Wizi wa kula na Kuanguka kwa mawaziri - Kenya

G.MWAKASEGE

Senior Member
Jun 29, 2007
153
15
Na katika hatua nyingine, baadhi ya wajumbe wa ECK wamejitokeza wakitaka uchunguzi ufanywe na chombo huru kuhusu madai kwamba kura za Kibaki zilizidishwa mno zilipofika ofisi za Makao Makuu ya ECK kulinganisha na zilizokuwa zikitangazwa majimboni.

Maofisa hao wanne wanataka uchunguzi ufanyike kubaini kama baadhi ya maofisa wa chini yao walihusika katika madai hayo ambayo ndiyo ambayo yamekwa yakitajwa na kundi la Raila na chama chake cha Orange Democratic Party (ODM).

Kwa maoni yao, maofisa hao wanasema kuna dalili kuwa kulikuwa na hitilafu kubwa katika hesabu za kura hizo na kwamba kama ni hivyo wahusika sharti wajulikane.

Maofisa hao: Jack Tumwa, D.A. Ndamburi, Samuel arap Ngeny na Jeremiah Matagaro walitoa maoni yao hayo katika mkutano na waandishi wa habari hapa.

Katikati ya malalamiko ya wizi huo wa kura ni ule unaodaiwa ulifanyika katika Jimbo la Molo, inakoelezwa kwamba zilikuwa na tofauti ya kura 20,000 juu ya zile zilizotangazwa jimboni.

Ukiacha masuala hayo ya wizi wa kura, uchaguzi huu uliwabwaga vigogo ambao wamekuwa wakivuma na kutikisa hapa.

Hao ni pamoja na aliyekuwa Makamu wa Rais Moody Awori (80). Wengine ni aliyekuwa Waziri wa Habari, Mutahi Kagwe; Waziri wa Mambo ya Nje, Raphael Tuju na Waziri wa Barabara, Simeon Nyachae.

Lakini pengine, ukiacha Awori, kigogo Nicholas Biwott

Aliyeangushwa katika Jimbo la Keiyo South naye kuanguka kwake ni habari kubwa.

Yeye alikuwa ni rafiki wa karibu na rais mstaafu Daniel arap Moi ambaye sasa ataungana na watoto watatu wa Moi ambao wote wameagushwa katika majimbo yao na kuhitimisha umaarufu wa familia hiyo katika eneo la Mkoa wa Bonde la Ufa.

Mawaziri wengine walioanguka ni pamoja na Musikari Kombo, Newton Kulundu, Kipruto Kirwa, Moses Akaranga, Njenga Karume, David Mwiraria, Mohamud Abdi Mohammed, Morris Dzoro, Suleiman Shakombo, Mutahi Kagwe and Paul Sang.
 
Back
Top Bottom