Lazima tuendelee kuweka wazi kwamba ufisadi ulifikia hatua ngumu kabisa! Wakati kuna wanafunzi mamia wanakosa nafasi ya kulipiwa na bodi ya mikopo, sasa hivi vyuo vimeonyesha idadi ya wanafunzi hewa waliokuwa wakilipiwa na bodi ya mikopo. Kwa maana nyingine, wanafunzi wenye mahitaji walinyimwa mikopo na wasiostahili na au wasiokuwepo chuoni wakawa wanapewa mikopo.
Nimeangalia website ya chuo cha SUA inaonyesha takriban wanafunzi 400 wakiwa ni hewa. Maana yake ni kwamba pesa hizo zilikuwa zikifika chuoni na wahusika ktk chuo hiki waliziramba. Ni aibu zaidi kwamba hapo chuoni kuna wanafunzi wengi wasiyo na uwezo wanasoma kwa taabu kabisa kwa matatizo ya kifedha lakini wamenyimwa mikopo!
Naomba serikali isiishie kutaja majina ya wanafunzi hewa. Lazima wakuu wa vyuo hivi wawajibike na pesa hizo zirudishwe. Naamini pia pesa hizo zimeibiwa zaidi ya miaka 5 iliyopita. Ni muhimu kurudi nyuma na kuangalia kumbukumbu maana kuna watu wanadaiwa wakati hawajawahi kukopa toka bodi ya mikopo.