Wizi Mkubwa Tunaofanyiwa na Mamlaka za Maji Mjini

Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,315
7,113
Ndugu wataalam wa sheria naomba mnisaidie.

Nimekuwa nikiletewa ankara za maji ambazo ni wazi kabisa kuwa zimekaa kiwizi wizi vile. Kila nikienda kulalamika wananiambia hayo ndiyo matumizi yangu nikiwaomba waje waangalie dira yao huenda ni mbovu hawataki.

Matumizi yenyewe yale ya ndani tu eti inafikia lita karibia 2,000 kwa siku (yaani mapipa 10), nimewalilia sana na kuwaambia niefanya audit kwenye mfumo mzima wa maji pale nyumbani kwangu hakuna bomba linaliovujisha maji inakuwaje ankara kila kukicha inapanda tu? Sijapata msaada wowote kutoka kwa hawa wataalam wetu ambao ndo tunawategemea maana siyo wote tumesomea mambo ya maji. Nilichoamua kukifanya napanga kununua tanki la lita 1,000 ili nilijaze chini ya usimamizi wangu mwenyewe nione dira yao itasoma lita ngapi hadi litakapojaa.

Sasa nikiona hiyo dira inasoma lita 2,000 na huku ilipaswa kusoma lita 1,000 (kitu ambacho nahisi hawa jamaa kabla ya kuzigawa hizo dira kwa wateja huwa wanazichakachua), kuna sheria yoyote itakayonisaidia kuishitaki mamlaka ya maji safi (kama yapo) na maji taka mjini kwetu?

Naomba msaada wenu wakuu!!!!!
 
Back
Top Bottom