Wizi mkubwa Wizara ya Nishati na Madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi mkubwa Wizara ya Nishati na Madini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by frema120, Jul 5, 2012.

 1. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,103
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Habari JF,

  Majuzi kulitokea wizi mkubwa sana katika wizara hii, saa tisa usiku walikuja watu na gari wakaingia ndani na wakati nje kuna watu wa tanesco emergency, wezi wakabomoa milango takiribani yote na baadaye kuiba na kuondoka.

  Cha kunishangaza hakuna taarifa ya kipolice, vyombo vywa habari n.k
  na inavyoonekana wamechota mapesa na document muhimu!

  JE, TUTAFIKA KWELI?

  SOURCE: Mimi mwenyewe nipo jirani na wizara hiyo.
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Si ajabu wakakana kuibiwa, sijui nayo ni siri?

  Nini kinadaiwa kuibiwa? Huna tips za kilichoendelea hadi sasa? Hao watu wa Emergency, hawakuona tukio likitokea? Kwanini hawakuwasiliana na Polisi? Ujasiri wa wezi utakuwa umetokana na nini?
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Huenda ni hujuma kubwa inayoendelea kufanyika ndani ya serikali ya JK kutokana na maadui wengi ndani na nje ya serikali. Dawa ni kuwaweka kando wote, tuweke misingi mipya ya taifa letu!!

  Inapofikia wakati hawawezi hata kusema wameibiwa sababu ni aibu, na huenda ingezidisha maumivu zaidi kama wangetoa taarifa kwa umma.
   
 4. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Tanzania tubaki kuhesabu ufisadi wizara hii! wizara ile ? wizi hapa wizi pale! hawa wameweka pesa uswis! hawa wameuza wanyama hai! hawa wamefisadi radar!epa richmond!n.k pia tubakie kutaja tanzania imebarikiwa wanyama pori, mlima mrefu, maji mengi, madini, ardhi, amani, vivutio vya utalii n.k kama hatutachukua hatua stahiki hakuna haja kulist hayo yote sana sana tunazidi kujisononesha tuu wakati wao wanatuona sisi wajinga wapiga kelele tuu!
   
Loading...