Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,923
Hii ndiyo habari yenyewe kutoka katika gazeti la Mwananchi:
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha amehoji kwa nini aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP), Abdallah Zombe hakutoa mapema taarifa za uhalifu zinazomhusisha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
"Huyu kwanza sasa hivi si mwajiriwa wetu, angekuwa bado ni mwajiriwa wetu kwanza mimi ningemwuliza alikuwa wapi muda wote huo kutoa taarifa hizo na kwa nini amezitoa sasa," alisema na kuongeza;
"Ndiyo ningemwuliza ni Waziri gani aliyekuwa amemsimamia nyuma yake akamzuia kuzisema na sasa hayupo ndiyo maana ameamua kuzisema?"
Alikuwa akijibu swali kuhusu hatua ambazo jeshi hilo limezichukua dhidi ya Lema kuhusiana na tuhuma hizo ofisini kwake, Dar es Salaam jana alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru na changamoto zinazoikabili. Hata hivyo, alilitaka jeshi hilo kutokuzipuuza taarifa hizo.
Aliwaagiza maofisa wa jeshi hilo kupitia kwa Kamishna wa Polisi Utawala na Fedha, Clodwig Mtweve kumuita Zombe na kumwuliza juu ya tuhuma hizo na kuzifanyia kazi.
"Sisi tunasema kwa kila taarifa inayotolewa inakuwa na chembe ya ukweli. Labda niwape mfano mmoja, nitatumia mfano mbaya kidogo... ukikutana na mlevi akakwambia kuwa katika njia hii kuna majambazi japo ni mlevi lazima utakimbia kupitia njia nyingine;
Kwa hiyo hata hizi taarifa za Zombe hatupaswi kuzipuuzia kwani hawezi mtu mzima kusimama na kutoa taarifa kama zile hadharani hivihivi tu. Kwa hiyo maofisa wa jeshi nendeni mkae naye muulize maana inaonekana ana taarifa nyingi."
Agosti Mosi mwaka huu, Zombe alimhumu Lema kuwa alikuwa na mtandao wa uhalifu wa wizi wa magari akidai kwamba anao ushahidi wa tuhuma hizo kwa kuwa alipokea taarifa hizo wakati akiwa RCO Dar es Salaam ambazo alidai kuwa alikuwa ameshaanza kuzifanyia kazi kabla ya kukamatwa na kuwekwa ndani kwa tuhuma za mauaji.
Mauaji ya wafanyabiashara wa Mahenge
Aidha, Nahodha ameahidi kufuatilia sababu za jeshi hilo kushindwa kuwakamata askari wawili waliotajwa kuhusika katika mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva teksi wa Manzese, Dar es Salaam.
Waziri Nahodha aliahidi kukaa na maofisa wa jeshi hilo kuona ni kwa nini askari hao hawajakamatwa na kuangalia hatua za kuchukua kuhakikisha kuwa wanapatikana.
Mbali na kuangalia namna ya kuwasaka pia aliahidi kufuatilia kuona kama askari hao walishafutwa kazi au wanatambulika na kama wanaendelea kulipwa mshahara na ambaye anauchukua.
Alitoa ahadi hiyo baada ya kutajiwa majina ya askari hao ambao ni pamoja na Koplo, Saad Alawi aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha Oysterbay ambaye ndiye alitajwa kuwaua wafanyabiashara hao kwa kuwapiga risasi, pamoja na Koplo, James Frank ambao hadi sasa haijulikani waliko.
Awali Waziri Nahodha alionyesha kutokuwa na taarifa rasmi juu ya kesi hiyo ya Zombe na askari hao waliotoroka, pamoja na uamuzi wa Mahakama Kuu, lakini baada ya kufafanuliwa na waandishi kuwa askari hao wanafahamika alionekana kushangaa kidogo na kutoa ahadi hiyo.
