vocha za simu ambazo zimeshatumika na ukiondoka umeliwa

  Saa zingine Abiria anaweza kua amefanya kosa badala ya askari kumchukulia hatua anaweza kulazimishwa kuachia Laptop yake au Kamera ili mradi ni kifaa kinachouzika haraka ndio maana ndani ya maduka hayo vifaa vile havina charge , battery na vifaa vingine vya kuviwezesha kufanya kazi kwa uhakika .

  Ukizunguka upande wa Pili kuna duka la kuuza vyakula kuna mtanzania mwenye Asili ya ki-Asia ukizungumza nae kwa upole na vizuri anaweza kukuuzia laptop hata kamera ambazo husahauliwa au huibwa katika mgahawa anaousimamia uwanjani hapo kwa jina la (kapuni) .

  Ukienda mbele kidogo Kuna duka la ziada Nalo la vitu vidogo vidogokuna kijana mwenye asili ya visiwani kazi yake kubwa ni kununua simu zilizoibwa uwanjani hapo ni mtaalamu wa kubadilisha hizo simu ziweze kutumika Tanzania .

  Ndani ya duka iloilo wauzaji wa Tiketi bandia za kusafiria wapo na ukitaka ni bwerere haswa za mashirika yetu ya ndani kama Air
  Tanzania , PrecisionAir na ZanAir .


  Ukikaa uwanjani usishangae kuona askari polisi anatoka kwenda kwenye gari ya msafiri mara nyingi ni kwenda kupeana cha juu.

  Kwa hisani ya Michuzi Blog
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ama kweli nchi yetu imeoza!! Inaumiza sana.
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2010
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  duh!

  wengine watabisha hakuna wizi!!!
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,472
  Trophy Points: 280
  hii sasa kali ngoja tuendelee kuwaanika.
   
 5. K

  KIBE JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitu kinanikera na kuiabisha taifa kama wizi unaoendelea siku hadi siku katika uwanja wa ndege wa kimataifa jk.nyerere dar es salaam... Hii ni mara ya pili sasa naibiwa vitu katika begi langu...
  Hili ni tatizo kubwa tena kubwa sana na ni hatari kwa heshima ya nchi yetu..sasa sijui viongozi wa swissport wameshindwa wachukulia hatua hawa watumishi wanaopakua mizigo toka kwenye ndege .
   
 6. T

  Tayseer JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kama baba ni mwizi au mama je wategemea watoto watakuwa waumini wa imani gani?

  so nchi hii inaongozwa na majizi makuu(mapapa) hivyo usitarajie kama tunaweza kuwa na wafanyakazi waadilifi huko pengine ndio hali halisi
   
 7. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Usiseme dar maana hata kia pia mchezo ni huo huo
   
 8. D

  DARKMAN Senior Member

  #8
  Dec 11, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi nilitokea china nilifunga begi langu na kufuli nikakuta wametoboa begi ila kitu walichokuwa wanataka kukichukua walishindwa maana nilikuwa nimevifunga kwa kuviunganisha vyote kwa hiyo ukitaka kukichukua kimoja inabidi uvitoe vyote
   
 9. Varbo

  Varbo JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kesho ninasafari ya Kuja bongo najawa na wasiwasi hawa washenzi watanichukulia zawadi za ndugu zangu!! Na ikitokea pale airport nitageuka kichaa!!
   
 10. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Kila mtu ni mwizi bongo tofauti ni kila mtu anakula urefu wa kamba yake.

  Kama kuna mtu masafi hapa aseme!
   
Loading...