Wizi Ndsani ya benki! twafwa

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,161
Hii inaweza kuwa ya mwaka. Mteja mmoja wa benji ya azania bancorp amejikuta akiibiwa sh milioni 10 katika mazingira ya kitapeli akiwa ndani ya benki;
bwana huyo anasema kuwa aliingia ndani akiwa na mifuko miwili ambayo kila mmoja alikuw amehifadhi sh mil 10 kwa ajili ya kudeposit kwenye akaunti yake.
lakini wakaingia watu watatu, wakamzingira kila upande na kumuuliza maswali ya kumbabaisha wakati akiwa ameweka kifurushi kimoja cha sh mil 1o juu ya meza.
mmoja wa watu wale alijifanya kuulizia mambo ya kuweka hundi na mwingine alimuomba carbon paper. walipoondoka, kutahamaki, kile kifurushi chake alichoweka hakikuwa na fedha bali magazeti!
kali zaidi ni kuwa aliporipoti kwa uongozi wa benki na kuangalia security cameras, ingawa zilionyesha tukio zima, lakini hazikuweza kuonyesha sura za wale watu. kwa maneno ya mwathirika huyo, picha zilionekana kama vikaragosi hivyo alishindwa kuwatambua watu wale.
sijui kama watu wa Benki Kuu wameipata hii na wakakague hizo kamera kama kweli zinafaa kwa kazi hiyo. na si tu kukagua katika kabenki hako, bali ufanyike ukaguzi katika mabenki mengine kuona iwapo mifumo yao ya ulinzi inaendana na hali halisi.
Na hao azania watuambie inakuwa matapeli wanafanikiwa kuingia katika himaya yao na kufanya utapeli kama huo?
 
Duu!!!!
jamaa lazima apagawe. ila nadhani jamaa walishamsoma kwa muda mrefu sana.
vilevile, kama kamera zenyewe ndo zinafanyakazi hivyo, basi hamna haja ya kuziweka. au walinunua kamera feki ili wabaki na chenjii?? na hapo hasara ni kwa jamaa. inauma sana.
 
kamera hazina matatizo matatizo yapo ktk viwango vya hizo kamera
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom