Wizi wa mitihani

Mtz.mzalendo

JF-Expert Member
Jul 22, 2012
357
49
Hivi hii imekaaje wadau? Yaani shule mwaka uliopita zimeingia kwenye top.10 ila mwaka huu upo kwenye kumi mbovu...ikiwa walimu na miundo mbinu yote ni ileile...nazungumzia st.mary na green acers
 
Hao wezi wa mitihani miaka yote!hiyo green acres ilikua na bifu na necta tangu matokeo yaliyopita form 4
 
Hivi hii imekaaje
wadau? Yaani shule mwaka uliopita zimeingia kwenye top.10 ila mwaka huu
upo kwenye kumi mbovu...ikiwa walimu na miundo mbinu yote ni
ileile...nazungumzia st.mary na green acers

walimu ni walewale,
miundo mbinu ni ile ile,
shule ni ile ile,
vitabu ni vile vile,
SWALI.
Wanafunzi waliofanya mtihani mwaka juzi na waliofanya mwaka jana ni walewale?
Thea4,wala hakuna tatizo lolote hapo.
 
Tatizo lipo,ingekuwa kutoka ni kwenye top.20 tu,isingukuwa tatizo..lakini kumi mbaya?sio kawaida.. Hapa kuna kitu nyuma ya pazia
 
Kila kitu ni kilekile ila wanafunzi ndo wamebadilika.Huoni ni sababu tosha ya kupata matokeo hayo?
Unaonekana huna ufahamu na maswala ya kielimu zaidi ya ushanta na umbea kwenye taaluma ziziso kuhusu.
Kufaulu ni uwezo binafsi wa mwanafunzi na kujituma,Hivyo kama wanafunzi mwaka huu hawakutia nguvu kwa kufikiri wako kwenye shule inayofaulisha watakuwa wamejifelisha wenyewe na si suala la uwizi wa mitihani/jina la shule.
 
walimu ni walewale,
miundo mbinu ni ile ile,
shule ni ile ile,
vitabu ni vile vile,
swali.
Wanafunzi waliofanya mtihani mwaka juzi na waliofanya mwaka jana ni walewale?
Thea4,wala hakuna tatizo lolote hapo.

na bado marian shule wanazosoma watoto wa walioko juu
 
Tatizo lipo,ingekuwa kutoka ni kwenye top.20 tu,isingukuwa tatizo..lakini kumi mbaya?sio kawaida.. Hapa kuna kitu nyuma ya pazia

Acha kutuletea umbea hapa kama kuna kitu nyuma ya pazia si ulifungue basi hilo pazia ili kionekane? Hili ni jukwaa la great thinkers kama hujui unachoongelea usituletee thread za aina hii hapa.
 
Ni kweli kufaulu kwa mtu kunategemea zaidi uwezo wa mtu binafsi jinsi atakavyojituma,lakini mazingira ya shule na miundombinu kwa ujumla inamchango mkubwa pia,na ndio maana shule za kata zinafanya vibaya sababu miundombinu mibovu...hiki kinachonishangaza mimi
 
:llama:Inasikitisha kuona kwamba mleta mada hana kumbukumbu sahihi! Mwaka uliopita St. Mary's na Green Acres zilikuwa nafasi ya ngapi? Au metumwa ili kupoteza muda wa watu? Shule hizi ziliwahi kuvuma enzi walizokuwa wananunua Mitihani, na tangu mwaka 2008 hawajawahi kuwemo hata kwenye 40 bora. Kichaa wangu!
 
Hivi hii imekaaje wadau? Yaani shule mwaka uliopita zimeingia kwenye top.10 ila mwaka huu upo kwenye kumi mbovu...ikiwa walimu na miundo mbinu yote ni ileile...nazungumzia st.mary na green acers

Kwi kwi kwiii! Labda kwa kuwa wanafunzi wa mwaka jana ni tofauti na wa mwaka huu!
 
Sio kweli kuwa kufaulu ni juhudi ya mwanafunzi peke yake. Kama wewe ni mwalimu lakini hauko peke yako humu JF na Tanzania. Kufaulu kwa mwanafunzi mmoja mmoja yawezekana kuwa juhudi binafsi lakini collectively kama shule kunategemea mambo mengi kama vile: Mazingira ya shule, ubora darasa yaani chumba maktaba, waalimu zana za kufundishia, maabara yenye vitendanishi morali wa walimu orodha ni ndefu na niliyoyataja ni baadhi tu. Matokeo mazuri huanza kuonekana polepole kwa kupanda polepole hadi kufikia kwenye kilele. Matokeo mazuri ya kidato cha Nne kwa mfano ni matokeo ya maandalizi mazuri kuanzia kidato cha kwanza. Usajili mbaya au ufundishaji mbaya huanza kuonekana baada ya miaka minne na kuendelea kushuka polepole pia. Hii ni kanuni ya maendeleo ya kitaaluma katika shule.Suala la kushuka ghafla kutoka 10 bora hadi 10 dhaifu sio kawaida na ndiyo maana inatoa nafasi ya watu kujiuliza kuna nini. Jibu la swali hili haliwezikupatikana kwa hoja za kijiweni inahitaji vichachawizo kulijibu.
Kila kitu ni kilekile ila wanafunzi ndo wamebadilika.Huoni ni sababu tosha ya kupata matokeo hayo?
Unaonekana huna ufahamu na maswala ya kielimu zaidi ya ushanta na umbea kwenye taaluma ziziso kuhusu.
Kufaulu ni uwezo binafsi wa mwanafunzi na kujituma,Hivyo kama wanafunzi mwaka huu hawakutia nguvu kwa kufikiri wako kwenye shule inayofaulisha watakuwa wamejifelisha wenyewe na si suala la uwizi wa mitihani/jina la shule.
 
Umeona mkuu,kama wangekuwa wafuatiliaji wazuri wa vyombo vya habari wangeona jinsi walivyoripoti hii inshu
 
Back
Top Bottom