Wizi mpya kwa "spray ya kichina" Dar

Majoja

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
612
186
Wizi mpya umeibuka jijini Dar.
Wezi wanaigia na kupaki karibu sana na gari lako na kuchungulia umeacha nini garini.
Kama umeacha laptop umekwisha!!
Wanachukua "spray ya kichina" ambayo inapuliziwa kioo.Kioo hicho kina kauka(harden) halafu kikiguswa tu kina katika vipande vipande kama chembe chembe.
Wanaingiza mkono na kufungua mlango kiulaini sana na kuchukua wakitakacho.
Jana mimi nimelizwa!!!
CIMG0896.JPG
 
Mkuu mbona huu wizi hapa Dar una miaka! Mwaka jana mimi nimeona pale Kinondoni makaburi watu wanazika jamaa wanafanya wizi wao!
 
pole sana naona hata kama ni wa muda mrefu ila kwangu mimi hili ni tukio karibia la tano kusikia ndani ya wiki mbili tu
 
Ni team iliyoachwa na vijana wa Mahita, tutakoma kuwa na jeshi la polisi wenye maslahi duni
 
POle sana Majoja...

we should just kill those dudes who steal, inauma sana aisee
 
POle sana Majoja...

we should just kill those dudes who steal, inauma sana aisee

mimi binafsi nikimkamata nitamchinja ka kuku
nina hasira nao sana.
nimechunguza nasikia kuna baadhi ya wanamuziki wa kizazi kipya
wanamtandao wao.naendelea na uchunguzi ila ole wake atakaeingia mikononi mwangu!!
 
Wizi mpya umeibuka jijini Dar.
Wezi wanaigia na kupaki karibu sana na gari lako na kuchungulia umeacha nini garini.
Kama umeacha laptop umekwisha!!
Wanachukua "spray ya kichina" ambayo inapuliziwa kioo.Kioo hicho kina kauka(harden) halafu kikiguswa tu kina katika vipande vipande kama chembe chembe.
Wanaingiza mkono na kufungua mlango kiulaini sana na kuchukua wakitakacho.
Jana mimi nimelizwa!!!
View attachment 37095

Aisee shukuru sana MUNGU WAKO siku hizi wachache wanapuliza huwa wanaiba gari kabisa. Nitakuletea picha ya gari imeibiwa siku mke wa aliekuwa waziri mmoja serikali ya kikwete wakizika jamaa waliingia wakawasha a/c kwanza ikaonekana iko sawa wakaaga na kuondoka.

Hii wewe unaenda tu pale kwa wahuni kariakoo gerezani tena pata vijana wa nje muulize mpe namba ya gari yako ukanunue vilivyochukuliwa kwenye gari hivyo vya laptop labda tuwaulize BMTL kama wakiiba wanawapelekea kama gerezani ama lah ukavinunue tena.
 
Ni team iliyoachwa na vijana wa Mahita, tutakoma kuwa na jeshi la polisi wenye maslahi duni

Umeonaeeeh! Kijiwe chao ni Mango Garden na PR Camp K'ndoni. Wanakula na polisi, tangu miaka ya Babu Hita mpaka sasa.
 
pole sana naona hata kama ni wa muda mrefu ila kwangu mimi hili ni tukio karibia la tano kusikia ndani ya wiki mbili tu
Du! inaelekea mi ndo nimetembelewa, tena nje tu ya ofisi yangu.
 
Ni team iliyoachwa na vijana wa Mahita, tutakoma kuwa na jeshi la polisi wenye maslahi duni

na tibaigana alfred walichofanya ni kurithishana nakwambia hata alipoingia kova wakamwita mzee wakamsomesha na sasa kila ukisikia mamilion

yako mikononi mwa wazee wa kazi kova ana yake thamani
 
Mkikamata msiache kuchinjilia mbali.
Viribiti hawa washenzi kweli, ukipeleka polisi anaachiwa saa hiyo hiyo.

kuna mmoja alilamba laptop maeneo ya muhimbili, akaipeleka kuihifadhi kwa polisi pale kituo cha muhimbili geti la chuo, alivyoona vidume vimetembeza kitu kwenye sikio moja, akasema mwenyewe.
 
pole mkuu,tulishazoea kulizwa,kwa taarifa yako sifungi milango ya gari ili wasinitie hasara ya kununua kioo,lakini natoa kila kitu kwenye gari
 
Kwa mwenye kufahamu ... Hii "spray" ina matumizi mengine zaidi ya wizi? Au imekuwa "imported" kwa kazi hiyo tu?
 
Rip our mirror
jamani was so nice rest in peace
majoja hawa watu nunua spray moja inaitwa felcos nilinunua southafrica incase ukikutana na washenzi kama hawa unaspray unaingia kwenye gari wanatafutana ni balaa nilikuja nazo 5 moja imefanya kazi sana ikaisha wakati nikiwa
nahamia kwangu si unajua maisha nikaweka nyavu kwanza wakawa wanachana mmmh nikajipanga nikaanza kuweka madirisha ya CHUMBA CHANGU KWANZA ,siku inayofwata nikalala chumba cha wageni wakaja usiku nilispray kwenye macho mmoja kama sina akilinzuri haoni mpaka leo
na alikutwa asb pemben ya nyumba watu wamemzingira sikutaka hata kumjua..nikaenda job
 
Kuna maswali huwa najiuliza, Sierra Leone, Liberia wamepigana vita zaidi ya miaka 10 lakini ukiacha gari yako mtaani hata iwe miezi sita hakuna mtu atagusa, sasa sisi wazee wa nchi ya amani vipi???????? Halafu huu wizi wa vifaa vya magari, vitu ndani ya gari kwa bongo upo Dar tu, mbona mikoani hamna?
 
nitaleta maisha bora kwa kila mtanzania,nitazalisha ajira kwa vijana,naenda ulaya kuwatafutia mitaji.
 
Rip our mirror
jamani was so nice rest in peace
majoja hawa watu nunua spray moja inaitwa felcos nilinunua southafrica incase ukikutana na washenzi kama hawa unaspray unaingia kwenye gari wanatafutana ni balaa nilikuja nazo 5 moja imefanya kazi sana ikaisha wakati nikiwa
nahamia kwangu si unajua maisha nikaweka nyavu kwanza wakawa wanachana mmmh nikajipanga nikaanza kuweka madirisha ya CHUMBA CHANGU KWANZA ,siku inayofwata nikalala chumba cha wageni wakaja usiku nilispray kwenye macho mmoja kama sina akilinzuri haoni mpaka leo
na alikutwa asb pemben ya nyumba watu wamemzingira sikutaka hata kumjua..nikaenda job

Ha ha ha !
Du hapa Mkuu ulilamba dume.
Na mimi hasira yangu ingeisha.
Nitapata wapi hiyo felcos?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom