mwisho2016
JF-Expert Member
- Jun 27, 2016
- 724
- 625
Kama mnavyofamu baadhi yetu tunatumia simu na vifaa vyao startimes na pindi kifaa katika simu kinapopata hitilafu naenda ofisi zao zilizotapataa kila mtaa wa majiji yetu.
Nimekutana na kitimbwi hiki makao makuu pale bamaga, kabla ya kwenda kununua Battery ya simu yangu ya startimes nilifanya uchunguzi kwa wapiga dili wa Battery za kuchonga kariakoo, nilichonga Battery bila mafanikio, nilipeleleza na-kuona maduka yao vipo vipuri vya bidhaa zao.
Lakini watu hawa wanaajili wezi, inashangaza sana unashawishiwa kiwizi, kijinga na ulaghai wa kipuuzi. Batteryile inauzwa sh 15000 za kitanzania. Hii ni bei ya Battery niliyopewa baada ya kuulizia kwenye maduka yao ya pembezoni, kabla nilipoamua kwenda Bamaga mkabala na TBC nilijua pale sitakosa kifaa hiki, nikashangazwa na kuambiwa tunauza sh 15000/- lakini mpaka jumatatu Battery zilizopo zinauzwa sh 25000/- mtu binafsi kazinunua anaziuza baada ya zile za ofisi kwisha..! maajabu.
Nikamwambia binti huyu asiyejua nini maana na madhara ya anachokifanya. Nikasema, sawa mimi nitakuja Jumanne najua sitakosa. Nikaenda Siku ya Jumanne, nilipaki Petro station nikatembea baada ya kuvuka barabara. Yule dada nikamkuta tena, akanipa jibu la utata tena, kuwa zimeisha, nikamwambia pana watu wananunua kwa jumla? akajikanyaga, nilikuwa nimeshika sh 15000/-
nikawaza je nikaongeze hii pesa ninayo kwenye gari ili niondoe usumbufu huu? au nisepe tu? Nikajipa moyo kwa kuwa hakuna walionunua kwa ajili ya kuuza mtaani. Nikaongeza 5000/ akaniuzia kwa 20000/- nikadai risiti akasema hii haina risiti.
Ndugu zangu watanzania sisi ni wa ajabu sana.
Star times wahusika liangalieni hili na mtoe fundisho magazetini. KWENYE mabenki yetu wafanyakazi wanaokosea hutolewa magazetini, wizi, kutokuwa waaminifu ni tatizo kwenye biashara zenu, nilivyoamua kuhamia samsung ilikuwa si mapenzi, niliipenda sana startimes bidhaa zenu lakini kwa kutokuwa makini, mtawakosa wengi