Wizi Mkubwa Ukarabati wa Flati za NSSF

kishegheni

Member
Mar 6, 2012
21
85
Kule Masaki NSSF wanafanya ukarabati mkubwa wa gorofa zake. Ukarabati huo unahusisha uvunjaji na kubadilisha madirisha na magrill, kupaka rangi n.k. lakini kazi hii wanaifanya wenyewe hawakumpa Contractor wala hakuna usimamizi wa injinia wa majengo mwenye ujuzi, wanatumia vibarua wa mitaani ambao nao pia hawana vifaa vya kujikinga. Ukiingia getini utaona uwanja umegeuka karakana ya ujenzi kwani hata vyuma vya grill na vioo vinachomewa hapo bila tahadhari yoyote.

Kibaya zaidi ujenzi huu mkubwa unafanyika bila tahadhari yoyote huku wapangaji wakiwa ndani ya nyumba hivyo kuhatarisha maisha na afya za wapangaji pamoja na familia zao. Vile vile hawana kibali cha Ujenzi cha Manispaa ya Kunondoni kwani hakuna Bango lolote linaloonyesha kua kuna ukarabati, namba ya kibali, jina la mkandarasi na jina la msimamizi.

Inasemekana fedha ya ukarabati zilishatolewa muda mrefu mwaka wa fedha ulioshia 30 Juni, zimetumika ndio maana wanafanya ukarabati wa kubabaisha bila kutumia mkandarasi kama inavyotakiwa kwenye ujenzi mkubwa kama huu.

Tunaomba Serikali na Taasisi zinazohusika, Manispaa ya Kinondoni, PCCB, OSHA, Wizara ya Nyumba na Makazi watusaidie kwa ajili usalama wa wapangaji.
 
E0NhMwdXIAAW0HL (1).jpeg
 
Acha ujinga umekosa tender unakuja jf kutujaza ujinga
 
Hujaonesha wizi wowote bali umeonesha kuwa unayo malalamiko ambayo kimsingi hujaweka facts
 
Back
Top Bottom