Wizi wa Kampuni za Simu na vinywaji Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi wa Kampuni za Simu na vinywaji Tanzania

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Kiuno14, Feb 26, 2008.

 1. K

  Kiuno14 Member

  #1
  Feb 26, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  napenda kuwakilisha kwa machungu kabisa wizi wa wazi wazi unaofanywa na Kampuni ya simu ya VODACOM...

  Vodacom imekua na dealers wengi Tanzania nzima na katika hao dealers wengi pia wanateua sub-dealers kudeal kwa niaba yao mikoani....

  Vodacom imekua inatangaza sana huduma zake kwatika radio, TVs, Newspapers, etc... kwa kipindi cha December 2007 walikua na Vouchers kibao zainazo-karibia ku-expire mitaani...kama kweli inawajali wateja wake ilishindwa nini kutangaza na kuwaambia wateja wake wawe makini wanunuapo vouchers?????

  Binafsi nimekutwa na mkasa huo na kwa masikitiko nimejikuta napigwa danadana isioeleweka...mara ooh!! vouchers sio za dealer husika i.e. vouchers zinaonyesha ni za shivacom na wewe mteja unadai umenunua Alphatel!!!!

  KWELI HUU NI WIZI WA WAZI WAZI KWA WALALAHOI NA PIA SIO USTAARABU KABISA...LEO HII WANASHEREHEKEA WATEJA MILION 4 LAKIN WAELEWE KUWA KUTOMRIDHISHA MTEJA 1 KWA JAMBO DOGO INAWEZA IKAWAHARIBIA HAYO MAFANIKIO WANAYOJIVUNIA!!!!
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Kiuno14,ndugu yangu mi nakushauri tu kwa nia njema...usianze kwa kulalamika,...weka wazi umefuata na kuwasilisha malalamiko wapi?vodacom wakakujibu nini?maana mimi ni mteja wao sana na nilipatwa na mkasa kama huo nilikuwa na vocha kibao zilizopita muda na nikapeleka pale makao makuu..nikabadilishiwa bila usumbufu wowote..umejaribu kwenda pale ppf tower?kama uko dar nakushauri uende pale kama mikoani wana ofisi zao kila sehemu....ukiona hujafanikiwa ndio hapo sasa uanze kuwashutumu kama unavyofanya.....ushauri wa bure tu kaka yangu.....
   
 3. K

  Kiuno14 Member

  #3
  Feb 26, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru Ndugu yangu kwa ushauri wako mzuri...
  hadi nimefikia hatua ya kulalamika naomba wenzagu muelewe nimejitahidi kila njia lakinin sijfanikiwa...nlianza kufuatilia hii issue kuanzia Midi-December 2007 (mkoani)....hadi leo hii mtu wa Head office (jina nahifadhi) nlipompigia simu akaniambia "ISSUE YAKO IMEAMULIWA HUTAPATA REFUND YOYOTE..."
   
 4. K

  Kiuno14 Member

  #4
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  napenda kuwakilisha kwa machungu kabisa wizi wa wazi wazi unaofanywa na Kampuni ya simu ya VODACOM...
  Vodacom imekua na dealers wengi Tanzania nzima na katika hao dealers wengi pia wanateua sub-dealers kudeal kwa niaba yao mikoani....

  Vodacom imekua inatangaza sana huduma zake kwatika radio, TVs, Newspapers, etc... kwa kipindi cha December 2007 walikua na Vouchers kibao zainazo-karibia ku-expire mitaani...kama kweli inawajali wateja wake ilishindwa nini kutangaza na kuwaambia wateja wake wawe makini wanunuapo vouchers?????

  Binafsi nimekutwa na mkasa huo na kwa masikitiko nimejikuta napigwa danadana isioeleweka...mara ooh!! vouchers sio za dealer husika i.e. vouchers zinaonyesha ni za shivacom na wewe mteja unadai umenunua Alphatel!!!!

  KWELI HUU NI WIZI WA WAZI WAZI KWA WALALAHOI NA PIA SIO USTAARABU KABISA...LEO HII WANASHEREHEKEA WATEJA MILION 4 LAKIN WAELEWE KUWA KUTOMRIDHISHA MTEJA 1 KWA JAMBO DOGO INAWEZA IKAWAHARIBIA HAYO MAFANIKIO WANAYOJIVUNIA!!!!
   
 5. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  nahisi au nadhani umewahi kuituma hii.... au naota...!
   
 6. a.9784

  a.9784 Senior Member

  #6
  Mar 16, 2008
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hoja hii imekwishajadiliwa kitambo,usituletee usanii hapa JF,sisi sio wasanii kwamba tunashughulikia suala moja tu,we have a lot of things to discuss.
   
 7. M

  Mama Lao JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 238
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KAMPUNI ya vinywaji baridi ya Coca Cola imetajwa kuwa miongoni mwa kampuni zisizolipa kodi.

  Kutokana na hali hiyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewasilisha taarifa yake serikalini ili zichukuliwe hatua.

  Taarifa hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Bodi ya TRA, Dk. Marcellina Chijoriga katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, baada ya baadhi ya wabunge kuhoji kuhusu taarifa kuwa baadhi ya kampuni hazilipi kodi.

  Miongoni mwa wabunge hao, akiwamo Mbunge wa Kisarawe, Athuman Janguo (CCM) walitaka ufafanuzi kuhusu tetesi kuwa kampuni zote za simu za mkononi hazitozwi kodi ingawa zina mapato makubwa, jambo ambalo walisema siyo haki.

  Akijibu, Chijoriga alizitaja kampuni kama vile Vodacom na Celtel kuwa zinalipa kiasi. “Wapo wengine ambao hawalipi kabisa,” alisema na kuongeza kuwa atazihifadhi majina kwa sasa.

