Wizi wa aluminium kwenye jimbo la Anne Kilango Malecela... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi wa aluminium kwenye jimbo la Anne Kilango Malecela...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngwendu, Dec 29, 2010.

 1. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wadau kuna taarifa kuwa kuna mtu mmoja anaitwa willy akishirikiana na foreigners wanachimba na kusafirisha aluminium kwenda Kenya. Inavyojulikana serikalini ni kuwa huyu mtu anachimba chokaa kuipeleka kenya lakini kiuhalisia ni kuwa kwenye magari yake chokaa inawekwa juu tu kuficha kilichopo ndani. Tafadhali kama kuna mhusika au kuna mtu yuko karibu na wahusika basi taarifa hizi zifanyiwe kazi. Sehemu yenyewe ni huko Ndungu milimani mkoani Kilimanjaro kwenye jimbo la mheshimiwa Anne Malecela. Sorry kwa kuileta hii thread kwenye jukwaa la siasa. Lakini mimi nimeichukulia kama issue sensitive inayogusa moja kwa moja masilahi ya taifa letu.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Evidence plse?
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kama unauhakika je umepeleka taarifa polic
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wakuu ni evidence gani mnataka tena. Nimesema kila siku magari yanapita kutoka ndungu milimani kwenda kenya yakiwa yamepakia alminium lakini juu yakiwa yamefunikwa na chokaa kama geresha. sasa ushahidi gani tena? assume mimi ni muajiriwa hapo. ningeadikaje? Na kwa nini niongope? kwa maslahi yapi? Nitafaidikaje?
  Narudia tena kama kuna mtu ana-access na wahusika akiwemo Mh Anne Kilango Malecela basi wataarifiwe.
   
 5. Muro

  Muro Senior Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Una uhakika huko Kenya inayeyushwa kuwa Alluminium? nakama ni kweli ina maana seikali yetu haijui?huyu Ndg ninavyomfahamu anafanya biashara ya mabati Arusha na Moshi na mabati anayachukulia Dar sasa hiyo biashara ya Alluminium kwanini aipeleke Kenya awache Dar anakochukuia mabati.
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu we niamini. Narudia tena kwamba hii ni taarifa wala tusilete ushabiki wa kisiasa kwenye issue serious ya uporaji wa rasilimali zetu. Please kwa ambaye ana access na wahusika let them know it.
   
 7. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  C uende polic au takukuru kama una uhakika?
   
 8. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2010
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Huyu vipi? Anakj kushtaki hapa kwenye JF? Nilifikiri anatupa taarifa juu ya hatua alizo chukua, any way wadau ujumbe umefika tuufuatilie
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,525
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  JF mbona inakuwa hivi? Mtu kaleta taarifa nyie mnamletea siasa, ndio maana mgao wa umeme unatupiga na tupo kama mikondoo tu. Kama kuna waandishi wa habari inabidi wafuatilie na kulipeleka hili swala kwenye vyombo vya dola. Sasa kama huyu mleta taarifa anaishi milima ya upare let say myamba. Kule hakuna vituo vya polisi wewe unayemshauri aende kituo cha polisi si uende wewe? Kwani wewe sio mtanzania? Kama huna cha kuchangia basi changia kuhusu dowans huko na mgoa wa umeme
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Biashara ya UCHIMBAJI 'HARAMU' TANZANIA si jambo geni sana kwa baadhi ya maafisa wetu serikalini.

  Kati ya machimbo hayo, uchimbaji wa URANIUM unaendelea na baadhi tu ya maafisa wetu wa pale TUME YA NUCLEAR pale Sayansi ndio wenye undani huo zaidi na ushiriki wa wataalam toka Iran.

  Hadi sasa shughuli za MACHIMBO ya aina hiyo yanaendelea nchini maeneo 7 kwa madini mbali mbali na kufanywa SIRI KUBWA wenye mali tusijue.

  Mara baada ya katiba mpya mengi tu ya uvunguni yanaanza kuanikwa mezani kwa faida ya Umma na ustawi mzuri wa taifa letu kwa ujumla wake.
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,525
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  kapime akili
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  SUbirini hapo EVIDENSI mtapakuliwa tu wakati mwafaka.
   
