Wizi mpya Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi mpya Dar es Salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NATA, Jun 29, 2011.

 1. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kumeibuka maajamaa wanakaa karibu na maduka ya kubadili pesa na kurubuni watu kuwa wao wanarate nzuri zaidi.
  Ukikubali tu unapelekwa uchochoroni wanakupa makalatasi wanachukua dola zako. Au wanakunyang`anya pesa zako na kukuacha unashangaa.
  Hapo IPS kuna wapemba wanajitia wao ni waislam safi hawana dhurma usiwaamini kabisa!take care!
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kuna dada hapa kachukuliwa dola 700 zake hivihivi!
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Binafsi nashukuru sana kawa kunipa taadhari,kwani kuanzia sasa nitakuwa mwangalifu sana.However,Kichwa habari kingesomeka "WIZI MPYA DAR"it could make more sense.Asante mkuu!!
   
 4. Elizaa

  Elizaa Senior Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 160
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hawa jamaa miezi kadhaa walikaribia kumtapeli mme wangu. Walimkuta KCB ya posta akiwa anaulizia rate, wakamfuata na kuanza kuongea nae,

  wakaenda nae mpaka steers bahati nzuri wale waliotakiwa kulipwa pesa walishtukia wakaamua walipiwe kupitia account yao, kwa kuwa sisi hatuishi Tanzania ikawa imemponya. Lakini baada ya wao kuona dili imeshindikana wakaendelea kuongea wakapeana no za simu., mwezi watano nikaja huko dar, Mr akawa anasisitiza niwapigie hao jamaa maana rate yao ni nzuri, na walimwambia wanafanya kazi na wahindi wanaopeleka pesa kwa wafanya biashara wakubwa nje ya nchi. Nikawapigia, kweli swali langu la kwanza tu lilinijusha hawa jamaa ni matapeli


  Kwa kuwa sikuwa mwenyewe nikaamua niwaone sura. Nikafika steers nikakaa nje, ananilazimisha niwafuate. Jibu langu la mwisho niliwaambia kama mnabadilisha pesa , nifuante hapa KCB Bank tulipane hapa ndani na hiyo pesa nitaideposit hapo.

  Walikataa wanataka nichukue pesa niwafuate Exim Bank. Niligoma biashara ikaishia hapo. Ningefurahi sana kama kuna mwana jamii forum anaweza kuwafuatilia wakamatwe. Namba zao ni 0658242524.
   
 5. Revolution

  Revolution JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 567
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 60
  Huu wizi sio mpya sana, mimi walishawahi kunipiga dolar 100 maeneo hayo hayo kwasababu hiyohiyo ya kukimbilia rate nzuri, nilipofika maeneo ya corner ya nmb maeneo ya pamba road nikasema ngoja niangalie mzigo wangu mfukoni, kuchomoa...hamad!!! nikakutana na vocha za voda zilizotumika za 5000 ila wakati wanahesabu mkwanja nilikuwa ninaona elfu tano tano tena mpya tupu.....hii imenitokea mwaka 2009.

  Ni karibu na IPS building kama unakuja nmb kuna kichochoro kinaingia georgies bar au nbc club.
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hii kali kumbe wapo long. kwakweli ni hatari sana.
   
 7. F

  FUSO JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  Huu wizi si mpya, ulikuwapo miaka mingi sana anayeibiwa kajitakia mwenyewe kwa tamaa ya kupata zaidi. Tamaa mbele mauti nyuma. jamaa kama hawa walikuwepo pale monte carlo cassino opp. na life hse those days, waliwaliza watu wengi sana na mtindo wa kutaka rate nzuri ya dola.
   
 8. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Si tamaa mkuu ni kupunguza ukali wa maisha na kwanini kama kunanafuu uwende kwenye ghali?
   
 9. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kweli aina hii ya wizi siyo mpya. Mimi niliponea chupuchupu miaka 9 iliyopita
   
 10. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Basi watu wengi hawajui bado ndio maana wanazidi kulizwa!
   
 11. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  labda kwa lugha nzuri tuseme ni wizi wa zamani unaotumia mbinu mpya' it is new because you ever knew' au vp hapo??
   
 12. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,948
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni tamaa wewe unaona kuna bureua na mbao za matangazo zimewekwa rate zake kwa nini kama unahitaji rate nzuri usitembelee bureau mbalimbali na toka lini mtu binafsi akawa na rate nzuri kuliko bureau,hakika tamaa ikizidi mwishowe hupata hasara.Sidhani kama ukiingia bureau kuna mhusika atakutapeli kwanza hapo unapewa risiti nawewe unatoa kitambulisho chako,hayo mambo ya njia za mkato na kutaka kupata faida fasta ndio inakuwa imekula kwako,wabongo si wakuwaamini hata chembe ,biashara za vichochoroni zimepitwa na wakati,hii ndiop BONGO bana ni Nusu Nigeria
   
 13. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Huu wizi ni wa siku nyingi sana, enzi zile za Salamander na coffee bar iliyokuwa pale Extelecoms!.
   
 14. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #14
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  jamani kwani bank zetu hamzi amini?

  mimi huwa sifagilii wabadilisha pesa wa mitaani,huwa naenda NMB na CRDB,
   
 15. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 525
  Trophy Points: 280
  kwanini usiingie ndani ya bureu de change???
  Bure gharama
   
 16. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Mimi nasema hao yanayowakuta hayo astahili yao tena ndio baada ya kuwakuta warudi kuwa waaminifu. Wee Mabenki yote yaliokuwepo, maduka yote ya kuchenji fedha kihalali na receipt unapewa, leo huridhiki unataka kwenda vichochoroni? Inashangaza. Kweli aliyezowea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.
   
 17. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Ni kweli jamaa nimewapigia wamesema niwaone kesho wamenipa bei ya kuuzia leo ni shs/usd 1600 tena wamesisitiza kesho saa tano tuonane nao.Mimi ninasafiri kesho lakini kwa mzalendo yeyote kati yetu anaweza kufanya nao contact ili kutengeneza mtego wa polisi wako moto ile mbaya wame-insist niwapigie kesho same hr. hapo red ni kweli cm yao
   
 18. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  toka niingizwe mjini mara kadhaa sidhani kama kuna mtu ataniingiza tena mjini kiupumbavu pumbavu, labda atumie teknolojia ya computer kuniibia. infact kwenye hela simuamini mtu tena.
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mbona huo utapeli upo siku nyingi .sSio mpya kabisa tena mitaa hiyo hiyo ya IPS na wengine Samora
   
 20. Elizaa

  Elizaa Senior Member

  #20
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 160
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Natamani sana wakamatwe maana mtandao Sao ni mkubwa sana.
   
Loading...