  Hata hivyo, baadhi ya wabunge, akiwamo Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF) ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, walimtaka ataje kwa kile walichomweleza kuwa analindwa na Kamati hiyo ya Bunge na ndipo akaitaja Kampuni ya Coca Cola kuwa ni miongoni

  Source Habari Leo

  HabariLeo: Gwiji la habari Tanzania | Coca-Cola yadaiwa hailipi kodi

  Hivi kweli tunataka kuendelea? Tuna tatizo mahali!
   
 8. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2008
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kodi zote including VAT? Mbona tunawapa wao watulipie TRA?
   
 9. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huu sasa ujuha huu, mtu halipi kodi lakini eti jina linahifadhiwa, kuna nini hapa, ujinga huu ndio unaopelekea wananchi kuhisi kuna wakubwa wanapata mgao wa "vijisenti" toka kwenye hizo kampuni zisizolipa kodi na zisizotajika.
   
 10. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Yaani kampuni za simu hazilipi kodi? mbona kila tukipiga cmu tunaambiwa ni sh kadhaa kwa sekunde bila vat? ama kadhaa ikiwa na VAT? ama kodi ipi hiyo? au ina maana huwa tukikatwa zinapelekwa wapi? hapa nimelewa tafadhali mwenye kuelewa msaada...
   
 11. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mbona wanafanya heavy adverts ... wanatoa vijizawadi vingi tu na vijisafari ... this would not be a problem maana the company is big.

  Sasa inatubidi tuwashughulikie, sote wana JF tuungane tupige marufuku watoto, waume, wake, ndugu jamaa na marafiki kunywa coca cola ... huenda ikasaidia
   
 12. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hii habari ina maana kubwa sana. Ukiangalia inasema "Coca Cola hawalipi" halafu "Vodacom na Celtel wanalipa kidogo" ndio wanataka kusema Coca Cola hawalipi kabisaaaa!!!! Lakini kwa gazeti serious kama Habari Leo, hii habari ina mapungufu makubwa sana maana haina ufafanuzi wowote, hata kujaribu kumuuliza Hamad Rashid au hata watu wa TRA ambao walikuwapo hapo au Coca Cola wenyewe, ambao nadhani NINA HAKIKA WATAIBUKA NA TAARIFA KUBWA YA UFAFANUZI. Ninavyojua haya makampuni Vodacom, Coca Cola na Celtel ni walipa kodi wakubwa.

  Kuna takwimu halisi kabisa zinaonyesha kwamba Vodacom ni walipa kodi wakubwa na kama zikosei waliwahi kupata na cheti kwa ajili hiyo. Inawezekana kuna misamaha katika baadhi ya maeneo jambo ambalo nafahamu ndio ilikuwa theme ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi na hilo lilijibiwa na TRA waliosema kwamba wao hawajawahi kutoa misamaha bali Wizara ya Fedha ndio inatoa misamaha na wao wanasamehe kodi iliyoanishwa kisheria mfano Taasisi za Kidini na vitu ambavyo vimeondolewa kodi.

  Mjadala lazima uangalia kwa mapana badala ya kushabikia makosa kama haya ya kiuandishi usio na UMAKINI
   
 13. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2008
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,658
  Likes Received: 2,464
  Trophy Points: 280
  Halisi,

  kwanza nakushukuru kwa kutoa ufafanuzi huo,pili ningependa kujua ni kodi ipi inaongelewa hapa,mapato (income),vat,paye au?

  kwa sababu haiingii akilini kuwa vat tunayolipia katika huduma wao wasiiliope TRA,ukiachilia mbali income tax amabyo iko subject to abuse by those corporate chaps...au inawezekana vyombo vyetu vya habari vinafanya makosa katika kuripoti?
   
 14. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2008
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwangu haijalishi aina ipi ya kodi. Kwa nini hazilipwi? Makampuni haya yanatengeneza faida kubwa. Nadhani matatizo ni yetu wenyewe, tumeshindwa kusimamia na kufuatilia suala hili.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  inauma sana hawa TRA ukiwaona wanavyo nyanyasa wafanyabiashara wadogo utawaonea huruma.........kumbe giant companies wanakumbatiwa dah hii nchi bora kufa tu watu tumesha jikatia tamaa.
  Hayo makampuni kuna mikono ya watu wa serikali si bure wanakula tu 10% wote tunafahamu Rostam ana hisa Voda na Lowasa ALPHATEL. yaani wao tu kila kitu wao.
  Bora kufa tu ss wanyonge tutashika wapi?Kama kila kitu ni cha high class vibopa huko juu.
   
 16. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2008
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Halafu kina kada mpinzani wanataka tukae kimya!!
   
 17. T

  TrueVoter JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 870
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 80
  Ni mambo ya ajabu haya, pamoja na promotion nyingi za bahati nasibu za kipumbavu watu zaidi ya million mbili kugombea kagari kamoja kumbe hata kodi hawalipi!
  Hatuna serikali!!! TRA nao ni wajinga tu!!

  Wabunge warekebishe sheria zinazohusu mawasiliano! kampuni zote za simu zinazoendesha bahati nasibu, nusu ya kiwango wanachokusanya toka kwa wateja wanaocheza bahati nasibu lazima walipe kama kodi!!

  Siku hizi watu hata kazi za maana hawafanyi, kutwa kutuma message ashinde zawadi za bahati nasibu!! nchi imekwama hii!
   
 18. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Nahisi ni Zantel ambao Karume ana mkono wake pale na washikaji zake ama wewe unasemaje ?
   
 19. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #19
  Jun 5, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Zantel Haiwezi Kufanya Hivyo Hata Siku Moja
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  If these giant companies are not paying, from where does the govt get its revenue which is increasng every month?
   
Loading...