 13. B

  Bobby JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Ivuga na mtoa mada thanks a lot! Hivi JF tumekumbwa na nini mtu ameleta data tunamshushua sasa tunatakaje jamani? Mimi sijaenda huko lakini nimepigiwa simu na mtu anataka kukodi magari yangu kupeleka huo udongo kiwanda cha cement Nairobi. Kwa jinsi nilivyomhoji though ni kupitia kwa simu nahisi kuna mchezo mchafu unafanyika hapo kwa kweli. Hata kama ni chokaa I'm sure taratibu kibao zitakuwa hazifuatwi believe it or not. Mimi nitalifiatilia hili jambo kadiri nitakavyoweza then nitaleta feedback.
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu Wa-Tanzania KWA KUDAI EVIDENCE wakati mji unahamishwa?? Kwani na Tanzanite kuibukia Kenya kuongoza kwa export yake ilhali yapatikana Tanzania tu nako mliletewa evidence sio????????
   
 15. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #15
  Dec 31, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,994
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama utaweza kunipatia jina la pili la huyo Willy, itakuwa rahisi kulifutilia?
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Dec 31, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,145
  Trophy Points: 280
  ..suala hili linajulikana tayari. labda hatua ndiyo hazijachukuliwa.

  ..majuzi nimesikia Waziri Maige kamtimua afisa misitu wa wilaya.

  ..labda kilio hiki kipelekwe kwa Waziri mapema kabla hajaijua fedha na kuzama kwenye ufisadi.

   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Dec 31, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,145
  Trophy Points: 280
  ..naona hapa mwandishi wa raia mwema naye anaripoti suala hilohilo.

  ..inaelekea watawala wamekuwa wazito kuchukua hatua.

   
 18. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #18
  Dec 31, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Wana JF habari hizo tusizipuuzie kwani zinawafaidisha jirani zetu, huku Hombolo, Dodoma kuna kiwanda kinachotengeneza Wine na kilevi (alcohol) inayotoa Valuu inayonunuliwa na Konyagi.
  Kinamilikiwa na viongozi waandamizi wazawa na hisa nyingine inamilikiwa na M-Italia ambaye naye anachimba madini na kuyapeleka nje, wote tunamuona na nyumba yake ipo mlangoni mwa Chuo cha Serikali za Mitaa cha Waziri Mkuu.
  Tumenyamaza Je? tukashtaki wapi na Kituo cha POLISI kipo hapohapo ndege zinztua huko porini na kuondoka, anayebisha afike Hombolo.
  Milima hiyo kwa nyuma yake (kaskazini, unapoelekea Wilaya ya Kondoa haohao wa-Italia wakishirikiana na wa-Korea wananunua madini wanayoyaita Granite (yana rangi ya kijani) wanachimbua bila woga na vitalu wamenunua ofisi za Madini Makao makuu hapa Dodoma
  hivyo mdau ngwendu mwenye hii thread unaweza kukuta wanakibali kutoka Madini zaidi ya hapo tunaibiwa, kama vile Mpwapwa (dhahabu), Bahi (Uranium) Manyoni (dhahabu) WANAOHUSIKA TUOKOENI MADINI TUNAIBIWA KAMA BULYANKULU, MWADUI, MIRERANI NA KWINGINEKO
   
 19. K

  King kingo JF-Expert Member

  #19
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hao mnaowapigia kelele wachukue hatua hawana hata habari na wengine ndio wanashirikiana na hao wanaowabia madini/udongo wenu kama vipi chukueni hatua wenyewe..
   
 20. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #20
  Dec 31, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu huyo mtu na project zake anajulikana kama Willy Enterprises. Kibali alichonacho ni cha kuchimba huo udongo kama walivyoandika wengine humu ndani, lakini kiuhalisia kinachosafirishwa ni Allminium, na hiyo wanapakia toka juu milimani halafu akishuka huku chini kidogo anaweka huo udongo kwa ajili ya kuficha kilichopo ndani. Nawafanyakazi wote wanajua hilo dili linalofanyika.
  Kuhusi hizo habai za Dom, is so sad to me. Jamani wahusika wajibikeni, mbona uroho umezidi? Hivi jamani kwanza mnapata mishahara kwa kodi zetu sasa badala mtuhudumie nyinyi mnachofanya ni kutuibia? hivi nyinyi ni watu gani ambao hamridhiki? Hamna huruma na watanzania wenzeni ambao kupitia kwao ndo mnapata mishahara?
  Issue hizi za kijinga mziache ama sivyo nyakati zitawaachisha.
   
Loading...