"Kama walikuwa ni waajiriwa wa jeshi la polisi mimi sioni linaloshindikana, maana kama hao 13 walikamatwa kwa nini hawa wawili, mimi nadhani hili halishindikani, nitaakaa na maafisa wa jeshi kuona namna ya kulifanyika kazi."
Mafanikio ya Wizara hiyo
Kuhusu mafanikio ya wizara hiyo alisema pamoja na mambo mengine, imewaingiza askari wote katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuwawezesha kupata huduma za afya za uhakika wao na familia zao kwa lengo la kuwaongezea ari.
Pia alisema jeshi limejenga nyumba za ghorofa 30 jijini Dar es Salaam eneo la Kurasini, Barabara ya Kilwa kwa ajili ya familia 120 na nyingine katika Mikoa ya Mara, Mwanza, Iringa na Kaskazini Pemba.
"Ili kuwajengea wafungwa uwezo wa kujitegemea Jeshi la Magereza linawapatia wafungwa mafunzo ya ushonaji wa nguo, utengenezaji wa sabuni, uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mkonge na utengenezaji wa chumvi, samani na kilimo."
Katika jitihada za kutumia nishati mbadala, Jeshi la Magereza limeanzisha matumizi ya makaa ya mawe katika Magereza ya Ruanda, Tukuyu na Songwe mkoani Mbeya. Utumiaji wa biogas umeanza katika Chuo cha Maofisa Magereza Ukonga.
Kuhusu kuimarisha uoto wa asili ulioko kwenye maeneo ya Magereza, miti 3,701,594 imepandwa katika eneo la ekari 6,136 katika Magereza ya Malya, Bariadi, Isupilo, Msalato na Idete kwa lengo la kuhifadhi mazingira.
Waziri Nahodha aliongeza kuwa jeshi hilo limeanzisha programu ya maboresho wa miaka 10 kwa lengo la kuwajengea uwezo askari na weledi, mazingira bora ya kazi.
Licha ya mafanikio mengine kama kupambana na kupunguza uhalifu kama ujambazi wizi na wahamiaji haramu, alisema bado wizara yake inakabiliwa na changamioto nyingi ambazo alizitaja kuwa ni pamoja na ujambazi kwa baadhi ya maeneo ajali za barabarani, wahamiaji haramu na msongamano katika Magereza.
Alisisitiza kuwa licha ya changamoto hizo wizara yake imeweka mikakati ya kuendelea kulinda amani na usalama wa raia kwa kuwa bila amani maendeleo hayawezi kupatikana.
Akizungumza kuhusu mradi wa vitambulisho vya taifa alieleza kushangazwa na mbunge aliyehoji kutengewa Sh300bilioni akisema kuwa mradi huo una faida kubwa katika suala zima la ulinzi na usalama kwa kuwa utawezesha kuwatambua Watanzania na wageni wanaoingia nchini kwa nia mbaya.
Hata hivyo alifafanua kuwa si kwamba fedha hizo zitatolewa kwa wakati mmoja, bali ni katika kipindi cha miaka mitano.
Mazungumzo ya Wizara na Kampuni ya Barrick
Kampuni ya Barick inayomiliki Mgodi wa Madini Nyamongo imekubali kutoa mrabaha wa asilimia moja ya faida yake ya madini yanayouzwa pamoja na Dola za Marekani 100,000 kwa vijiji saba vinavyozunguka mgodi huo kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya wananchi.
Pia kampuni hiyo imekubali kutenga Dola 4.5milioni kwa ajili ya kuwaendeleza wachimbaji wadogo katika mgodi huo ambazo zitatumika kwa ajili ya kununulia vifaa vya kisasa ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa kitaalamu katika shughuli zao.
Kampuni hiyo imekubali kutenga fedha hizo yakiwa ni makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo baina yake na Waziri Nahodha alipofanya ziara katika mgodi huo kutokana na mgogoro ulipo baina ya kampuni hiyo na wananchi.