Wizi mwingine huu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi mwingine huu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 16, 2007.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,814
  Likes Received: 83,212
  Trophy Points: 280
  ...Wabunge watatafuna pesa na hakutakuwa na ufuatiliaji wa maana kuhakikisha kama kweli pesa zimetumika jimboni

  Posted Date::10/16/2007
  Miswada mipya saba kusomwa Bunge lijalo
  Na Tausi Mbowe

  JUMLA ya miswada mipya saba inatarajiwa kusomwa kwa mara ya kwanza na mingine tisa ya zamani kujadiliwa katika kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Oktoba 30, mwaka huu.

  Miswada hiyo ni pamoja na mswada Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (Consituency Development Fund Act, 2007) ambapo serikali itatenga fedha kwa ajili ya kuendeleza majimbo.

  Sheria hii imeigwa kutoka nchini Kenya ambapo wabunge wake wamekuwa wakitengewa posho maalum kwa ajili ya kuendeleza majimbo yao.

  Miswada mengine ni Sheria mpya ya Kupambana na Kuzuia Ukimwi, muswada wa Nishati ya umeme na wa Usambazaji wa Mafuta (The Petroleum Supply Act, 2007).

  Mengine ni muswada wa Benki ya NBC, Muswada ya Fedha pamoja wa Taasisi ya Huduma za Uendeshaji wa Mashitaka nchini.

  Katika hatua nyingine, Spika wa Bunge, Samwel Sitta, alisema kuwa rasimu ya kubadilisha kanuni za bunge ipo tayari kuwasilishwa katika kikao kijacho.

  Sitta, alisema kuwa rasimu hiyo yenye jumla ya kanuni 153 ni sehemu ya mchakato wa marekebisho Katiba, itakayopelekwa kwenye kikao hicho kikatachoketi mwishoni wa mwezi huu.

  Spika huyo aliongeza kuwa hatua hiyo imefikiwa ili kwenda na wakati kutokana na kanuni za awali kupitwa na wakati.

  Alisema kuwa rasimu hiyo inatokana na mapendekezo ya wadau mbalimbali waliojadili kwa siku mbili na itapelekwa bungeni kwa ajili ya kupitishwa.

  Alizitaja baadhi ya kanuni hizo kuwa ni pamoja na Utaratibu wa Mbunge kutoa hoja, namna bunge linavyoamua mambo yake na utaratibu wa maswali katika vikao hivyo.

  "Huu ni muendelezo wa demokrasia, kumekuwa na lawama nyingi zinazohusiana na maamuzi ya spika, hivyo rasimu hii itaweka bayana majukumu ya kila mmoja wetu," alisisitiza Sitta.

  Wakati huo huo, Sitta alimtaka mfanyabiashara anayedai kutapeliwa na Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Mgana Msindai, kupeleka taarifa ofisini kwake ili mbunge huyo aweze kufikishwa katika kamati ya maadili kuhusiana na tuhuma hizo.

  Mbunge huyo anadaiwa kujipatia zaidi ya Sh191 milioni kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa mfanyabiashara, Joseph Mushi, anayeishi nchini China.

  "Mbunge akienda kinyume na maadili ya Bunge lazima achukuliwe hatua za kinidhamu, ikiwa ni pamoja na kumuita katika kamati ya maadili na ikithibitiska kuwa madai hayo ni ya kweli lazima sheria ichukue mkondo wake," alisema Sitta.
   
 2. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Katiba inapaswa kuandikwa upya, sio kuweka viraka kila uchao. Tushachoka.
   
Loading...