Wizi na utapeli unaofanywa na wakongo kushirikiana na watanzania... TRA, Wizara mpo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi na utapeli unaofanywa na wakongo kushirikiana na watanzania... TRA, Wizara mpo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by stroke, Apr 19, 2012.

 1. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,406
  Likes Received: 6,595
  Trophy Points: 280
  Haya ni baadhi ya makampuni ya Congo DRC , yanayofanya utapeli kwa wageni wanaokuja kununua madini aina ya Gold, Copper cathodes,Tantalite na diamonds hapa nchini.

  Kwa kipindi kirefu sasa, wakongo wengi waishio hapa nchini wamekuwa wakifanya utapeli kwa kuwahadaa wageni kutoka nje kuwa wanahifadhi ya dhahabu nyingi, pamoja na copper cathodes hapa nchini, wamekuwa wakibadilisha mizigo baada ya kuwaonesha halishi na kuwapatia feki baada ya malipo kufanyika, watu hawa wana mitandao mikubwa sana , kuanzia bandarini, polisi, tra , viwanja vya ndege pamoja na sehemu nyingi tu muhimu..baada ya kufanya utapeli wao.hutoa sehemu a fungu kwa wahusika wote katika idara tajwa waliotoa misaada yao ya kufanikisaha biashara yao..hivi ndivyo hawa majamaa wanao jiita mapapaa hapa mjini wanavyoishi..kuendesha magari ya kifahari na kuishi maisha ya anasa ..kwa UTAPELI wakilindwa na baadhi ya watanzania wenye njaa..makampuni kama COMICO ( Congo minerals company) Mazengo Company ya Temeke, ne mengineyo mengi yamejaa matapeli wanaongiza mizigo ya madini kutoka kongo kwa njia za magendo kwa minajili ya kutapeli ama kuiuza bila kulipia kodi..kwa uchunguzi wangu nilioufanya kwa kipindi cha miaka miwili..nimegundua uoza wa ajabu unaondelea katika sekta ya madini..ni asilimia 20 tu ya wafanyabiashara hufanya biashara halali na kwa kulipa kodi wengine wote ni wezi tu..ufuatao ni mfano wa document wanazotumia hawa jamaa kufanyia utapeli wao.

  Ninachoomba ni kwa vyombo vya usalama, mamlaka husika kama TRA na uhamiaji, kusafisha idara zao kwa kufukuza wafanyakazi wasioitakia mema nchi yetu, kwa kuikosesha mapato na kukimbiza wageni wanaotaka kufanya biashara halali.

  Nawasilisha
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu lete basi utafiti ili nasi tujue nini ulikiona. Nilidhani ume attach document inayoelezea mchakato mzima, nakuta ni kabarua ka page moja. Kusema kweli sijapata mwanga ni jinsi gani wanafanya. Utafiti wa miaka miwili nilitegemea document lililosheheni nondo Mkuu.
   
 3. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,406
  Likes Received: 6,595
  Trophy Points: 280
  subiria mzee..hapa utapata kila kitu kwa hatua..naanza taratibu...huo mi mfano tu wa barua za kitapeli..ninazo document nyingi tu..passport copy zao na kila kitu wanachotumia..patience..
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Nadhani kwenye utafiti wako umeangalia pia namna Matapeli wanavyokwapua Mabilioni ya Mapesa kwenye Mabenki yetu chini ya ulinzi imara wa jeshi la polisi.
   
Loading...