Wizi wa Magari: Godbless Lema achunguzwa na Polisi

Wadau nimepata wazo naomba mawazo yenu.
Wale wote waliowahi ibiwa Magari huko Arusha miaka ilee mjitokeze hadharani mtupe uzoefu wenu hata kama hamna ushahidi wamoja kwa moja wa Mhusika.
Karibuni.
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha amehoji kwa nini aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP), Abdallah Zombe hakutoa mapema taarifa za uhalifu zinazomhusisha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Alikuwa akijibu swali kuhusu hatua ambazo jeshi hilo limezichukua dhidi ya Lema kuhusiana na tuhuma hizo ofisini kwake, Dar es Salaam jana alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru na changamoto zinazoikabili. Hata hivyo, alilitaka jeshi hilo kutokuzipuuza taarifa hizo.

Aliwaagiza maofisa wa jeshi hilo kupitia kwa Kamishna wa Polisi Utawala na Fedha, Clodwig Mtweve kumuita Zombe na kumwuliza juu ya tuhuma hizo na kuzifanyia kazi.

“Sisi tunasema kwa kila taarifa inayotolewa inakuwa na chembe ya ukweli. Labda niwape mfano mmoja, nitatumia mfano mbaya kidogo... ukikutana na mlevi akakwambia kuwa katika njia hii kuna majambazi japo ni mlevi lazima utakimbia kupitia njia nyingine;
Kwa hiyo hata hizi taarifa za Zombe hatupaswi kuzipuuzia kwani hawezi mtu mzima kusimama na kutoa taarifa kama zile hadharani hivihivi tu. Kwa hiyo maofisa wa jeshi nendeni mkae naye muulize maana inaonekana ana taarifa nyingi.”

Agosti Mosi mwaka huu, Zombe alimhumu Lema kuwa alikuwa na mtandao wa uhalifu wa wizi wa magari akidai kwamba anao ushahidi wa tuhuma hizo kwa kuwa alipokea taarifa hizo wakati akiwa RCO Dar es Salaam ambazo alidai kuwa alikuwa ameshaanza kuzifanyia kazi kabla ya kukamatwa na kuwekwa ndani kwa tuhuma za mauaji.

Source: Gazeti Mwananchi.

My Comment: Muda si mrefu rangi halisi za huyu mbunge zitakuwa hadharani.
Waliopoteza kura zao kumchagua imekula kwao.
Mkuu vipi uchunguzi wako umefikia wapi ?
 
Kwa siasa hizi za sasa sidhani kama angebaki salama na hizi tuhuma. Kidole chochote atakachonyooshewa mpinzani bila uthibitisho wa kimahakama siuhafiki na wala haunisumbui
 
Albadili ni mbaya sana,Mara oooo sisi tunashughulikia taarifa zote hata za mlevi.Mara Mara oooo muulizeni taarifa za kufatiliwa ziliripotiwa kituo gani?Maana sisi hatuwezi kufatilia taarifa za mitandaoni na vyombo vingine,cha msingi ni kutoa taarifa ofisini.Zombie ametoa taarifa ktk kituo gani? Na kwanini amekaa muda wote huo bila kufatilia tukio?Je kwanini hizo taarifa wanataka kufatilia sasa?Je taasisi husika ilikuwa wapi muda wote huo?Kwanini taasisi husika isiwajibishwe kwakutowajibika kufata kanuni husika?Kwanini taasisi husika hufanya mambo katika mlengo wa fikra ya daraja la kwanza? Tuje sasa ktk fikra pevu,oooh kipimo kinagoma.Labda kwa mtoto wa chekechea na mgonjwa wa akili aliye katika hali mbaya.
 
Safi sana jeshi letu kwa kufatilia kila kauli,ehe na ile ya kutishiwa maisha lema na Nasari nayo ipoje?
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha amehoji kwa nini aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP), Abdallah Zombe hakutoa mapema taarifa za uhalifu zinazomhusisha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Alikuwa akijibu swali kuhusu hatua ambazo jeshi hilo limezichukua dhidi ya Lema kuhusiana na tuhuma hizo ofisini kwake, Dar es Salaam jana alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru na changamoto zinazoikabili. Hata hivyo, alilitaka jeshi hilo kutokuzipuuza taarifa hizo.

Aliwaagiza maofisa wa jeshi hilo kupitia kwa Kamishna wa Polisi Utawala na Fedha, Clodwig Mtweve kumuita Zombe na kumwuliza juu ya tuhuma hizo na kuzifanyia kazi.

“Sisi tunasema kwa kila taarifa inayotolewa inakuwa na chembe ya ukweli. Labda niwape mfano mmoja, nitatumia mfano mbaya kidogo... ukikutana na mlevi akakwambia kuwa katika njia hii kuna majambazi japo ni mlevi lazima utakimbia kupitia njia nyingine;
Kwa hiyo hata hizi taarifa za Zombe hatupaswi kuzipuuzia kwani hawezi mtu mzima kusimama na kutoa taarifa kama zile hadharani hivihivi tu. Kwa hiyo maofisa wa jeshi nendeni mkae naye muulize maana inaonekana ana taarifa nyingi.”

Agosti Mosi mwaka huu, Zombe alimhumu Lema kuwa alikuwa na mtandao wa uhalifu wa wizi wa magari akidai kwamba anao ushahidi wa tuhuma hizo kwa kuwa alipokea taarifa hizo wakati akiwa RCO Dar es Salaam ambazo alidai kuwa alikuwa ameshaanza kuzifanyia kazi kabla ya kukamatwa na kuwekwa ndani kwa tuhuma za mauaji.

Source: Gazeti Mwananchi.

My Comment: Muda si mrefu rangi halisi za huyu mbunge zitakuwa hadharani.
Waliopoteza kura zao kumchagua imekula kwao.
Hahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaahahahahahahaahahahahahahahahahahahahaha mnahangaika mpaka huruma, Arusha jimbo halirudi CCM hata mtembee bila nguo... mshachokwa bora mtulie tuuuu Arusha hata jiwe litachaguliwa sio CCM.."PERIOD"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom