Wizi wa karafuu:Unafiki wa wazanzibari wachache!

Majoja

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
612
186
Katika kuumbua unafiki unaojijenga kuwa katika Muungano wazanzibari hawanufaiki, methibitika kuwa wao wenyewe wanajihujumu.
Mwakilishi wa CCM,jimbo la Kwamtipura Ndg Hassan Juma, ameliambia Baraza la wawakilishi kuwa karafuu inatoroshwa usiku na mchana kwenda Kenya.
Uchunguzi kutoka huko Shimoni,Kenya unaonyesha kuwa pale karafuu inapatikana kwa wingi sana hata kuliko Zanzibar.
Uchunguzi umeonyesha kuwa toka mwaka 2001 hadi 2009 Kenya imesafirisha karafuu tani 9,510 yenye thamani ya USD16 million.

Kenya HAINA mashamba ya karafuu popote.
Leo Kenya ndio inaongoza kwa kusafirisha karafuu, na imeipita Zanzibar inakolimwa!

Hii ni licha ya ukeli kuwa kuna Polisi kule, Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo na usalama kem kem

Huu ndio unafiki wa wenzetu kulia na umeme wa bure, madini tule wote na bado wenyewe chao chao, chetu sisi chetu sote.
(source:Guardian-Business & Foreign 29th July 2011)
 
Mkuu Majoja, umesikia hatua zilizochukuliwa mwaka huu kudhibiti magendo ya karafuu?
 
Back
Top Bottom