Wizi utabakia kuwa wizi tu hata uupambe kwa lulu.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Spika wa bunge Anne Makinda na waziri wa nchi sera na uratibu wa bunge Lukuvi, wametoe sababu mbali mbali kuhalalisha ulipwaji wa posho za vikao kwa wabunge. Pamoja na maelezo yao yote, suala msingi hapa ni kwamba kazi ya mbunge ni kushiriki kwenye mijadala ya mbunge na kamati zake; na ni kazi hiyo inayompa stahili ya kulipwa mshahara, na hivyo kuzidi kumlipa posho kwa kazi hiyo hiyo, ni kumlipa mara mbili kwa kazi moja, jambo ambalo ni wizi. Sina budi niseme kwamba kwa bahati mbaya imekuwa sasa ni tabia ya bunge letu kushiriki kwenye vitendo vya udanganyivu bila kujali nafasi lililonalo bunge katika ustawi wa nchi yetu. Chukua hili suala la lita 1000 za mafuta anayopewa mbunge kila mwezi kwaajili ya kutembelea jimbo lake. Wabunge wanalipwa mafuta kwa kutumia viwango vya shs. 2500 kwa lita. Kila mtu anajua kwamba pamoja na bei ya mafuta kuwa juu haijawahi kufikia huko. Sihiyo tu, hata wabunge wa viti maalum ambao hawana majimbo pamoja na mawaziri naspika mwenyewe ambao wakienda majimboni mwao wanatumia magari ya serikali nao wanalipwa posho kwaajili ya mafuta hayo. Kama huu si wizi ni nini!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom