Wizi na utapeli wa ubinafsishaji wa mashirika ya umma unaoendelea kufumbiwa macho na watawala: case study Kilombero Sugar Company.

Tomahawk

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
232
217
Habari wana jamvi, kwa mda mrefu kidogo nimejaribu kufanya uchunguzi kuhusiana na uuzwaji wa mashirika yetu ya umma ulivyofanyika miaka kadhaaa nyuma, nakiri wazi ubinafsishaji Ni Jambo jema kwa uchumi wa kisasa ila ulinde maslahi ya pande zote.

Kilombero Sugar company Ni muunganiko wa viwanda viwili vya sukari kwa maaaana ya ruhembe factory (Kilombero 2) na Msolwa factory (Kilombero 1). Miaka ya 1999 kuelekea 2000 ivi viwanda vilibinafsishwa kwa pamoja kwa kampuni Moja ya Afrika Kusini ikiitwa Illovo Sugar Group yenye makao makuu jijini Durban uko Afrika ya Kusini, ikisemekana ivi viwanda vyote viliuzwa kwa Bei ya kutupwa kwa pamoja ya Tsh Billion 18(hakuna ushaidi).

Baaada ya iki kiwanda kuuuzwa ikatokea fununu kuwa kilichouzwa Apo Ni kiwanda kimoja tu cha Kilombero 1(msolwa factory) na icho kingine Kuna wakubwa kadhaaa wamejimilikisha wa serikali ya awamu ya tatu uku Moja ya masharti waliyopewa wa Illovo Ni kwamba wakiendeshe kile kiwanda Kama Chao ila pesa iende kwa wakubwa usika. Labda kadhia iyo ya away wachache kujimilikisha icho kiwanda yaweza kuwa kweli kwa maaaana illovo waliwekeza tu kwenye kiwanda kile ambacho walichodai ndo wameuziwa iki kingine Wala hakuwa wakikijali Sana hata makazi yao yalikuwa kule kwenye kiwanda Cha Kilombero 1 na wakiweka kila aina ya miundo mbinu kwa makazi na biashara uku wakikichukulia poa iki Cha pili kwa maaaana Cha Kilombero 2.

Miaka ya 2000 wafanyakazi wakapunguzwa kulingana na matakwa ya wamiliki wapya...Cha ajabu mpaka Leo hiii watu hawajalipwa pesa zao. Inadaiwa waliopunguzwa walikuwa Kama watu 3000 ivi viwanda vyote viwili.....Mzungu kwa maaaana ya Illovo sugar Group ilikuwa iko tayali kulipa wafanyakazi wake wote wa kile kiwanda inachodaiwa wanakimiliki Cha Kilombero 1 ila wamiliki wa kiwanda Cha Kilombero 2 wale watawala fulani waliojimilikisha kile kiwanda wakawaambia wale wazungu wasiwalipe wale wafanyakazi wa Kilombero 1 kwakuwa wakilipwa wa Kilombero 1 wa kilombero 2 nao watadai wakati wale wamiliki weusi hawana pesa ya kuwalipa ivyo ingeleta purukushani....mpaka ninapoandika ivi Sasa tangia watu waachishwe kazi mwaka 2000 watu hawajalipwa mpaka Leo.....inasikitisha mno, na akitokea mtu yoyote wa kutaka kufuatilia ayo malipo anatulizwa anatulia tuli....alikuwepo mtu anaitwa Bashange alijitaidi kupigania iyo haki ya ao wafanyakazi kulipwa alivyotulizwa tulizwa anajua mwenyewe mpaka akakimbilia kwenye siasa za Chama Cha CUF uko, hakuna mbunge alieweza kuzungumza popote Ilo swala iwe bungeni ama popote pale maaaana anatulizwa kwakuwa INASEMEKANA iyo Ni ishu ya viongozi kadhaaa wa serikali ya awamu ya tatu, imepelekea iyo sehemu kuwa na upinzani mno kwa Chama tawala (CCM) mpaka kupoteza Jimbo husika, mbunge wa Sasa wa Apo Ni Joseph Haule (professor Jay).

Mwaka 2003 Illovo sugar Group ikauza hisa zake baadhi kwa kampuni ya Associated British Foods ya Uingereza lakini ilipofika 2006 Associated British foods ikanunua hisa zote za illovo sugar Group kwa maaaana Associated British foods ndio mmiliki wa Illovo na Kilombero sugar company.

Associated British Foods Plc inamilikiwa na Wakfu wa Wittington investment kwa asilimia 79 na asilimia 21 inamilikiwa na Wenston family ambao kwa pamoja wanamiliki Kilombero sugar company kwa asilimia 55 za hisa kupitia illovo sugar Group, wakati Kilombero sugar company inauzwa tuliambia illovo ndo wamiliki halali wa Kilombero sugar factories Sasa baadane nikataka kujua Kama 55% ndo inamilikiwa na Associated British Foods izo asilimia zingine ziko wapi??? Labda kwa kuwa wazungu sio watu wa maghumashi na kuweka data zao wazi ikapelekea mzalendo Mimi kujua izo hisa zingine ziko wapi????

Baaada ya utafiti nikaja gundua kuwa 45% asilimia iliyobaki iko ivi, kampuni inayoitwa ED & F MAN ya nchini Uingereza inamilikiwa asilimia 20 ya Kilombero sugar company na asilimia 25 inamilikiwa na serikali ya Tanzania.

Ni kajaribu kufuatilia hiii company inayoitwa ED & F MAN kimsingi habari zake hazieleweki siwezi nikaiukumu Moja kwa Moja ila inanipa mashaka.

Ikumbukwe habari zote za hisa izi imekuja kujulikana baaada ya raisi wa awanu ya nne ndugu Jakaya kikwete kutembeleea Apo kiwandani labda baaada ya kujuzwa Ayo madudu ya Apo na hatimaye Mambo yakawekwa Kama yalivyowekwa ila hakuna malipo bado ya wale wafanyakazi walioachishwa kazi mwaka 2000, hata mwezi wa tano mwaka huuu raisi Magufuli alipotembelea uko akuzungumzia chochote kuhusiana na habari ya icho kiwanda.

Bado Nina maswali kichwani mwangu:
1. Wapi ED & F MAN ilinunua izo hisa za 20% Kilombero sugar company???? Wakati Kilombero sugar company au Illovo haijawai kuwekwa kwenye soko la hisa la Tanzania??????
2.Kwanini wafanyakazi wale hawajalipwa mafao yao mpaka Sasa???
3.wakati wa mauzo ya Kilombero sugar company ilitajwa illovo tu wapi inatokea hiiii ED & F MAN???
Naendelea fanya utafiti na naruhusu kukosolewa kujuzwa kwa maaaana wote Ni wazalendo na tuna mapenzi na nchi yetu...

Nawakilisha.
 
Back
Top Bottom